Haya ni kijijini kwetu, je kwenu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ni kijijini kwetu, je kwenu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Feb 4, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Niko kijijini kwetu kwa vacation nilikuwa sijafika kwa miaka 2 nimefurahi kukuta maendeleo ambayo ni mazuri kwa mfano barabara ina kiwango cha lami hadi karibu na mpakani.

  Ila kilichonishangaza ni hizi nyumba za kifahari kali kuliko hata baadhi ya nyumba za maeneo ya masaki na O'bay ambazo hazina wapangaji wala mtu anayeishi, unakuta nyingi zina babu na bibi ambao wanafanya usafi na kuitunza. Kwa mtazamo wangu tungejenga rum 2/3 kwa ajili ya siku kuu za xsmas na mwaka mpya na hizo hela zikafanya mambo mengine. najua huku kuna mashule na hospital basi tusaidie wengine/wa eneo tofauti. Baadhi ya hizi nyumba zingekuwa zinabebeka zingekuwa dispensary maeneo mengine au hata hospitali za rufaa.

  Hapa kijijini kwetu raha kweli ukiwa padre unaheshimika kuliko hata waziri wala mmbunge. Ukisoma seminary ukaacha unaweza pewa radhi na bibi yako...huku padre anaitwa mopiaa....raha kweli.

  Kuna makanisa yenye kengele ambazo ingekuwa dar ikipigwa ule mchana kwa mfano st. Peters wangesikia hadi bagamoyo. Ikipigwa hata kama mtu anakunywa/ria pombe ya mbege anaacha na kusali sala ya malaika/anjelusi hata kama amelewa ulevi unakata then unarudi upya baada ya sala.

  Kijijini kwetu kweli raha bado mambo ya ndizi na matunda.  Kilichonishangaza zaidi ni kuwa makao makuu ya mkoa kuna gym 1 tena ina masharti magumu sana kuweza kufaidi huduma hio. Zilizokuwepo zote zimefungwa na sijapata sababu ya msingi ila nahisi ni demand kuwa ndogo.

  Je kijijini kwako?
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,107
  Trophy Points: 280
  Kijijini kwenu safi ile mbaya.
  kijijini kwetu vijana wote wamekimbilia kwenye miji mikubwa kufanya biashara ndogondogo.
  kwetu kijijini, ardhi yenye rutuba amepewa mwekezeja ambaye alitudanganya kutujengea shule na zahanati, lakini hajafanya hivyo.
  Mkimuuliza mwenyekiti wa kijiji unatupwa kwenye rumande iliyoko kwenye jengo la mahakama ya mwnzo, na ili uachiwe ni lazima utoe faini ya kuku au bata.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,478
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Kwetu barabara ya lami haijafika,ila inapitika mwaka mzima,hatuna mwekezaji ila tumewekeza wenyewe. Shule yetu ya kata ni miongoni mwa shule bora kabisa ktk mkoa wetu. Kilichoniacha hoi ni namna walimu wa shule hiyo walivyopokelewa, walipewa chakula cha mwaka mzima na wanakijiji. Kijijini kwetu ukifika toka safari vijana huona fahari kukupokea mizigo na kukufikisha kwenu salama.

  Nyumba za kwetu ni za matofali ya kawaida na kuezekwa kwa bati. Mbunge huwa anapitapita mara kwa mara. Kipo kituo cha afya ila umeme haupo. Matunda ni ya msimu.
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kijijini kwetu vumbi mpaka ndani ya nyumba
  watu wanakata miti hovyo hovyo karibu patafanana na jangwa la Kalahari
  Kijijini kwetu umeme tunauona kwa mbali (mission/kanisani) pity

  maji ya bomba ni ndoto ya mchana, mtoni penyewe watu wamelima miwa na nyanya

  hakuna mamlaka za kudhibiti uharibifu wa mazingira!!!!!
  kijijini kwetu maisha ndo hayo na karibu watajitangazia rais wao na dola yao!!!!!!!
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha ha, kijijini kwetu kuna mgambo wakali na uizi umezibitiwa huku ukitaka kifo gusa shamba la mtu bora uguse chochote kuliko shamba lake. Mazingira yametunzwa vizuri sana.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,107
  Trophy Points: 280
  Hicho kitakuwa siyo kijiji ila Jamhuri iliyoasi na kujitenga.
   
 7. l

  libaba PM Senior Member

  #7
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hongera kwa hicho kinachoitwa maendeleo, ila katika ziara yangu yakutembelea mkoa wa morogoro mwaka jana mwishoni ilinifikisgha wilaya ya Ulanga, katika mji wa Mahenge ndipo nilipokutana na nyumba isio kaliwa wala kuishi mtu, ni nyumba nzuri ya aina yake, nikauliza mbona hii nyumba imezungukwa na majani...nikaambiwa mwenyewe amewekwa ndani , na anakabiliwa na kesi ya uhujumu, mtu huyo anaitwa Liyumba alikua mkurugenzi wa BOT
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,107
  Trophy Points: 280

  kwani asuingewekwa ndani ndio angekuwa anaishi kwenye hiyo nyumba?
   
 9. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  dah umenikumbusha mbali kweli,
  kijijini kwetu ahueni kwa sasa kuna maji ya bomba na umeme hili likuja baada ya wananchi kukigomea CCM kwani maji yaliletwa na mkoloni kipindi hicho, barabara ilikuwa haipitiki,Vuguvugu la upinzani lilipokuja wanakijiji wakahamua kuhamia upinzania kwa muda wa miaka 15, katika harakati za kulikomboa jimbo tukaletewa maji, umeme, na nimajuzi tu niliona tangazo la zabuni ya kujenga barabara yetu kwa kiwango cha lami.

  chakusikitisha vijana wadogo wapo kama wazee sasa wanakunjwa gongo, lishe duni na chakusikitisha maambukizi ya ukimwi ni ya kutisha kwani akitokea binti alikuwa mjini akarudi kijiji, sio wazee, vijana wanajichukulia na swala la condom ni dhambi na wala hazipo.sijui bomu litakapoanza kulipuka kama kijijini kwetu kutabakiwa na watu hususani vijana
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kijijini kwetu maji kila nyumba kwa sasa na yanapatikana wakati wote..Suala la kulipa bill ndo lilitaka kuleta utata kwa wazee hawajazoea kulipia maji maishani kwao. wanaamini ni bidhaa ya bure toka kwa mungu.

  Barabara inapitika hata wakati wa mvua na tetesi huenda ikatengenezwa kiwango cha lami kama tutachagua chama chenye dola...

  Shule zimeongezeka na idadi ya vijana wanaosoma ni kubwa na kujiunga na vyuo vikuu nchini.

  Wanywa pombe aina ya gongo wanaongezeka na vijana wengi kujihusisha na udokozi/wizi.

  Mahudhurio ya kanisani kila jumapili bado ni makubwa pamoja na kanisa kuwa mbali na kutokuwa na kigangoo..

  Tuliotoka Dar na maeneo mengine tukionekana weneyeji wanafurahi na kutuomba chochote hasa pombe aina ya mbege, beer na pesa.

  Majadiliano ya kisiasa na mustakabali wa nchi yameshamiri na Zitto Kabwe ni miongoni mwa wanasiasa maarufuu akimfuatia MZEE WA KIRARACHAAA.
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,112
  Likes Received: 2,411
  Trophy Points: 280
  Hii ni hatari sana kwa vijiji vingi vya Tanzania hasa maeneo ambayo yanatoa wasichana wengi wa kazi (Maids) mijini. Wakirudi vijijini inakuwa balaa, wenye tuhela na wasonazo wote watataka 'kumpitia'! Inatisha sana.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Hongera sana ndugu yangu. Unaweza kuwa na amani kwa kuwa umeongea na watu wa JF, kwani uko salama. Vinginevyo ungejikuta umeshikiwa mikuki kurudisha pesa za watu wakidhani kwamba ziliibiwa kwao zikajenga kwenu!

  Seriously, kama kwenu kuko hivyo basi ni Geneva ya Tz. Sie tumezoea ukienda kijijini unalala kwenye kibanda na humo humo kuna kuku, mbuzi, ng'ombe etc. Kiboko yake ni viroboto na kunguni. Nyie mmebarikiwa kuliko wanaume na wanawake wote wa nchi hii!!:rolleyes:
   
 13. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dark City, hard work pays. Kijiji changu ni kama cha akina Nguli, hakuna pesa iliibiwa mahali. Ni watu kujituma tu. Sasa utasema kijiji flani watu wanalala na mifugo na kung'atwa na kunguni/ viroboto kweli ni hadi aje mtu wa nje au hadi hela iibiwe sehemu?

  Wafundishe wanakijiji hao uchapaji kazi na kujituma
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  @nguli
  mkuu umeniacha hoi alafu sikujua kama na ww ni mchaga yani kama ukienda machame uuwiiii yaniutashindwa kuelewa kama upo kijijini utafikiri upo obeyi tatizo kijijini kwetu vijana wamepungua sana na wapo busy sana kuchimba makaburi karibu kila siku watu wanapandishwa kuzikwa kwenye nyumba ya milele
   
 15. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #15
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,318
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  kijijini kwetu tunatumia mabomba ya kupump, tunayaita "mdundiko"; muda wote utakuta ndoo zipo kwenye foleni, yaani wamama kule wakiamka tu wanafikiria kupeleka ndoo bombani kuweka foleni then wanarudi home kuendelea na shughuli mpaka zamu yake ifike.
  ninachofurahia nikiwa kule unaweza ukakaa wiki 2 bila kutumia hela, unakula chakula kizuri na kulala, utatoa hela kama unataka kununua pombe.

  pia wazee wa kijijini kwetu wakarimu sana, kila mzee/mmama akijua tu wewe ni mtoto wa fulani atakukaribisha nyumbani na kukuchinjia kuku, na kwa mila za kwetu yule kuku lazima ummalize, usipomaliza unafungashiwa uende ukamle baadae; ha ha haaaaaaa, raha tupu
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nguli,

  Kwetu mzee bila kuwa mgumu huwezi kwenda kusalimia - ni km kama 1000 hadi napoiacha barabara kubwa ya lami, then nakwenda km zingine 450 hadi kijijini kwetu, hii barabara ni mbovu saana - vumbi, mashimo na matope wakati wa masika usipime - average ni km 15 hadi 20 kwa saa ukiwa dereva mzuri.

  Nipo jirani sana na waziri wangu mkuu, toka kijijini kwetu hadi kwao ni kama km 90 kwa upande wa pili - ambapo unaweza kupiga kwa baskeli tu na ukafika.

  Kwetu bwana hali ni MBAYA SANA, vijana wamekata tamaa wanakunywa pombe za kienyeji - "ngogo" ambapo chupa ya orange inauzwa sh 500 na ndogo ya soda sh 250.

  Class mates wangu washakuwa wazee, si kwa umri ila shida walizonazo - wasichana wa wakati ule tuliosoma shule pamoja sasa ni wabibii - hawa ndiyo wanaochuja gongo kuwauzia wenzao, ili zoezi nzima la kugawana umaskini likamilike.

  Kijijini kwetu umaskini ni wa wote, hakuna nyumba nzuri watoto ambao tulibahatika kupata elimu hii ya kambarage ya bure kawaida hatutaki kurudi kuwekeza sehemu isiyo na barabara wala chochote cha kutega uchumi, kwa hiyo tumengagania mjini kujaribu kujikimu ki mtindo mtindo.

  Ila kwetu bia na soda hukosi, zinauzwa ingawa bei ni mara mbili ya ile ya mkoani, zinawekwa kenye chungu maalum kwa wale wanaopenda za baridi, kuku wa kienyeji eg jogoo kubwa ni sh 1200, nyie huku mnauziwa hadi sh 15,000k. kwetu bwana kuku hata kila siku ukitaka.

  Kwetu bwana usafiri ni alfajiri na BASI lipo moja tu linaondoka saa 10 na nusu – ukipenda usingizi wa asubuhi inakuwa imekula kwako linakuacha hadi kesho yake tena, nauli ni kubwa mno kiasi watu wanashindwa ku afford badala yake wanatumia baskeli na gari la ngombe - ni km 450 hadi mkoani – siku za mwisho wa mwezi linajaa sana maana walimu, manesi, bwanamganga, bwana mifugo wote ndani ya basi letu mjini kuchukua mshahara – kasheshe kupumuliana manake wengine wanakuwa wamelala nazo tena za kienyeji – mmhhh.

  Mafisadi wa kule ( wenye nazo) ni waalimu, bwana mganga na wale wenye viosks, kweli hali ni ngumu mno - kwa mfano ukienda likizo ukamaliza pesa zako hadi nauli basi itakuwa imekula kwako maana hakuna benki kule mpaka usafiri hizo km nilizokwambia.

  Kule kijijini kwetu bwana tuna shule ya sec ya kata moja ambapo kuna watoto wa ndugu yangu wanasoma pale, yupo mmoja form four nikamuuliza vitu basic tu hajui chochote hata test tube hajawahi kuiona.

  Bwana kule kwetu ardhi ni bure kabisa ila haina rutuba - watu wanajaribu kulima tumbaku, mahindi, karanga, alizeti ila kwa heka moja ukipata gunia mbili ujue una bahati sana chief, hali ni mbaya sana, hakuna matumaini yoyote kwenye hiki kilimo.

  Kijijini kwetu hakuna umeme, kwa hiyo nilivyokuwa huko nilikuwa naenda kwenye mnara wa celtel ili kucharge simu yangu ya nokia – bahati huduma hii ya simu imetufikia, nawapongeza sana hawa jamaa – mkiwaona wapeni big up.

  Ukipata nafasi wakuu, njooni mtutembelee huku kijijini kwetu ili kama ikiwezekana tuugawane umaskini pamoja.
   
 17. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145


  nimependa kjijini kwenu uwezi kunitambulisha kama mwanafamilia wenu na mm nikafaidi kuku wabure mh
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,318
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Karibu sana drphone, ukweli utakula kuku mpaka ukumbuke mboga za majani, maana kijijini kwetu mgeni hapewi mboga za majani mpaka aombe
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kijijini kwetu hakuna mabadiriko sana tangu nilipoondoka miaka 4 iliyopita. Lakini kubwa nililoona kuwa kuna ongezeko kubwa la watu. Kwani kutokea makao makuu ya wilaya kwenda kijijini kwetu usafiri bado ni ule wa Mandolin (Landrover 109) na kutokana na wingi wa watu gari hii hubeba watu mpaka sehemu ya mbele ya gari kwa nje (kwenye boneti) na dereva anaachiwa kajinafasi tu ka kuona njia.

  Kijijini kwetu umeme bado ni hadithi kubwa, lakini kuna bwana mmoja nimeambiwa ni nduguye "Mathawe, Temba, Mushi na Kimario" jamaa ameweka jenereta yake na kila siku usiku hufanya maonyesho ya sinema kwa kiingilio cha sh.200 kwa kila mtu. Pia huyu bwana amefanya watu wa kijijini kwetu kupata bia na soda za baridi kwa kuwa ana jokofu linalotumia nishati ya mafuta ya taa.

  Kijijini kwetu maji ya kunywa, kuoga na kufua ni yale yale ya rangi ya madhiwa (maji ya kisima) na ili kuwza kupata angalau ndoo 2 shurti uamke saa 10 usiku.

  Mawasiliano bado ni tatizo nimeambiwa kijijini kwetu ukitaka kuongea na simu au kupigiwa simu kwa muda ulioahidiwa basi unatakiwa kwenda kwenye kichuguu mbele ya nyumba ya mwalimu mkuu, ingawa nimesikia kuwa huyu mwalimu ameamua kufunga mbwa ili kudhibiti udokozi maana juzi juzi aliibiwa gunia la mtama na anahisi ni wale wale wanaojidai wanakwenda kutafuta mawasiliano.

  Nilibahatika kukutana na mbunge wa jimbo letu na katika mazungumzo huyu bwana hakuzungumzia kabisa jinsi anaweza kutuletea maendeleo kijijini kwetu zaid ya mikakati aliyonicholea ya kutaka kutetea kiti chake kwa kuwa tu amesikia kuna watu wanataka kugombea nae.

  Kimsingi kijijini kwetu hata suala la afya bado kabisa kuna mzee Madaraka ambaye tangu nikiwa mdogo nilikuwa namfahamu kwa kuwatibu watu kwa dawa za mitishamba ndio mpaka leo anaendelea kuwatibu watu.Zahanati iko takribani kilometa 5. Pale kwenye shule mwalimu mmoja ambaye tulisoma nae shule ya msingi ananiambia kuwa shule ina mwaka wa 6 haijatoa hata mwanafuni mmoja kwenda kidato cha kwanza. madai yake ni kuwa serikali imewavunja moyo kiasi kwamba morali ya kazi hakuna. Mwisho wa mwezi mshahara ukitoka walimu wote wanakuwa makao makuu aya wilaya kufata mishahara shule inasimamiwa na mwenyekiti wa kijiji iliupokea wageni wanaoweza kuja shuleni.
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hebu niambie kwanza kijiji kwenu ni wapi halafu ndo nianze kujadili.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...