Haya ni kijijini kwetu, je kwenu?

Si kijijini kwetu bado hakuna maendeleo kabisa.
Watu wanajenga mijini tu huko kijijini wanasema bush watapoteza pesa ajenge nyumba wakati anarudi kwa mwaka mara 1 napo x.mass tu
 
Karibu sana drphone, ukweli utakula kuku mpaka ukumbuke mboga za majani, maana kijijini kwetu mgeni hapewi mboga za majani mpaka aombe

yani nashukuru mkuu ninaitaji kwenda vakesheni la 2wiki nitakutafuta mkuu da mm na kuku damudamu
 
Kijijini kwetu hakuna mabadiriko sana tangu nilipoondoka miaka 4 iliyopita. Lakini kubwa nililoona kuwa kuna ongezeko kubwa la watu. Kwani kutokea makao makuu ya wilaya kwenda kijijini kwetu usafiri bado ni ule wa Mandolin (Landrover 109) na kutokana na wingi wa watu gari hii hubeba watu mpaka sehemu ya mbele ya gari kwa nje (kwenye boneti) na dereva anaachiwa kajinafasi tu ka kuona njia.

Kijijini kwetu umeme bado ni hadithi kubwa, lakini kuna bwana mmoja nimeambiwa ni nduguye "Mathawe, Temba, Mushi na Kimario" jamaa ameweka jenereta yake na kila siku usiku hufanya maonyesho ya sinema kwa kiingilio cha sh.200 kwa kila mtu. Pia huyu bwana amefanya watu wa kijijini kwetu kupata bia na soda za baridi kwa kuwa ana jokofu linalotumia nishati ya mafuta ya taa.

Kijijini kwetu maji ya kunywa, kuoga na kufua ni yale yale ya rangi ya madhiwa (maji ya kisima) na ili kuwza kupata angalau ndoo 2 shurti uamke saa 10 usiku.

Mawasiliano bado ni tatizo nimeambiwa kijijini kwetu ukitaka kuongea na simu au kupigiwa simu kwa muda ulioahidiwa basi unatakiwa kwenda kwenye kichuguu mbele ya nyumba ya mwalimu mkuu, ingawa nimesikia kuwa huyu mwalimu ameamua kufunga mbwa ili kudhibiti udokozi maana juzi juzi aliibiwa gunia la mtama na anahisi ni wale wale wanaojidai wanakwenda kutafuta mawasiliano.

Nilibahatika kukutana na mbunge wa jimbo letu na katika mazungumzo huyu bwana hakuzungumzia kabisa jinsi anaweza kutuletea maendeleo kijijini kwetu zaid ya mikakati aliyonicholea ya kutaka kutetea kiti chake kwa kuwa tu amesikia kuna watu wanataka kugombea nae.

Kimsingi kijijini kwetu hata suala la afya bado kabisa kuna mzee Madaraka ambaye tangu nikiwa mdogo nilikuwa namfahamu kwa kuwatibu watu kwa dawa za mitishamba ndio mpaka leo anaendelea kuwatibu watu.Zahanati iko takribani kilometa 5. Pale kwenye shule mwalimu mmoja ambaye tulisoma nae shule ya msingi ananiambia kuwa shule ina mwaka wa 6 haijatoa hata mwanafuni mmoja kwenda kidato cha kwanza. madai yake ni kuwa serikali imewavunja moyo kiasi kwamba morali ya kazi hakuna. Mwisho wa mwezi mshahara ukitoka walimu wote wanakuwa makao makuu aya wilaya kufata mishahara shule inasimamiwa na mwenyekiti wa kijiji iliupokea wageni wanaoweza kuja shuleni.

so interesting na huyo mbunge anawadanganya nn tena ili aweze kupata kula yani amwoni hicho ni kipimo tosha cha kumjima kura jamani tuamke sasa watanzani tumia nafasi hiyo kuwaelimisha wanakijiji wenzako
 
Nimefurahi sana kusikia habari za vijiji vingine vilivyo nilikuwa nacheka sana na sehemu nyingine nimesikitika kwa mfano swala la watu kuzika kila siku ni la kweli na hata hapa kijijini kwetu naona limeshika hatamu.

Wapi Xspin na Sipo sijapata za vijijini kwenu.
 
@nguli
mkuu umeniacha hoi alafu sikujua kama na ww ni mchaga yani kama ukienda machame uuwiiii yaniutashindwa kuelewa kama upo kijijini utafikiri upo obeyi tatizo kijijini kwetu vijana wamepungua sana na wapo busy sana kuchimba makaburi karibu kila siku watu wanapandishwa kuzikwa kwenye nyumba ya milele

Woo Dr, neewe ni Mmashami da? Mbakwi?
 
Aisee wewe lazima utakuwa unatoka mkoa wa Kagera, mambo ya Kanyigo nini?
 
Jamhuri ywa watu wa Mbeya tupo juu zaidi nitkupa baadhi ya Mikoa kwenye Jamhuri yetu, Mkoa wa Kyela pale tuna kituo bora kabisa cha mabasi kuliko Ubungo na Soko letu pale ni kubwa kuliko Kariakoo na isitoshe tuna Kyela FM na internet cafe nyingi. Una cha ziada?
 
Nimefurahi sana kusikia habari za vijiji vingine vilivyo nilikuwa nacheka sana na sehemu nyingine nimesikitika kwa mfano swala la watu kuzika kila siku ni la kweli na hata hapa kijijini kwetu naona limeshika hatamu.

Wapi Xspin na Sipo sijapata za vijijini kwenu.

yani mkuu acha tu na wengi ni vijana nakbwa zaidi ni akakaugonjwa mara ya mwisho kwenda kijijini vijana wanalalamika sana kuhusu kuzika da
 
picha jamani, acheni stori wekeni imeji tuone! kwetu bado choka tu, vijana niliocheza nao utotoni wameshazeeka vibaya, tena wamechakaa
 
Nguli,

Kwetu mzee bila kuwa mgumu huwezi kwenda kusalimia - ni km kama 800 hadi napoiacha barabara kubwa ya lami, then nakwenda km zingine 450 hadi kijijini kwetu, hii barabara ni mbovu saana - vumbi, mashimo na matope wakati wa masika usipime - average ni km 30 hadi 40 kwa saa ukiwa dereva mzuri.

Nipo jirani sana na waziri wangu mkuu, toka kijijini kwetu hadi kwao ni kama km 60 kwa upande wa pili - ambapo unaweza kupiga kwa baskeli tu na ukafika.

Kwetu bwana hali ni MBAYA SANA, vijana wamekata tamaa wanakunywa pombe za kienyeji - "ngogo" ambapo chupa ya orange inauzwa sh 500 na ndogo ya soda sh 250.
(Alcoholic ya chupa ya gongo moja ni sawa na bia 10 kwa wale wanywaji)

Primary Xul class mates wangu washakuwa wazee, si kwa umri ila shida walizonazo - wasichana wa wakati ule tuliosoma shule pamoja sasa ni wabibii - hawa ndiyo wanaochuja gongo kuwauzia wenzao, ili zoezi nzima la kugawana umaskini likamilike.

Kijijini kwetu umaskini ni wa wote, hakuna nyumba nzuri watoto ambao tulibahatika kupata elimu hii ya kambarage ya bure kawaida hatutaki kurudi kuwekeza sehemu isiyo na barabara wala chochote cha kutega uchumi, kwa hiyo tumengagania mjini kujaribu kujikimu ki mtindo mtindo.

Ila kwetu bia na soda hukosi, zinauzwa ingawa bei ni mara mbili ya ile ya mkoani, zinawekwa kenye chungu maalum kwa wale wanaopenda za baridi, kuku wa kienyeji eg jogoo kubwa ni sh 1200, nyie huku mnauziwa hadi sh 15,000. kwetu bwana kuku hata kila siku ukitaka.

Kwetu bwana basi lipo moja tu linaondoka saa 10 na nusu alfajiri – ukipenda usingizi wa asubuhi inakuwa imekula kwako linakuacha hadi kesho yake tena, nauli ni kubwa mno kiasi watu wanashindwa ku afford badala yake wanatumia baskeli na gari la ngombe - ni km 450 hadi mkoani – siku za mwisho wa mwezi linajaa sana maana walimu, manesi, bwanamganga, bwana mifugo wote ndani ya basi letu mjini kuchukua mshahara – kasheshe kupumuliana manake wengine wanakuwa wamelala nazo tena za kienyeji – mmhhh.

Mafisadi wa kule ( wenye nazo) ni waalimu, bwana mganga na wale wenye viosks, kweli hali ni ngumu mno - kwa mfano ukienda likizo ukamaliza pesa zako hadi nauli basi itakuwa imekula kwako maana hakuna benki kule mpaka usafiri hizo km nilizokwambia.

Kule kijijini kwetu bwana tuna shule ya sec ya kata moja ambapo kuna watoto wa ndugu yangu wanasoma pale, yupo mmoja form four nikamuuliza vitu basic tu hajui chochote hata test tube hajawahi kuiona.

Bwana kule kwetu ardhi ni bure kabisa ila haina rutuba - watu wanajaribu kulima tumbaku, mahindi, karanga, alizeti ila kwa heka moja ukipata gunia mbili ujue una bahati sana chief, hali ni mbaya sana, hakuna matumaini yoyote kwenye hiki kilimo.

Kijijini kwetu hakuna umeme, kwa hiyo nilivyokuwa huko nilikuwa naenda kwenye mnara wa celtel ili kucharge simu yangu ya nokia – bahati huduma hii ya simu imetufikia, nawapongeza sana hawa jamaa – mkiwaona wapeni big up.

Mkipata nafasi wakuu, njooni mtutembelee huku kijijini kwetu ili kama ikiwezekana tuugawane umaskini kwa pamoja.
 
Mara ya mwisho kwenda kijijini kwetu ilikuwa mwaka 2004 kwenye msiba wa bibi yangu. Nilikuta kuna umeme wa gridi ya taifa, network za Celtel na Vodacom. Kwa sasa nimeambiwa kwamba wana shule moja ya sekondari ya kata ambayo mwaka huu imetoa wanafunzi wa kidato cha nne kwa mara ya kwanza!

Pia Mbunge wetu Rostam amewezesha kijiji chetu kupata mitambo ya kusukuma maji toka mtoni kwenda kijiji. Kwa hiyo shida ya maji haipo tena. Pia naambiwa kwamba kilimo cha mpunga ndiyo chanzo kikubwa cha mapato na uchumi wa kijiji chetu. Kuna miundombinu ya mfumo wa umwagiliaji ambayo imechakaa na inahitaji ukarabati mkubwa. Lakini baadhi wa wanakijiji wamejimudu kununu pump za maji na majenereta ili kumwagilia mashamba yao. Kilimo cha pamba kimedorora sana!

Bia zipo kwa mama mmoja tu ambaye simkumbuki jina na wateja kwa kuwa ni wachache huwa tunanywea sebuleni kwake! Pombe za kienyeji kama kawaida!

Huduma za afya na shule za msingi pia zipo. Nyumba za wanakijiji nyingi ni za matofali ya udongo na zimeezekwa kwa bati. Baadhi yao wana nyumba za matofali ya kuchoma. Usafiri kuna basi moja tu la kwenda mjini, na barabara inapitika muda kipindi chote cha mwaka. Ni kilometa 23 tu toka kwenye barabara kuu ya lami. Siku za Jumapili hakuna usafiri wa kwenda mjini, na mara ya mwisho nilipokwenda nililazimika kukodi baskeli mbili, moja nikapanda mimi na nyingine ikabeba begi langu. Baiskeli hizo ni maarufu kwa jina la daladala!

Karibuni kijijini kwetu kwani watu ni wakarimu sana!
 
picha jamani, acheni stori wekeni imeji tuone! kwetu bado choka tu, vijana niliocheza nao utotoni wameshazeeka vibaya, tena wamechakaa


Kwa masikitiko makubwa nilisahau kamera, nilisahau kuongeza kuwa vijana wa kijijini kwetu walikuwa wanaoa wanawaacha wake zao kijijini wanaenda mjini kutafuta fedha wazee wakadumisha mila na wakwe zao na kuwapa ujauzito, vijana waliporudi ikawa fundisho hakuna anayemwachia baba yake mke tena.
 
Niko kijijini kwetu kwa vacation nilikuwa sijafika kwa miaka 2 nimefurahi kukuta maendeleo ambayo ni mazuri kwa mfano barabara ina kiwango cha lami hadi karibu na mpakani.
Mbunge wa uko kwenu anaitwa nani, hapa ni wazi kuwa umeshampigia kampeni ya kutosha dhidi ya wapinzani wake
 
Mbunge wa uko kwenu anaitwa nani, hapa ni wazi kuwa umeshampigia kampeni ya kutosha dhidi ya wapinzani wake


Wewe toa za kijijini kwako kwanza. Nini kinajiri huko???
 
Niko kijijini kwetu kwa vacation nilikuwa sijafika kwa miaka 2 nimefurahi kukuta maendeleo ambayo ni mazuri kwa mfano barabara ina kiwango cha lami hadi karibu na mpakani.

Ila kilichonishangaza ni hizi nyumba za kifahari kali kuliko hata baadhi ya nyumba za maeneo ya masaki na O'bay ambazo hazina wapangaji wala mtu anayeishi, unakuta nyingi zina babu na bibi ambao wanafanya usafi na kuitunza. Kwa mtazamo wangu tungejenga rum 2/3 kwa ajili ya siku kuu za xsmas na mwaka mpya na hizo hela zikafanya mambo mengine. najua huku kuna mashule na hospital basi tusaidie wengine/wa eneo tofauti. Baadhi ya hizi nyumba zingekuwa zinabebeka zingekuwa dispensary maeneo mengine au hata hospitali za rufaa.

Hapa kijijini kwetu raha kweli ukiwa padre unaheshimika kuliko hata waziri wala mmbunge. Ukisoma seminary ukaacha unaweza pewa radhi na bibi yako...huku padre anaitwa mopiaa....raha kweli.

Kuna makanisa yenye kengele ambazo ingekuwa dar ikipigwa ule mchana kwa mfano st. Peters wangesikia hadi bagamoyo. Ikipigwa hata kama mtu anakunywa/ria pombe ya mbege anaacha na kusali sala ya malaika/anjelusi hata kama amelewa ulevi unakata then unarudi upya baada ya sala.

Kijijini kwetu kweli raha bado mambo ya ndizi na matunda.



Kilichonishangaza zaidi ni kuwa makao makuu ya mkoa kuna gym 1 tena ina masharti magumu sana kuweza kufaidi huduma hio. Zilizokuwepo zote zimefungwa na sijapata sababu ya msingi ila nahisi ni demand kuwa ndogo.

Je kijijini kwako?

NGULI,

nimekupa. Maendeleo unayoyasifia kijijini kwenu ambayo ukiangalia kwa mamakini ni tofauti na katika maeneo mengine, hayo ni matokeo ya mfumo usio sawa (imbalance system) wa kugawa pato la taifa, kwa maana kwamba maeneo fulani fulani hasa maeneo unakotoka wamekuwa wakijipendelea sana kuliko maeneo mengine.Angalia unazungumzia bara bara za lami kijijini, nyumba za kifahari na umeme mapaka umewekwa kwenye miti, wakati mikoa kama Kigoma hakuna umeme wa grid, barabara ya lami ni moja iliyopo mjini tena mbovu sana imejaa mashimo, hakuna wenye uwezo wa kujenga nyumba zisizotumika vijijini. Hapa tunaona matokeo ya akina Basil Mramba, Waziri Mkuu wa zamani Msuya kupendelea mikoa wanayotoka na kusahau kabisa mikoa mingine kwa sasa ninyi mlioendelea mnaiita mikoa ya pembezoni.

Kulikokujisifia namna hiyo ebu piga kelele na mikoa mingine ipewe mgawo uliosawa na huo unaopelekwa kwenue ili wote kwa pamoja tusifie vijiji vyetu kama ulivyosifia vya kwenue. MUNGU IBARIKI MIKOA YA PEMBEZONI NAYO IKUMBUKWE KIMAENDELEO
 
nimekupa.

Mazee hapa umenipa nini?

Maendeleo unayoyasifia kijijini kwenu ambayo ukiangalia kwa mamakini ni tofauti na katika maeneo mengine, hayo ni matokeo ya mfumo usio sawa (imbalance system) wa kugawa pato la taifa, kwa maana kwamba maeneo fulani fulani hasa maeneo unakotoka wamekuwa wakijipendelea sana kuliko maeneo mengine.
Msuya kupendelea mikoa wanayotoka na kusahau kabisa mikoa mingine kwa sasa ninyi mlioendelea mnaiita mikoa ya pembezoni.

Tunajipendelea na nini? soma historia ya nchi vizuri...kwa hio hata wakoloni walitupendelea?? na kama ndio kwa nini?? Je mikoa yenu haina viongozi? kama wapo kazi yao ni nini? mbona wasipendelee kama wetu unavyodai wanatupendelea?

Kulikokujisifia namna hiyo ebu piga kelele na mikoa mingine ipewe mgawo uliosawa na huo unaopelekwa kwenue ili wote kwa pamoja tusifie vijiji vyetu kama ulivyosifia vya kwenue.

Kwa taarifa yako kuna maeneo huku kijijini kwetu yamewekwa lami na watu binafsi na hawakuisubiri serikali.


MUNGU IBARIKI MIKOA YA PEMBEZONI NAYO IKUMBUKWE KIMAENDELEO

Mungu ameshabariki siku nyingi hapa nahisi anakushangaa na hio statement watu wafanye kazi kwa bidii watunze mazingira ..kwa mafano kijijini kwetu ni kosa kukata miti ila unaruhusiwa kupanda miti, kumegeuka msitu, ikifika jumamosi kuna kitu kinaitwa msarakambo lazma wote mwaamke saa 12 am mkasafishe vyanzo vya maji au kuchimba barabara na usiposhiriki wanakuja kuchukua mbuzi 1 wanauza wanamlipa kibarua anafanya ile kazi yako. Je kwenu hilo lipo??
 
@nguli
mkuu umeniacha hoi alafu sikujua kama na ww ni mchaga yani kama ukienda machame uuwiiii yaniutashindwa kuelewa kama upo kijijini utafikiri upo obeyi tatizo kijijini kwetu vijana wamepungua sana na wapo busy sana kuchimba makaburi karibu kila siku watu wanapandishwa kuzikwa kwenye nyumba ya milele

Aisee! hiyo hali inatisha sana kijijini kwenu,nadhani hao wanaochimbiwa makaburi kila kukucha nikutoka Mjini ndio wanarudishwa hapo kijijini kwenye nyumba yao ya milele.

Mwaka jana nilipata msiba wa rafiki yangu na kwao ni Machame Nkuu tulikwenda uko kuzika sikuamini macho yangu nilichokiona huko yaani kumejengeka ile mbaya na kingine ni kwamba misiba ya huko watu wanakodi mziki kwa jili ya maombolezo na MC kabisa pamoja na wapambaji eneola msiba,vijana hawachimbi kabiri bila kupewa pesa yaani huko kuna tisha kwa jinsi maisha ya livyo.
 
Nguli

Kweli kijijini kwenu raha mpaka Internet mnapata ya kuweza kuandika maneno mengi hivyo. Kwetu tuna raha kuu moja tu, Chakula ni kingi sana kwani tunalima mahindi, karanga, maharagwe, viazi vitamu, pia kuna maembe na matunda mengi sana ambayo sisi hatuwezi kula na kumaliza hivyo vinatuozea tu kwa kukosa usafiri. Kwani hapa fikiki kirahisi kwa ubovu wa barabara.
 
Back
Top Bottom