Haya ndo masharti magumu ya MCC

Haya ndo masharti magumu ya MCC

Wakuu haya ndo masharti magumu ya MCC ambayo viongozi wengi wa CCM wanasema ni magumu.

Utawala bora.
Haki za binadamu na utawala unaofuata sheria mlizojipangia wenyewe.

Kweli haya masharti ni magumu mno[emoji1]
Magumu sana....
 
Binafsi sikubaliani na mawazo yako!!

MCC waliionya serikali December mwaka jana walipoahirisha msaada wa MCC. At the same time US, EU na nchi wahisani waliandika barua ya kupinga uchaguzi kufutwa na wakatoa ushauri. By that time Magufuli alikuwa ni Rais wa nchi. Kwa hiyo Magufuli kama Rais wakati huo alikuwa kabisa na uwezo wa kulishughulikia hili swala ........... kama sheria ni kweli hazimruhusu lakini busara ilitakiwa kutumika.

Tatizo waliunder estimate au hawakutegemea pigo kama hilo kuwatokea. Hii ni probably nchi kubwa kama China, UK na US zimekuwa zinaonyesha interest kubwa na Tanzania hasa kwenye kipindi cha Mkapa na Kikwete!! Tumeona akina Bush na Obama wanatembelea Bongo na kulala!!

Badala ya kupiga kelele na kujifanya maskini jeuri ni bora tuangalie namna ya kurekebisha mambo. Tatizo ni kwa kuwa hatukuwa tumejiandaa!!

Rais Magufuli aubebe tu huu mzigo wake maana wananchi tunamtegemea ......... asitafute mchawi nje. Mchawi ni CCM. Period!!
Na hiyo ndio demokrasia ya kukubali kutokubaliana tusiwe kama ccm tuliposhindwa tunalazimisha kushinda
 
Hilo swala linaweza liwepo lakini serikali ilikuwa inapokea misaada walikuwa hawaoni hicho kipengele?hili swala halihusu ndoa ya jinsia moja,imeibuka kutokana na uchaguzi wa Zanzibar kurudiwa

Ok, ok, it is possible, lakini masuala au masharti ya MCC siyo mawili tu yako zaidi ya 12, nadhani.

Halafu to make it clear kuhusu matumizi ya maneno naomba uwe unatumia 'suala' badala ya 'swala' au 'masuala' badala ya 'maswala'. Neno 'swala' lina maana nyingine kabisa. Maana yake inaweza kuwa aina ya mnyama na maana ya pili ni ibada. Naomba radhi kwa kuweka wazi maana ya neno 'swala'. Nimekukuwa nikiona wengi humu JF wanachanganya maneno haya mawili.
 
Thanks mkuu kwa masahihisho
 
Sharti kuu la MCC ni utawala bora. Utawala unaopiga vita rushwa na viongozi wake kupatikana kwa njia ya uchaguzi huru na wa haki. Hilo ndilo ambalo Tanzania haitaki, na inaona inaingiliwa uhuru wake.
Tanzania au ccm.Mimi najua kuna tofauti ya Tanzania na ccm
 
ccm ni chama cha hovyo sana ! na ni mkosi mkubwa sana kwa nchi hii kuwemo ndani yake ccm .
 
ni aibu sana kunyimwa misaada kwa sababu ya kukandamiza haki za raia .
 
Wakuu haya ndo masharti magumu ya MCC ambayo viongozi wengi wa CCM wanasema ni magumu.

Utawala bora.
Haki za binadamu na utawala unaofuata sheria mlizojipangia wenyewe.

Kweli haya masharti ni magumu mno[emoji1]

Umesahau hata matokeo ya uchaguzi tuliambiwa tukae nyumbani hii ndio CCM wakuu tumejitawala zaidi ya miaka 50 lakini hadi leo sheria kandamizi zinatungwa na kupitishwa na wabunge wetu njaa/ wala rushwa refer kelele za Lugola lazima wadhungu watufundishe adabu.
 
Kwani wewe ulikuwa una kikampuni kinafadhiriwa na MCC mbona unakomaa sana na hilo , au wewe ni jipu ulitaka kukwapua maana MCC imekuwa MCC.
Tumeishasema hatuitaki hiyo misaada yao.

Tatizo letu kubwa sisi Watanzania ni kuchukulia vitu 4 granted, lakini tungekuwa tunatafakari mchango mkubwa wa maendeleo kwa Taifa letu uliotokana na Serikali ya Marekani tangu utawala wa JK wala hakuna ambaye ange beza beza suala la MCC kutukomalia.

Mtu akisha panda basi au kuendesha gari lake toka pembe moja ya Taifa letu kwenda pembe nyingine hajui kwamba asili mia kubwa ya ujenzi wa barabara za lami umefadhiliwa na the USA, mitambo karibu yote ya uzalishaji umeme wa gesi inatoka Marekani save Wartsila za IPTL zinazo toka Finland,miundo mbinu za umeme mijini na vijijini wachangia wakubwa ni USA, maji, afya nk - hawa kweli ni watu wa kupondwa ponda na kudai eti wanataka kututawala - uzushi mtupu.

Kwanza Marekani yenyewe imewahi kuwa koloni la Uingereza sijawahi kusikia hata siku moja kwamba inatafuta makoloni ya kutawala, huo si utanaduni wao tusiwasingizie.

Mimi ambapo Wamerikani huwa sielewani nao ni adventure zao za kijeshi Duniani mambo mengine nawaona wana ubinadamu sana sina tatizo nao hata kidogo.

Sasa madai yako kwamba labda kikampuni changu kinafaidika na projects zao hiyo kwangu ni immaterial ingawa ni kweli ninewahi kufanya nao kazi za kiufundi kwenye Projects zilizo kuwa funded na kusimamiwa agency yao "USAID" jinsi wanavyo ji conduct wala hashangazi kwa nini Taifa hilo liko mbali karibu kwa kila kitu. Tuwasikilize wanatoa naoni/ushauri gani lakini sio kuwatukana na kuwasingizia mambo ya kubuni wakati sisi ndio wenye matatizo.
 
Umesahau hata matokeo ya uchaguzi tuliambiwa tukae nyumbani hii ndio CCM wakuu tumejitawala zaidi ya miaka 50 lakini hadi leo sheria kandamizi zinatungwa na kupitishwa na wabunge wetu njaa/ wala rushwa refer kelele za Lugola lazima wadhungu watufundishe adabu.
Madaraka ya rais ni makubwa mno,pia katiba haifuatwi ukifuatilia hata jinsi uchaguzi wa kwanza wa Zanzibar ulivyofutwa
 
Sharti kuu la MCC ni utawala bora. Utawala unaopiga vita rushwa na viongozi wake kupatikana kwa njia ya uchaguzi huru na wa haki. Hilo ndilo ambalo Tanzania haitaki, na inaona inaingiliwa uhuru wake.
Kama ingalikuwa ndo hvyo basi hata awamu ya kwanza tungekosaaa fedhaa hiyoo.
 
Wakuu haya ndo masharti magumu ya MCC ambayo viongozi wengi wa CCM wanasema ni magumu.

Utawala bora.
Haki za binadamu na utawala unaofuata sheria mlizojipangia wenyewe.

Kweli haya masharti ni magumu mno[emoji1]

Naamini hawa jamaa kuna mahali wamekwama ndio maana hata kabla ya kuamua kusitisha mwaka jana walitoa masharti ya kudhibiti rushwa kwanza ili watoe hizo pesa then baada ya kuona wamefanikiwa hilo ndipo wakatafuta point of weakness nyingine.

hivi kweli wana pesa hawa jamaa?
 
Wakuu haya ndo masharti magumu ya MCC ambayo viongozi wengi wa CCM wanasema ni magumu.

Utawala bora.
Haki za binadamu na utawala unaofuata sheria mlizojipangia wenyewe.

Kweli haya masharti ni magumu mno[emoji1]
Mbona suala la ushoga hujasema mkuu maana hiyo misaada lazima kwanza uruhusu ushoga.
 
Back
Top Bottom