Haya ndiyo mashairi ya kabwela wa staminnah

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Staminah ft Rich Mavoko - Kabwela


nimepigwa msumari wa kichwa mwili unangoja
kaburi
maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli
dunia tambala bovu nalidekia kwa shida
jitahidi kui'solve bila kutumia four figure
natamani nisimame ili nione magharibi
moyo umejaa ukame kuhema unajitahidi
macho yote yana ukungu utadhani chungu cha
bibi
nataka, kumuomba mungu shetani ananzidi
spidi men
vizuri viko wapi navisaka havionekani dah
napata makapi vinono navitamani
sina baba, sina mama, sina babu sina bibi
uchumi wangu umesimama kama behewa la
itigi
umaskini unanipodoa, bila kutumia cosmetics
daily unanizodoa, unanivuta bila magnetics
maisha yangu hayana swagga kama mmasai wa
Njiro
Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo
dah
leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu boo
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
sikusoma, kitajiri kichwa kimejaa madufu
maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua lufufu
naichora, lami na mkaa kwa kudhani nitaona
chochote
atleast, basi ningekaa nisingeitwa kiokote
pesa imegeuka yuda, daily inanisaliti
mishale inazidi muda, utajiri unaninyima seat
maisha kama gwaride, kuna wa mwisho na wa
kwanza
ikisikika nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa
kwanza
taifa la kichwa changu Raisi wake naona kichaa
na kitabu, cha dhambi zangu kwa Mungu
kimeshajaa
ah, napatwa wazimu shida zinanitia madoa
pesa imekuwa adimu kama bikra kwa
changudoa
banda nnalofugiwa sihemi halina dirisha
wasichana wananikimbia wananiita nyoka wa
kibisa
msosi wangu sio wa drafti sili mpaka nijitume
maisha yana super shaft yashanizidi nguvu za
kiume
dah
leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu boo
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
ushindi wangu ni wa uchafu kwenye vita ya
wasafi
kila nnayemuomba tafu anataka afanye na ulafi
maisha ni kombolela masikini ndio mlinda kopo
cha msingi ni kuunga tela mpaka utoke kwenye
msoto
kila jua linapozama natamani pasikuche
hasi inageuka chanya kapeto anageuka sunche
naona alama za mlango ila sioni pa kutokea
hii pesa imetoka jando inataka kuni-babu seya
nimegeuka konokono natembea na mzigo wa
shida
silali, nimekuwa figganigga maisha unakwenda na
mida
shida zishanipa ustaa, zaidi ya kanda ya loketo
tumbo umezoea njaa hadi shibe naiona mseto
vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani
na vijiko vya uhalifu nishaviweka kwenye sahani
mi nadhani, haya maisha yana ramani
na aliyewachorea masikini peni ilimgomea njiani
ah
leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu boo
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela. Mia
 
figganigga nipo out of post,but hivi unajua majina ya hawa majamaa walioimba bab kubwa?walikuwa kundi au walishirikiana tu kwenye huo wimbo wa bab kubwa?.
Chorus,
Hii ni bab kubwa hii ni bab kubwa sema bab kubwa,
au sio mazee sema kubwa...

,.......

aliyeanza kuchana anajua ile mbaya,dogo aliyemalizia kuchana ndo kafunika...sasa sielewi hawa majamaa walikuwaga kundi au walikutana tu?na wapo na wameacha mziki?
 
Last edited by a moderator:
figganigga nipo out of post,but hivi unajua majina ya hawa majamaa walioimba bab kubwa?walikuwa kundi au walishirikiana tu kwenye huo wimbo wa bab kubwa?.
Chorus,
Hii ni bab kubwa hii ni bab kubwa sema bab kubwa,
au sio mazee sema kubwa...

,.......

aliyeanza kuchana anajua ile mbaya,dogo aliyemalizia kuchana ndo kafunika...sasa sielewi hawa majamaa walikuwaga kundi au walikutana tu?na wapo na wameacha mziki?

Mkuu nimeshindwa kukujibu ile ishu, PM kwako zimefungwa...
 
ana mashairi ya kuungaunga tu ...

.bongo jua la utosi *HADI * juma
anakosa nature. .nina mistar mikali
*HADI rwanda ananionea
gele. .muziki nimeanza kale *HADI
leo sijaitwa pepe. .lyf ngumu *HADI
ombaomba kdonda anafanya
mtaji. ..Kipofu mwenye machale
anaijua *HADI* chuma
ulete. ...Nimesomea udereva
naendesha *HADI* mapenzi .Marafk
masnch wanasnch *HADI* kwa mke wangu.

hiphop gani hii RUBBISH.
 
ana mashairi ya kuungaunga tu ...

.bongo jua la utosi *HADI * juma
anakosa nature. .nina mistar mikali
*HADI rwanda ananionea
gele. .muziki nimeanza kale *HADI
leo sijaitwa pepe. .lyf ngumu *HADI
ombaomba kdonda anafanya
mtaji. ..Kipofu mwenye machale
anaijua *HADI* chuma
ulete. ...Nimesomea udereva
naendesha *HADI* mapenzi .Marafk
masnch wanasnch *HADI* kwa mke wangu.

hiphop gani hii RUBBISH.
Haiwezi kuitwa HIPHOP.
haya ni mashairi tu ya Kikomedi komedi.
Hakuna maana inayokidhi haja.
 
ana mashairi ya kuungaunga tu ...

.bongo jua la utosi *HADI * juma
anakosa nature. .nina mistar mikali
*HADI rwanda ananionea
gele. .muziki nimeanza kale *HADI
leo sijaitwa pepe. .lyf ngumu *HADI
ombaomba kdonda anafanya
mtaji. ..Kipofu mwenye machale
anaijua *HADI* chuma
ulete. ...Nimesomea udereva
naendesha *HADI* mapenzi .Marafk
masnch wanasnch *HADI* kwa mke wangu.

hiphop gani hii RUBBISH.

HADI zipo 7 hapo km nimehesabu vizuri
 
Back
Top Bottom