Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Nov 27, 2013.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 23,297
  Likes Received: 32,024
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]

  Hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo, ambao wiki iliyopita walivuliwa nafasi za uongozi, zinazoeleza mashtaka ya makosa 11 wanayotuhumiwa kuyatenda dhidi ya chama hicho.

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema barua hizo, ambazo Zitto na Dk. Mkumbo, walitarajiwa kukabidhiwa jana, zinawataka wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua zaidi, ikiwamo kufukuzwa uanachama.

  Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, siku mbili baada ya Zitto na Dk. Mkumbo, kuitisha mkutano na waandishi wa habari, Jumapili wiki iliyopita na kusema hadi siku hiyo walikuwa hawajapata barua hizo zaidi ya kusikia suala hilo kwenye vyombo vya habari.

  Mnyika alisema mashtaka ya makosa, ambayo Zitto na Dk. Mkumbo wanatuhumiwa kuyatenda, yanahusiana moja kwa moja na ukiukwaji wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama hicho.
  Alisema uamuzi wa kuwavua nafasi za uongozi ulifikiwa na Kamati Kuu (CC) ya Chadema katika vikao vyake vilivyofanyika wiki iliyopita.
  Mnyika alisema baada ya maamuzi hayo ya CC, juzi sekretarieti yake ilikutana kwa mujibu wa kazi zake za kikatiba.

  Alisema ikiwa sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya CC, sekretarieti ilikamilisha mapitio ya yaliyojiri pamoja na maamuzi ya CC juu ya suala hilo pamoja na kukamilisha barua hizo kwa wahusika.

  “Na naomba kuwajulisha tu kwamba, leo (jana) wahusika wote (Zitto na Dk. Kitila) watapatiwa barua zao kwa maana kwamba barua zao ziko tayari zinazoeleza maamuzi ya Kamati Kuu,” alisema Mnyika.

  Alisema maamuzi ya CC hayakuhusu tu kuwavua uongozi, bali yalihusu vilevile kutakiwa kuandikiwa kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua za ziada, ikiwamo kufukuzwa uanachama kutokana na makosa waliyoyafanya na waliyokifanyia chama.

  “Na kwa kweli ni makosa waliyoyafanya na ambayo wamekifanyia chama yalielezwa na maamuzi ya Kamati Kuu yaliyotangazwa,” alisema Mnyika.

  MAKOSA YANAHUSIANA NA WARAKA
  Alisema makosa hayo yalihusiana na waraka ulioandikwa, ambao kimsingi ulikiuka katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.

  “Sasa kwenye mashtaka yao na barua zao ambazo leo watakabidhiwa kumeeleza mashtaka na makosa 11, ambayo watajwa wameyafanya ya kukiuka kanuni, katiba na itifaki ya chama,” alisema Mnyika.

  Alisema mashtaka waliyoandikiwa, yamejikita katika maamuzi ya CC, ambayo yalihusu waraka wa siri.

  “Na siyo masuala, ambayo wahusika baada ya Kamati Kuu kupitisha maamuzi yale wameyasema kwenye vyombo vya habari masuala ambayo siyo yaliyoifanya Kamati Kuu ifikie maamuzi iliyoyafikia,” alisema Mnyika.

  Aliongeza: “Kwa hiyo tayari wahusika wameandikiwa barua na nisisitize kwamba, maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu ya chama yamefanywa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.”

  Maamuzi hayo ya CC yalimvua Zitto, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini wadhifa za Naibu Katibu Mkuu na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida.

  Kwa maana hiyo, Zitto ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, amebaki kuwa mwanachama wa kawaida.

  Aidha, uongozi wa wabunge wa Chadema uliagizwa na CC kumwandikia barua Zitto ya kumwondoa katika nafasi ya Naibu Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Fedha haraka iwezekanavyo kwa tuhuma za kukisaliti chama.

  Pia aliyekuwa Mjumbe wa CC, Dk. Kitila, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, ambao nao wamevuliwa nyadhifa zote za uongozi na kubaki kuwa wanachama wa kawaida.

  Akijibu yaliyozungumzwa na Zitto na Dk. Kitila baada ya maamuzi ya CC dhidi yao, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema ni maneno ya kupoteza lengo kwa kuwa walivuliwa nafasi za uongozi kwa sababu ya waraka ule na siyo kwa sababu ya kile alichokiita uongo wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

  ‘Uongo’ wa PAC unaodaiwa na Lissu, ni kauli iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto akisema hakuna chama chochote cha siasa, ikiwamo Chadema, ambacho hesabu zake zimekaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Lissu alisema hata Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatambua kuwa Chadema ni kati ya vyama, ambavyo hesabu zake zimekaguliwa.

  Alisema Chadema ina nyaraka zinazothibitisha hilo tangu mwaka 2010, 2011 na 2012, ambazo Zitto alipokuwa Naibu Katibu Mkuu alipaswa kuzijua.

  Lakini alisema Zitto alishindwa kuzijua nyaraka hizo kwa sababu alipokuwa kiongozi wa chama hakuwa na mazoea ya kufika ofisini, badala yake amekuwa akiishia kukitungia uongo chama.

  “(Zitto) Anatumia jukwaa la PAC kutukanyaga kwa hoja za uongo,” alisema Lissu.

  Mbali na hilo, Lissu alisema pia kuwa Zitto na Dk. Mkumbo hawakuvuliwa nafasi za uongozi katika chama kwa sababu ya yeye (Zitto) kukataa kupokea posho au kuuza majimbo ya uchaguzi, ambayo Chadema ilisimamisha wagombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Kuhusu hoja kwamba CC haina mamlaka ya kumvua mwanachama nafasi ya uongozi bali Baraza Kuu la chama, alisema haina msingi kwa kuwa katiba ya Chadema imeipa mamlaka CC kama itaona kuna dharura ya kufanya hivyo.

  Alitoa mfano akisema mwaka 2004 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Amani Kabourou alivuliwa nafasi hiyo na CC. Pia mwaka 2007, CC ilimvua Umakamu Mwenyekiti Taifa, marehemu Chacha Wangwe.

  Alisema vipindi vyote hivyo, Zitto alikuwapo na alishuhudia hayo.

  “Sasa kama CC ilikuwa sahihi vipindi vyote hivyo basi na sasa ni sahihi,” alisema Lissu.

  Alisema mashtaka ya makosa 11, ambayo Zitto na Dk. Kitila wanatuhumiwa kuyatenda hawawezi kuyaweka hadharani, bali watawakabidhi wahusika na kwamba, kama wao wataamua kufanya hivyo hilo litakuwa juu yao.

  Hata hivyo, alisema wanaweza kuyaweka hadharani baada ya CC kupokea utetezi kutoka kwa watuhumiwa.

  Alisema mwaka 2012, Chadema ilitengeneza mwongozo unaomtaka mwanachama kutangaza kusudio la namna ya kugombea uongozi katika chama na kwamba, walifanya hivyo ili kuzima chokochoko zilizokuwa zimekithiri kuelekea kwenye uchaguzi katika siku za nyuma.

  Kwa mujibu wa Lissu, mwongozo huo unataka mwanachama atangaze wazi kusudio lake hilo kwa kupeleka barua kwa Katibu Mkuu na siyo kwa kujificha na kuchafua wengine.

  “Kama wangekuwa wanataka mtu wao (awe mwenyekiti wa Chadema) wangetangaza. Maamuzi ya Kamati Kuu ni uthibitisho kwamba hakuna tunayemuogopa,” alisema Lissu.

  Alisema ni kweli suala la PAC lilijadiliwa katika vikao vya CC, lakini halikuwa hoja ya kuwashtaki wahusika.

  FEDHA ZA SABODO

  Kuhusu Sh. milioni 100 zilizowahi kutolewa na mfanyabiashara Mustafa Sabodo kwa Chadema mwaka 2009, Lissu alisema zipo kwenye ripoti ya CAG na ile iliyopelekwa na chama kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kwamba, hajawahi kumsikia Zitto akihoji fedha hizo na zile za ruzuku ya chama kwenye vikao vya chama.

  CHANZO: NIPASHE

  =============
   

  Attached Files:

 2. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2013
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,615
  Trophy Points: 280
  Kwani fedha ni za Sabodo tu
   
 3. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2013
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,615
  Trophy Points: 280
  Nimegundua watu wanachuki binafsi na Zito,hawataki ukweliii:vijana Wachadema si walisema Shibuda aliwaambia kipindi kile kesi ya Ugaidi,Waseme wametumwa na Mbowe na Slaa,ukitaka kujua ni unafiki wa kina Kileo na wenzao ndo huu,kwa akili ya kawaida kama yale maneno yana ukweli nani anakigawa CHAMA?????????
  Tuache UNAFIKI
  Samahani lakini,nirudi katika waraka nimeusoma huu waraka mara nyingi,sioni tatizo,zaidi ya kuwa na mambo mazuri kwa Chadema yenye afya kama yatafanyiwa kazi,bila hata Zito kuwa kiongozi,mimi kutoka Moyoni nataka Slaa na Mbowe waondoke katika Uongozi,pia Zito asiwe kiongozi wote wabaki kuwa washauri na wajumbe
  Nakubali Zitto Kabwe ana Udhaifu wake lakini Mbowe na Slaa sio Malaika!
  Swali kwa Wadau maana huu waraka tumejadili kihisi kumuhusu Zitto wakati yeye ajauandaa,Je ikitokea ukakamatwa waraka unamuhusisha Mbowe kutaka kusiwe na Ukomo katika nafasi ya Uenyekiti je mbowe achukuliwe Hatua gani????
   
 4. COARTEM

  COARTEM JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2013
  Joined: Nov 26, 2013
  Messages: 2,697
  Likes Received: 913
  Trophy Points: 280
  RED: Huo ndiyo utakuwa muafaka wa msingi ili kuunganisha wanachama wote.
  GREEN:100% nakubaliana na wewe.
  BLUE: Watasema umetengenezwa na CCM,TISS wakishirikiana na ZZK.
   
 5. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 23,297
  Likes Received: 32,024
  Trophy Points: 280
  Nimegundua ni vigumu kwa Zitto na Kitilla kusalimika baada ya kusoma kauli hii iliyotolewa na Lissu kwa waandishi jana.

  Habarileo limemnukuu Lissu kama ifuatavyo:

  "Waraka huu umetoa matusi mazito dhidi ya Mwenyekiti wetu,ikiwamo kuitwa kuwa ana elimu ya chini na ana akili ndogo na nzito,halafu mtu huyo huyo alietoa matusi hayo dhidi ya kiongozi wake wa chama anadai eti anakiheshimu chama,kwa hili tumewashitukia,"alisema.

  Ndugu mwana JF kama kweli hii ndio kauli kwenye waraka huo kuna kusalimika hapa?

  Ni vigumu kwa Zitto na Kitila kusalimika kuliko ilivyo vigumu kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
   
 6. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #6
  Nov 27, 2013
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,972
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Kwanza wanawachelewesha sana, Tusha Choka nao,
   
 7. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 218
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  Watu wanapigana na ukweli, hivi mwenye elimu ndogo tumuiteje?

   
 8. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,900
  Likes Received: 1,545
  Trophy Points: 280
  Mbona hayo mashitaka hawajaweka wanahofu nini waweke wazi tujue ili tupime.
   
 9. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama mahesabu ya CDM hayajakaguliwa sio suala la CDM, ni suala la CAG na msajili wa vyama; sasa CDM iingekuwa inawafuata waje kufanyakazi yao??? je ndo kazi zinafanyika hivyo??? hilo suala kamwe haliwezi kuwa la CDM ni watu wajinga tu kama wasaliti wanaweza kufikiria hilo ni la chama wakati ni la wenye majukumu hayo.
   
 10. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 23,297
  Likes Received: 32,024
  Trophy Points: 280
  Hivi mzazi wako au mtu yoyote utamdharau kwasababu tu ya elimu yake ndogo??!!

  Raisi Mwinyi alikuwa na elimu gani alipokuwa Raisi wa nchi hii?

  Acheni unafiki na kuendekeza siasa kwenye kila jambo!
   
 11. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,561
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Kweli mkuu, kwanza Tundu Lisu kasema hao wamefukuzwa na sio kuwa wameachishwa vyeo vyao tu na kubaki wanachama. Tundu Lisu atakuwa na jambo moyoni mwake limejificha.
   
 12. t

  thobias20 Member

  #12
  Nov 27, 2013
  Joined: Oct 18, 2013
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naipenda sn chadema kwa kuwa na maamuzi magumu,chama kinatakiwa kiendeshwe hivyo
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 24,363
  Likes Received: 1,751
  Trophy Points: 280
  huwezi ona tatizo km tatizo hilo limeletwa kwa akili hiyo hiyo..yaani kukosa uwezo kwa akili hiyo,ndiko kuliposababisha tatizo na hivyo tatizo kuwa ni ishara ya akili kusindwa na kuwa mzigo.
   
 14. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,574
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  na za mama yako pia......
   
 15. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,574
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  uyapime wewe nani.....silly
   
 16. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,574
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kweli mkuu wangu......
   
 17. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2013
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  hahahaahaha...kwa speech ya lisu tayari zitto anahujumiwa...eti hatutaki kuweka tuhuma wazi ila si alizozisema zitto na dk.mkumbo...eti ukiwa na nia ya kugombea unaandka barua kwa katibu mkuu hivi kweli kuna kitu kama hicho dunia ipi..et ohh zito ajawahi kuhoji pesa za sabodo na ruzuku kwenye vikao vya chama..sasa atahoji ili nani atekeleze? Mbowe au mkwe wake au vibaraka wa mbowe? Na watueleze ni kwa nini zitto alijitoa kuwa signatory kama si ufisadi wa mbowe na kufanya chama mali yake ikiwemo kukiuzia chama magari chakavu..kukikopesha chama ruzuku kama pesa yake..etc chadema ni saccos ya mbowe na mtei full stop vbaraka wengne wa mbowe njaa zinawasumbua mwsho umefka go zito go zito toa uozo chadema si mama yako wala baba yako..mvuto wa zitto kisiasa na uwezo wake wa kujenga hoja ndio umeifksha chadema pale ilipo toka enzi za buzwagi saga adi leo...chadema masalia wanaoshinda ufipa ni waganga njaa ndio maana mbowe anawawin kirahisi...mbowe si mwanasiasa ni bussines man na silaha anatafta pensheni kwa hili mnyka na umeonyesha udhaifu sana kwa sababu silaha tunajua alishakuwa mtumwa wa mbowe na mtei wewe nawe umeingia uko mnyka kuwa saccos member?
   
 18. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,900
  Likes Received: 1,545
  Trophy Points: 280
  Ndiyo tatizo la watanzania mtu anaelimu ndogo anataka kuitwa anaelimu kubwa mambo gani haya.
   
 19. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,900
  Likes Received: 1,545
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuitwa kuku halafu uwe na mtazamo chanya hata kidogo ndiyo maana unatukana hovyo tu.
   
 20. c

  casampeda JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2013
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Makao Makuu ya CDM wanagombana,maafisa wao kuutoa waraka ktk mitandao ya jamii,MNYIKA anajuta kwanini alienda safari ya nnje,hawakujua kama watakuwa UCHI.
   
Loading...