Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,495
- 5,531
Mshahara ni malipo/ujira anaopokea mtu baada ya kutekeleza majukumu yako katika kipindi fulani kwa mujibu wa makubaliano.
Mshahara unaweza kuwa mkubwa au mdogo kwa kulinganisha kiwango cha uzalishaji,gharama za maisha na mtazamo binafsi.
Kuna mtu au mazingira ambapo mshahara wa TZS ni 170,000 ni mdogo na kuna mazingira ambamo au mtu ambaye mshahara huo kwake ni mkubwa.
Kwa hakika hata mshahara wa milioni 10 una sifa hizo hizo.
Pamoja na tofauti za kimtazamo, ni ukweli usiopingika kwamba matumizi ya mshara ni yale yale.
Ili kutumia mshahara wako kikamilifu unapaswa utumie mfumo rahisi sana wa 2-3-3 ambapo mshahara wako unaugawa mara 2 kisha hizo nusu zinazopatikana unazigawa katika maeneo matatu.
Mshahara wako unaugawa katika Matumzi ya kawaida na Matumizi Maalum
Katika kundi la Matumizi ya Kawaida-Utakuwa Matumizi ya Lazima,Matumizi yasiokuwa na Lazima Dharura
Katika Matumizi maalum utakuwa na -Matumizi ya Maendeleo,Madeni na Akiba
MATUMIZI YA MAENDELEO ni kama vile kununua vitu vya maendeleo kama ardhi,furniture,etc
MATUMIZI YA LAZIMA ni kama vile Chakula,mavazi na malazi
MATUMIZI YASIYOKUWA YA LAZIMA ni kama vile burudani, hongo, mitoko na anasa zisizokuwa lazima
MATUMIZI YA DHARURA NI KAMA VILE MASUALA YA TIBA ajali etc
Tazama Jedwali hapa Chini. Kila inapofika mwisho wa Mwizo Fedha ambazo hazijatumika katika kundi lolote ziingizwe katika kundi la Fedha ZA AKIBA ili AKIBA YAKO IKUE.
Ni muhimu sana kupeleka Pesa katika eneo ambalo halijatumika katika Akiba ili akiba iendelee kukua.
Kiwango unachoweza bajeti katika kila eneo inategemea na mtindo wako wa maisha, gharama za maisha, vipaumbele vyako n.k.ila hakikisha kabisa hutumii pesa zaidi katika eneo fulani isipokuwa katika suala la kufa na kupona.
Nakutakia kila la heri.

Matumizi ya KAWAIDA | Matumizi Maalum |
Matumizi ya LAzima | Matumizi ya Maendeleo |
Matumizi yasiyokuwa ya Lazima | Matumizi ya Madeni |
Matumizi ya Dharura | Matumizi ya Akiba |