Haya ndio matumizi sahihi ya mshahara wako

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,435
5,404
Mshahara ni malipo/ujira anaopokea mtu baada ya kutekeleza majukumu yako katika kipindi fulani kwa mujibu wa makubaliano.

Mshahara unaweza kuwa mkubwa au mdogo kwa kulinganisha kiwango cha uzalishaji,gharama za maisha na mtazamo binafsi.

Kuna mtu au mazingira ambapo mshahara wa TZS ni 170,000 ni mdogo na kuna mazingira ambamo au mtu ambaye mshahara huo kwake ni mkubwa.

Kwa hakika hata mshahara wa milioni 10 una sifa hizo hizo.

Pamoja na tofauti za kimtazamo, ni ukweli usiopingika kwamba matumizi ya mshara ni yale yale.

Ili kutumia mshahara wako kikamilifu unapaswa utumie mfumo rahisi sana wa 2-3-3 ambapo mshahara wako unaugawa mara 2 kisha hizo nusu zinazopatikana unazigawa katika maeneo matatu.

Mshahara wako unaugawa katika Matumzi ya kawaida na Matumizi Maalum

Katika kundi la Matumizi ya Kawaida-Utakuwa Matumizi ya Lazima,Matumizi yasiokuwa na Lazima Dharura

Katika Matumizi maalum utakuwa na -Matumizi ya Maendeleo,Madeni na Akiba

MATUMIZI YA MAENDELEO ni kama vile kununua vitu vya maendeleo kama ardhi,furniture,etc

MATUMIZI YA LAZIMA ni kama vile Chakula,mavazi na malazi

MATUMIZI YASIYOKUWA YA LAZIMA ni kama vile burudani, hongo, mitoko na anasa zisizokuwa lazima

MATUMIZI YA DHARURA NI KAMA VILE MASUALA YA TIBA ajali etc

Tazama Jedwali hapa Chini. Kila inapofika mwisho wa Mwizo Fedha ambazo hazijatumika katika kundi lolote ziingizwe katika kundi la Fedha ZA AKIBA ili AKIBA YAKO IKUE.

Matumizi ya KAWAIDAMatumizi Maalum
Matumizi ya LAzimaMatumizi ya Maendeleo
Matumizi yasiyokuwa ya LazimaMatumizi ya Madeni
Matumizi ya DharuraMatumizi ya Akiba

Ni muhimu sana kupeleka Pesa katika eneo ambalo halijatumika katika Akiba ili akiba iendelee kukua.

Kiwango unachoweza bajeti katika kila eneo inategemea na mtindo wako wa maisha, gharama za maisha, vipaumbele vyako n.k.ila hakikisha kabisa hutumii pesa zaidi katika eneo fulani isipokuwa katika suala la kufa na kupona.

Nakutakia kila la heri.
 
Kwa mshahara gan...tunakopa..tunajenga na kununua asset kama, magari viwanja ect iliyobaki tunalewa na kula na haifiki mwiaho wa mwezi..maisha yanasonga ah ah
 
Kwa mshahara gan...tunakopa..tunajenga na kununua asset kama, magari viwanja ect iliyobaki tunalewa na kula na haifiki mwiaho wa mwezi..maisha yanasonga ah ah
Mkuu huo huo mshahara unaweza kuutumia na ukapo,ukajenga,ukanunua asset nainayobaki ukale na marafiki ili ukitaka kuila kwa raha bila kujikuta unaishi kama mtumwa fanya hicho nilichokwambia.hata kama baadhi ya maeneo utayaweke elfu kumi tu we anza kufanya hvo then nidhamu hio ikishakukaa utakuja kuleta mrejesho.

Ukiweka akiba yako ukaona inakua utapata hamasa,ukiweza kuwa na nidhamu ya matumizi na kutumia kila tu ulichopanga kutumia utapata raha ya ajabu katika nafsi yako na utajikuta mwnye amani.

Sijaweka kiwango kwa sababu mishahara inatofautiana na mtindo wa maisha pia ni tofauti ila matumizi ya mishahara na yale yale.
 
sasa lets say basic 1 million ok laki 5 matumizi lazima na kuhonga...laki tano iliyobaki ndo uweke akiba leta say 200, 000 uwekeze laki 2 bado hujalipa madeni ah ah kijana hii kitu imekaa kinadharia...we piga mkopo bakiza 1/3 unaishi kwa chakula na ulevia kwe akiba unawekewa na nssf sawa....iliyobaki kula na kulewa baada ya kuwekeza ule mkopo kwe asset kama nyumba au kiwanja
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom