Mwenye nidhamu kubwa ya kuweka akiba ya pesa huishi na mambo mawili

wamilazo1

New Member
Oct 31, 2021
3
7
Mtu mwenye nidhamu ya kuweka akiba ya pesa, mambo mawili humuongoza katika safari yake ya mafanikio
1. Matumizi ya lazima
2. Matumizi ya muhimu

Matumizi ya lazima
Ni aina ya matumizi ambayo mtu mwenye nidhamu ya pesa au mtu yeyote akikosa hupata madhara na kuhatalisha maisha yake. Mifano ya matumizi ya lazima ni Chakula, malazi, mavazi (basic needs). Mtu mwenye nidhamu ya pesa huzingatia sana matumizi haya kuliko mengine nje ya hapo.

Matumizi ya muhimu
Matumizi ya muhimu ni aina ya matumizi ambayo akikosa au binadamu yeyote akikosa hapati madhara. Mfano Habari (tv & radio) n.k
Mwenye nidhamu ya kujisamia. Na kutimiza malengo yake kwa kuweka akiba. Matumizi ya muhimu kwake sio kipaumbele cha maisha yake.

Hivyo hafanyi matumizi ya muhimu mpaka aweke akiba. Na hujaribu kupunguza matumizi ya lazima ili kukizi malengo yake.

Je wewe upo kundi gani
1. Unaweka akiba kabla ya matumizi ya lazima & muhimu?

2. Unaweka akiba baada ya matumizi ya lazima na Kabla ya matumizi ya muhimu?

3. Unaweka akiba baada ya matumizi ya lazima na muhimu?

4. Hauweki akiba kabisa.

Jichunguze sasa!
 
Nakumbuka mara ya mwisho kuweka akiba ikawa akiba kweli ni mwanzoni wa 2010.
Tokea hapo msamiati wa kuweka akiba kwangu umekua mgumu sana!
Lakini Mungu alivyo mwema tunapokutana na dharura jua halikuchwi tukiwa bado hatujaitatua.
 
Mfalme Suleimani aliwahi kusema hivi "kuna mtu anafuja na kutapanya pesa lakini anazidi kuwa tajiri" na "Kuna mtu anabana pesa na kuweka akiba lakini anazidi kuwa masikini"....
Ukute umejitungia hilo verse na kama lipo basi utasema umesahau linapatikana wapi ila litafute na tuwekee hapa tujue hukutunga toka kichwani mwako!.
 
Ukute umejitungia hilo verse na kama lipo basi utasema umesahau linapatikana wapi ila litafute na tuwekee hapa tujue hukutunga toka kichwani mwako!.
" Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji "
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ Mithali 11:24~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
 
Back
Top Bottom