round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 935
- 3,014
MAHUSIANO - Kuna watu wanapigania sana mahusiano yao yasivunjike, kuna waliochoka na mahusiano wanatafuta mlango wa kutokea lakini hawauoni mlango wa kutoka, wengine wana kiu ya mahusiano wanautafuta mlango wa kuingilia lakini hawauoni, watu wanasalitiwa na kuachiwa vidonda vya milele, mtu unampa kila kitu anachohitaji lakini wapi.
MADENI - Oyaaa sio poa ! Kuna watu wanateseka sana kwasababu ya kushindwa kulipa madeni, Mtu anachelewa kurudi kwake usiku ili kukwepa wanaomdai, mtu hana uhuru na simu yake anaizima kukwepa wanaomdai, Mtu anakosa amani ya kupita barabarani anakatiza vichochoroni, n.k. Wengine wanateseka kwasababu wanadai hela zao, kila ukienda kwa mtu unaemdai anaruka ukuta, mtu unaemdai ameku block simu isipatikane, mtu unaemdai anakwambia wewe fanya lolote ila hana pesa halafu mbaya zaidi awe ndugu yako, duh !!
MAAMUZI ULIYOWAHI KUYAFANYA ZAMANI - Maji yakishamwagika hayazoleki, maamuzi yana uzito mkubwa katika maisha, unatamani kurudi nyuma urekebishe baadhi ya vitu ulivyovifanya lakini muda umekata, Wapo waliotumbukia kwenye matatizo ya kiafya kutokana na maamuzi mabovu kwenye starehe na anasa za ujana, Wapo walioporomoka kiuchumi kwa sababu ya tamaa ya kupata utajiri wa ghafla au kushindwa kupanga maisha yao vizuri, Wengine wapo nyuma ya nondo gerezani wakihesabu miaka kwa majuto ya maamuzi.
KIPATO KISICHOKIDHI MAHITAJI - Watu wengi huamka asubuhi wengine hawalali usiku kwajili ya kutafuta kipato, wengine kwa njia halali wengine kwa njia zisizofaa lakini wimbo umebaki kuwa ule ule kwa miaka mingi, HELA HAITOSHI !! Umegeuka Jet Lee wa kuruka madimbwi kipindi cha mvua kwasababu huwezi kununua usafiri, Mchana unapiga dash bila kula ili ubane nauli kwasababu bajeti ni ndogo, Mwanafunzi mwenye akili hawezi kusoma chuo kwasababu kakosa mkopo na kwao hakuna pesa, n.k. Pesa sio kila kitu lakini hutatua matatizo mengi.
KESHO ITAKUWAJE - matatizo yanapokuwa makubwa akili inachowaza unapoenda kulala ni "Kesho itakuwaje", hali hii hupelekea msongo wa mawazo na magonjwa ya moyo, presha, kisukari, n.k. Mahusiano yako hayaeleweki unahisi unasalitiwa na hujui kama yatadumu, Madeni yamekuwa mzigo yamekuwa kivuli kinachokufuata kila kona, Kipato hakitoshi kila shilingi ina kazi nyingi, Maamuzi ya zamani bado yanakufuata kama mzimu yakikukumbusha kila mara kwamba baadhi ya njia hazikustahili kupitiwa. unatafuta njia ya haraka ya kutoroka ukweli, wengine wanajitumbukiza kwenye ulevi, mahusiano mapya, Kukopa zaidi, kucheza kamari, kujiingiza kwnye uhalifu, kwenda kwa waganga, n.k. wakidhani watapunguza matatizo kumbe wanayaongeza zaidi.