Haya mambo ya kuvutiwa sauti ya mtu kwenye simu

Haya mambo ya kuvutiwa sauti ya mtu kwenye simu

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,753
Reaction score
4,866
Unavyojua kinachotuvutia kwanza huwa ni sura au figure. Yanayofuata hapo kila mtu ana yake. Kwangu kifuatacho ni ubora kichwani. Hata tukijibizana hapa JF huwa tayari nimeshafahamu huyu ni kiwango gani.

Sasa ni enzi za elektonik. Unapigiwa simu na unapopokea unagundua ni simu iliyopotea njia. Lakini umeshapata namba ya simu na sauti umeisikia. Unaweza kuvutiwa. Nilishavutiwa na sauti na upweke ukanituma kuirejea incoming call list ya simu yangu ya kisasa kabisa! Nokia fulani ya kama laki 8. Nikaomba samahani kama yeye alivyofanya na nikakaribishwa. Nilichoomba ni kutaka kufahamu yuko wapi mwanadada. Nikajibiwa ni Moshi. Bahati nilikuwa njiani kuelekea Arusha na wakati huo niko Mombo kwenye vijiwe vya mulo wa wasafiri. Nikaomba tukutane mida ya saa 11. Nikakubaliwa.

Nilikaa karibu na kituo kikuu cha polisi pale moshi nikila. Watu waliingia na wengine kutoka. Nikahisi nimemuona huyo mwenye sauti nzuri akiingia. Kwa kutaka uhakika na baada ya kupata sms kwamba kishafika hapo, nikapiga ili tuangaliane. Bhana weeee! Aliyepokea huyoooo! Ni tofauti na ninayedhania. Sauti haikuendana na muhusika. Bila kupoteza muda nikazima simu yangu, soda nikaibugia haraka na kuwahi gari langu kwa safari ya Arusha.

Haikuwa vizuri kwa mwenzangu lakini uzalendo ulinishinda. Nadhani pamoja na mitandao, hebu turudi kwenye enzi za kufahamiana uso kwa uso.
 
Alikuwa na sauti tamu kama Halima Mdee?

Mmoja kati ya wanawake wenye sauti tam sana duniani (boysh voice), mwingine ni Toni Braxton
Rare sana kupata voice box hizo
 
umenikumbusha rafiki yangu alipata jamaa wanawasiliana ilikuwa wrong number. siku wanataka kuonana kumbe ni booongeeeee ya baba.
kamfata bishost akamuita kwa jina, shost ikabidi amwambie achana na mie umenijulia wapi.
alijikausha kama si yeye. tulimcheka hatari mwishowe akaacha kuonana na wrong number wake
 
Alikuwa na umri gani? Manake mambo ya hivyo hufanywa na watu either underage au hawajitambui. Kuonana na mtu sio dhambi, na hata ukionana nae haimaanishi kuwa mtakuwa wapenzi...so childish!!
 
Mdada alikuwa anataka kwenda Airport akisafiri kutoka Dar kwenda Mwanza. Akapiga simu ili kuita taxi ya kumpeleka Airport akakosea namba. Aliyepokea ni mwanaume ni kwa mipango ya Mungu naye alikuwa anasafiri siku hiyo hiyo kuelekea Mwanza na ndege ile ile. Kila mmoja akawa amevutiwa na sauti ya mwenzake. Mkaka baada ya maswali mawili matatu akafahamu kwamba alikuwa anaita taxi ili aende Airport hili na lile njemba ikaomba kama hakuna tatizo ikamchukue kwani naye anakwenda Airport kusafiri kuelekea Mwanza. Mdada hakuwa na hiyana. Baada ya kuonana kila mmoja mbali na sauti akawa kavutiwa na muonekano wa mwenzie na wakasafiri pamoja na kufanya yao walipokuwa Mwanza na yale yaliyowapeleka kule. Haikupita muda mrefu wakaamua kufunga pingu za maisha.
 
Samahani mkuu hii movie inaitwaje ??
 
Katika siku uliyoharibu ni siku hiyo. Mwanaume jiamini, ungesalimiana nae, mkachonga moja mbili, kama hakuvutii sie wanaume tunajua jinsi ya kumkataa mwanamke usiyemtaka. Kwa kuzima simu na kutoka nduki hujamtendea haki, hao mara nyingine huwa na bahati akakuunganisha na biashara au jambo lolote la faina pasipo ww kumsholola, mnabaki marafriki.
 
me ishawah nitokea kitu kama hii mkaka kakosea no
yuko tanga me nko dar akavutiwa na saut kanitongoza wee kwenye simu kumbuka bado hatujajuana
mimi sikua tayar kudate na mtu
simfaham sura
basi weee siku kafunga safar kuja dar kuniona duuu nilitok ndukii
mtu mwenyewe haendan na saut yakee daaaah ladies watchout
hao watu wa namna hii aseee
 
Alikuwa na umri gani? Manake mambo ya hivyo hufanywa na watu either underage au hawajitambui. Kuonana na mtu sio dhambi, na hata ukionana nae haimaanishi kuwa mtakuwa wapenzi...so childish!!

Alikuwa kama 17-18 kama sijakosea. Ilikuwa utoto kweli.
 
Me pia nashangaa wanawake huwa wanavutiwa na sauti yangu..
 
alikuwa na umri gani? Manake mambo ya hivyo hufanywa na watu either underage au hawajitambui. Kuonana na mtu sio dhambi, na hata ukionana nae haimaanishi kuwa mtakuwa wapenzi...so childish!!

umeongea point mkuu mbona hata humu nimeonana na watu wengi wake kwa waume na sijaona tatzo lolote mpaka sasa
 
Back
Top Bottom