Utani wa Makabila: Ijue Historia ya utani wa Makabila Tanzania

Mpevu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,805
173
Wakuu,

Nimezaliwa katika kizazi hiki cha dotcom na nikaikuta Tanzania ikiwa hai, ndani ya jamii ya nchi yetu hii nikakuta kuna muingiliano mkubwa wenye bashasha miongoni mwa wananchi. Ndani ya mipaka ya nchi hii ikajengwa hulka na tamaduni za kuondoleana utofauti kwa misingi ya dini, jinsia ukabila, ukanda n.k. Kinachonifanya kutafakari ni juu ya suala la Utani wa Makabila.
  • Je, ni nini kilikuwa chanzo cha kuanzisha utani wa kikabila (Mfano Wanyamwezi na Wagogo - WATANI)
  • Je, ni hali tuliyoirithi toka kwa wakoloni ama ilianza punde tulipopata uhuru?
  • Nani muanzilishi wa kutambulisha kabila hili ni watani wa kabila fulani?
  • Je, hali hiyo ya utani bado ipo mpaka leo na ikiwa hai au imebaki kuparurana tu?
  • Kwa wale mliokula chumvi nyingi, hali ya utani wa makabila ilijenga au lah!
Nawasilisha na naomba kusaidiwa kujuzwa ili niweze kufahamu juu ya hili, mniwie radhi iwapo nitakuwa nimeikosea jamii yetu kwa kuweka hoja hii mbele yenu.

----
BAADHI YA MICHANGO YA WANA-JF

Utani ni jambo la kawaida kabisa katika jamii zetu, na hususan sisi Waafrika. Yapo baadhi ya makabila yamekuwa yakiutumia utani kama chanzo cha kuhamasisha watu katika kufanikisha baadhi ya mambo fulani fulani muhimu katika jamii yao pindi yanapoonekana yamelegalega ama kwa uzembe, bahati mbaya au makusudi.

Kwa mfano, makabila ya Wangoni na Wahehe ni watani wa hali ya juu sana kiasi kwamba, wanaweza wakautumia utani wao hata katika mikusanyiko ya watu wengi pasipo kuzuka aina yoyote ile ya tafrani wala kinyongo miongoni mwao. Hii ni kwa sababu tu wanaelewa kuwa wao ni watani na vile vile wanafahamu fika kuwa kama mtu anapenda kutania pia ni lazima akubali kutaniwa.

Utani huu wa Mngoni na Mhehe unaweza kumfanya mmoja wao hata kuzuia maiti asizikwe katika hali ya utani, lakini mantiki yake hasa inakuwa ni kutaka kuchangisha fedha ambazo kwa namna moja au nyingine zitaendelea kuwasaidia watu wote katika shughuli za msiba huo. Hivyo kwa kuwa watu wote wa makabila hayo mawili wanauelewa utani huo hapo huwa hakuna kinyongo kati yao.

Tukiachana na utani kama huo wa makabila ambao ulianza enzi na enzi kutokana na mambo kadhaa ya kihistoria ya mababu zetu, vile vile katika jamii zetu kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kuzungumza kwa wakati wote bila kuongezea maneno mawili matatu ya utani katika kuzifurahisha nafsi zao na wale wanaozungumza nao. Jambo ambalo ni zuri katika mkao wa mazungumzo ya kawaida.

Kundi jingine la hawa wapenda utani kwa kweli hili ndilo nisilolipenda kabisa, na sidhani kama kuna mstaarabu yeyote ambaye anaweza akalipenda kwa kuwa halina mwelekeo wa kistaarabu hata kidogo.

Unamkuta mtu kakaa katika kundi la watu, mara baada ya wewe kufika sehemu hiyo anakupokea kwa maneno kibao ya utani, na kati ya hayo maneno mengine ni ya kukudhalilisha mbele za watu. Kisa? Kwa sababu tu yeye anapenda kutania! Anafanya hivyo bila hata ya kuelewa kuwa una uhusiano gani na watu wengine katika kundi hilo, kwa maana si kila utani unafaaa wakati wote mbele za watu wote.

Kwa kuwa wewe ni mstaarabu, unaamua kukaa kimya na kumwacha huyo bwana mpenda utani aendelee na utani wake usioangalia mipaka wala aina ya utani wakati wote.

Cha ajabu ni kwamba baada ya muda mtu huyo huyo aliyekuwa mstari wa mbele kutoa maneno kibao ya utani anapotokea mtu mwingine na kumtania yeye anakuja juu kama moto wa kifuu cha nazi, na kuwaacha wastaarabu wengine wote wakimshangaa kwa jinsi anavyobwatuka!

Hapo mimi nashindwa kuelewa, mtu kama huyo akilini mwake anawaza nini? Hivi alivyokuwa akiwatolea maneno kadhaa ya utani wengine hakufikiria kuwa na wao pia ni binadamu kama yeye, sasa mbona yeye anapotaniwa anakuja juu? Je, mtu huyo anajua kweli utani ni nini au yeye anapenda kuwafanyia wengine hivyo katika mazingira ya kufurahisha nafsi yake tu bila ya kuangalia athari zake kwa wengine pia?

Hayo siyo mambo, kama wewe unapenda kutania unatakiwa uwe tayari kutaniwa vilevile, kwa maana mkuki ni mchungu hata kwa nguruwe pia, si kwa binadamu tu.

Pamoja na yote hayo, lakini inatulazimu tujue ni nani na ni wakati gani wa kutoa maneno ya utani, kwa maana watu wengine kwa kuwa umezoea kutaniana nao, basi wao kila mahali wakikukuta wanaanza kukutania bila hata kujiuliza, je, mtu huyo anayemtania yupo na nani na katika mazingira gani?

Unaweza ukamtania mtu, kumbe yupo na mkwewe ukajikuta umemzulia kasheshe mbele ya safari yake, hivyo kama unapenda utani mbali ya kujua kuwa ni lazima ukubali kutaniwa pia, vile vile inakulazimu utambue kuwa utani una mipaka yake.

CHANZO CHA UTANI WA WAHEHE NA WANGONI

Wangoni ndio kabila ambalo ni watani wa jadi wa Wahehe, moja ya sababu ambazo hutajwa kuwa sababu ya utani huu ni kuwa katika vita za kikabila zilizokuwa zikiendelea kabla ya ujio wa wakoloni, Wahehe na Wangoni waliwahi kupigana na hakukupatikana mshindi, na kuanzia hapo walianza utani kila moja akitamba kuwa bora kuliko mwenzie.

Utani wa makabila haya mawili ni utani wenye heshima watu wa rika moja ndio ambao hutaniana, hauhusishi matusi kama ulivyo utani wa baadhi ya makabila. Na utani huu hugeuka nyenzo muhimu ya kusaidiana wakati wa misiba ambapo watani husaidia kukusanya michango na kufanya kazi ambazo zinawapunguzia mzigo wafiwa.
 
Nadhani ilikuja tu automatically. Starting point ni kujua haya mambo yalianza lini. Hii ya wahaya na waha sio common sana lakini nasikia enzi hizo wazungu walipokuja Kigoma wakauliza "What tribe you?" wakasema "Baha". Walipoenda Bukoba wakauliza "Are you also Baha?" wakajibu "Yeah". Kwa hiyo ile "ya" ikaongezwa mwisho kuwa "Bahaya".
 
Angalau naanza kupata pointi, naomba na wengine tutafute majibu
 
Utani ni jambo la kawaida kabisa katika jamii zetu, na hususan sisi Waafrika. Yapo baadhi ya makabila yamekuwa yakiutumia utani kama chanzo cha kuhamasisha watu katika kufanikisha baadhi ya mambo fulani fulani muhimu katika jamii yao pindi yanapoonekana yamelegalega ama kwa uzembe, bahati mbaya au makusudi.

Kwa mfano, makabila ya Wangoni na Wahehe ni watani wa hali ya juu sana kiasi kwamba, wanaweza wakautumia utani wao hata katika mikusanyiko ya watu wengi pasipo kuzuka aina yoyote ile ya tafrani wala kinyongo miongoni mwao. Hii ni kwa sababu tu wanaelewa kuwa wao ni watani na vile vile wanafahamu fika kuwa kama mtu anapenda kutania pia ni lazima akubali kutaniwa.

Utani huu wa Mngoni na Mhehe unaweza kumfanya mmoja wao hata kuzuia maiti asizikwe katika hali ya utani, lakini mantiki yake hasa inakuwa ni kutaka kuchangisha fedha ambazo kwa namna moja au nyingine zitaendelea kuwasaidia watu wote katika shughuli za msiba huo. Hivyo kwa kuwa watu wote wa makabila hayo mawili wanauelewa utani huo hapo huwa hakuna kinyongo kati yao.

Tukiachana na utani kama huo wa makabila ambao ulianza enzi na enzi kutokana na mambo kadhaa ya kihistoria ya mababu zetu, vile vile katika jamii zetu kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kuzungumza kwa wakati wote bila kuongezea maneno mawili matatu ya utani katika kuzifurahisha nafsi zao na wale wanaozungumza nao. Jambo ambalo ni zuri katika mkao wa mazungumzo ya kawaida.

Kundi jingine la hawa wapenda utani kwa kweli hili ndilo nisilolipenda kabisa, na sidhani kama kuna mstaarabu yeyote ambaye anaweza akalipenda kwa kuwa halina mwelekeo wa kistaarabu hata kidogo.

Unamkuta mtu kakaa katika kundi la watu, mara baada ya wewe kufika sehemu hiyo anakupokea kwa maneno kibao ya utani, na kati ya hayo maneno mengine ni ya kukudhalilisha mbele za watu. Kisa? Kwa sababu tu yeye anapenda kutania! Anafanya hivyo bila hata ya kuelewa kuwa una uhusiano gani na watu wengine katika kundi hilo, kwa maana si kila utani unafaaa wakati wote mbele za watu wote.

Kwa kuwa wewe ni mstaarabu, unaamua kukaa kimya na kumwacha huyo bwana mpenda utani aendelee na utani wake usioangalia mipaka wala aina ya utani wakati wote.

Cha ajabu ni kwamba baada ya muda mtu huyo huyo aliyekuwa mstari wa mbele kutoa maneno kibao ya utani anapotokea mtu mwingine na kumtania yeye anakuja juu kama moto wa kifuu cha nazi, na kuwaacha wastaarabu wengine wote wakimshangaa kwa jinsi anavyobwatuka!

Hapo mimi nashindwa kuelewa, mtu kama huyo akilini mwake anawaza nini? Hivi alivyokuwa akiwatolea maneno kadhaa ya utani wengine hakufikiria kuwa na wao pia ni binadamu kama yeye, sasa mbona yeye anapotaniwa anakuja juu? Je, mtu huyo anajua kweli utani ni nini au yeye anapenda kuwafanyia wengine hivyo katika mazingira ya kufurahisha nafsi yake tu bila ya kuangalia athari zake kwa wengine pia?

Hayo siyo mambo, kama wewe unapenda kutania unatakiwa uwe tayari kutaniwa vilevile, kwa maana mkuki ni mchungu hata kwa nguruwe pia, si kwa binadamu tu.

Pamoja na yote hayo, lakini inatulazimu tujue ni nani na ni wakati gani wa kutoa maneno ya utani, kwa maana watu wengine kwa kuwa umezoea kutaniana nao, basi wao kila mahali wakikukuta wanaanza kukutania bila hata kujiuliza, je, mtu huyo anayemtania yupo na nani na katika mazingira gani?

Unaweza ukamtania mtu, kumbe yupo na mkwewe ukajikuta umemzulia kasheshe mbele ya safari yake, hivyo kama unapenda utani mbali ya kujua kuwa ni lazima ukubali kutaniwa pia, vile vile inakulazimu utambue kuwa utani una mipaka yake.
 
Nafikiri ilikuwa ni strategical moves ya Nyerere kuwaunganisha watanzania na ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Kwani umewahi kusikia makabila ya jirani zetu waKenya ama kule Rwanda wakitaniana??
 
Hii ilitokana na vita vya enzi hizo za mababu zetu, mfano wangoni walipoingia Bongo toka South, waliingia Sumbawanga wakapiga kule, wakapita Tabora wakatwanga wanyamwezi na wasukuma, Iringa furusha wahehe, na wabena halafu ndo waka settle SONGEA/RUVUMA. sasa huko walikopita kote hawa sasa hivi ni watani wa WANGONI- Wafipa, wasukuma, wanyamwezi, wahehe, na kuna makabila menine madogo madogo na si strategy ya Nyerere wala mtu binafsi hii ni HISTORIA.
 
Hii nadhani ina ukweli wenyewe, wengine tuanzie hapa kupata point za kuchangia,
BIG UP
 
Utani ni matokeo ya vita. Makabila mengi ambayo ni watani yaliwahi kupigana zamani. hata Wahehe na wajerumani ni watani.

Ila, cha ajabu wewe ni mmoja wa wanaoiba mitihani? Una sababu gani ya kudokezwa kuhusu mtihani, soma ujibu swali lolote litakalokuja. Ndio maana mnakuwa na elimu bila maarifa.
 
Kibongo bongo watu wanataka kufaulu tuu mambo mengine baadae no wonder pale tunapolizwa na wajanja tunaanza kulalamika kumbe elimu yetu ni ya kubabia babia!!
 
Hii ilitokana na vita vya enzi hizo za mababu zetu, mfano wangoni walipoingia Bongo toka South, waliingia Sumbawanga wakapiga kule, wakapita Tabora wakatwanga wanyamwezi na wasukuma, Iringa furusha wahehe, na wabena halafu ndo waka settle SONGEA/RUVUMA. sasa huko walikopita kote hawa sasa hivi ni watani wa WANGONI- Wafipa, wasukuma, wanyamwezi, wahehe, na kuna makabila menine madogo madogo na si strategy ya Nyerere wala mtu binafsi hii ni HISTORIA.

Mkuu,
Si kweli kuwa waliwatwanga Wanyamwezi. No no no. Kwa wasukuma ndiyo hawakufika kabisa. Wangoni walikuja na vimipapa mipapa vyao na wakakutana na Wanyamwezi. Zilipigwa hadi wakaipata habari yao. Kama sikosei iliishia kutoka suluhu na Wangoni wakarudi nyuma. Yaani katika movement zao kutoka South Africa, walipiga kila kabila na wakaja kukwama kwa Wanyamwezi. Wengi waliamua kurudi na kwenda kuishi Songea na huku baadhi wakiajiriwa kwenye majeshi ya Mtemi Milambo (Maiti) kama askari wake waitwao Valugaluga (hili jina ni tusi, hii ni ile dudu ya mwanaume). Hawa jamaa walikuwa wakisifika kwa kuvuta bangi na hapo wanakuwa hawaogopi kitu.

Mtemi Mirambo akaanza kuchapa makabila ya karibu na Tabora na kuifanya Empire yake kuwa kubwa sana. Akaenda kwa Wafipa (Hadi leo tuna utani na Wafipa). Shinyanga na Mwanza ilikuwa ni makubaliano tu kuwa TUUNGANE na haikupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Hakutaka kwenda Mkoa wa Mara. Wahaya walikuja na kutangaza urafiki na Wanyamwezi. Mteni Nyunguyamawe enzi zake. Kwa sababu hatukupigana na Wahaya, ndiyo maana hatuna utani nao. Singida walikuali kuingizwa chini ya himaya yake bila vita.

Matatizo yalianza Dodoma. Wagogo walimdindia Mirambo na nafikiri walikuwa wakisumbua katika biashara zake. Basi akawavamia na zikapigwa si kawaida. Ilifika wakati Mirambo na Walugaluga wake wakawa wameishiwa risasi. Basi wakawa wamejifungia ndani ya nyumba fulani, wakawa wanavunja mawe na kutumia kama risasi. Ikafika point wakawa wameishia hata baruti maana enzi hizo risasi inawekwa na mwisho unaweka pamba na unga wa baruti.

Wagogo kusikia kimya wakafahamu Milambo kaishiwa. Wakaenda na kumwambia kuwa "tunakuachia, hatutakudhuru. Ila uende na usirudi tena". Kutoka hapo Mirambo akawa na heshima kubwa sana na upendo kwa Wagogo. Ila ikaacha UTANI wa hali ya juu hadi leo. Ndiyo maana ninaweza kusema "Malecela Mjinga Sana" na asinifanye kitu.

Ya
 
1. Nasikia Wazaramo walikuwa Wagogo zamani. Kulipotokea shida ya Chumvi, wakaamuwa kuwatuma wenzao waende Pwani kununua Chumvi na kuileta Dodoma. Jamaa walipofika Pwani wakaamua kubaki huko Milele. Kwa maana nyingine kwa Kiswahili cha kisasa ungesema "Walizamia" na hii ndiyo mwanzo wa jina la WAZARAMO yaani Walizaramia.

2. Wagogo zamani walikuwa Wazaramo. Kulipotokea Msiba huko pwani, wakaamua kuwatuma wenzao waende Dodoma kununua Mbuzi kwa ajili ya Arobaini. Jamaa wakaenda Dodoma na kufika huko, wakala zile hela za kununulia mbuzi na hawakurudi. Wazee wa pwani wakakaa na kuwaombea Albadiri (laana) na Wagogo hadi leo wana matatizo ya macho (Matonya and Comp.)

Sasa sijui kipi kina ukweli. Ila hawa jamaa wamekuwa watani hadi kesho.
 
Back
Top Bottom