Vijana sasa wanafanyia utani mkasa wa mwanaume kuangamizwa na mamba

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Tuliza mihemko yako, haya sasa.

Fikiria ni kuwa huyo anaefanyiwa utani kwenye mitandao ni baba yako, kaka yako, mjomba etc.

Vijana huko kwenye mitandao wanataka umaarufu bila ya kujali utu. Sasa wanamuiga yule mama anavyoongea akisimulia jinsi mamba alivyo muangamiza mumewe.

Ile ongea yake na story telling sasa watu wamefanya kama fursa ya kufanya utani mitandaoni huku wakisahau ishu wanayofanyia utani inajumuisha na uhai wa mtu uliotoweka na majonzi yaliyobaki kwa ndugu.

Kama na wewe una support ufala huo huku ukicheka cheka basi hayajakukuta mambo.

Ni kweli mama ongea yake inafurahisha lakini haimaanishi sasa muanze kuifanyia mzaha.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli Siyo Busara, Uungwana, Hekima Kufanya Utani, Mzaha Na Kifo Cha Mtu
Hata Nami Nimeona Watu Wanatania Sana Na Kuchora Katuni Hovyo
utu Ni Bora Kuliko Kitu.
 
Nadhani hakuna taifa lina watu wengi wanaopenda sifa za kipuuzi na kushadadia mambo ya kijinga kama Tanzania.
 
tulipoambiwa dunia itachoka sikuwa naelewa, kwa picha ya haraka' akilini ingekuja milima mabonde mito nk imepauka kwa rangi ya kijivu na hudhurungi.

Maadili yameporomoka sana, hapa ndiyo utaona ni kwa nini wenye maono yao walikuwa wanazuia sana utandawazi usiingie nchini, Nyerere na sera zake za ujamaa na kujitegemea was the best for humanity.

Hakuna jinsi wacha tuogelee kwenye bahari iliyochafuka.
Muhimu vaa swimming gears za silicone uchafu usipenye, ila si rahisi,
siku hizi ukisema ujumuike na watu kidogo tu kama akili yako haijajiandaa na bullshits utakereka haraka sana, siku moja niko hospitali tu,(hata si eneo la burudani) mtu anafungulia kwa sauti kusikiliza video zake za hovyo.

Ndiyo hivyo utandawazi umetufikisha hapa.
 
tulipoambiwa dunia itachoka sikuwa naelewa, kwa picha ya haraka' akilini ingekuja milima mabonde mito nk imepauka kwa rangi ya kijivu na hudhurungi.

Maadili yameporomoka sana, hapa ndiyo utaona ni kwa nini wenye maono yao walikuwa wanazuia sana utandawazi usiingie nchini, Nyerere na sera zake za ujamaa na kujitegemea was the best for humanity.

Hakuna jinsi wacha tuogelee kwenye bahari iliyochafuka.
Muhimu vaa swimming gears za silicon uchafu usipenye, ila si rahisi,
Siku hizi ukisema ujumuike na watu kidogo tu kama akili yako haijajiandaa na bullshits utakereka haraka sana, siku moja niko hospitali tu,(hata si eneo la burudani) mtu anafungulia kwa sauti kusikiliza video zake za hovyo.

Ndiyo hivyo utandawazi umetufikisha hapa.
Siku hizi ukiongea sense ndio unaonekana mshamba.

Ila watu wajinga ndio wanao trend.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom