Hemed Maronda
Senior Member
- Oct 27, 2010
- 138
- 43
Mkuu nashukuru kwa taarifa maana jamaa alikuwa anajituma kufanya kazi kwa umakini lakini yawezekana labda alipigiwa hesabu kubwa za kodi na TRA kwa kuwa alikuwa anawachachafya sana Serfikali.Moto moto lilikuwa la jamaa mmoja anaitwa Justin amefilisika kwa sasa
na Alasiri nalo je unalikumbuka?Je Dar leo vp na hlo!
Alasiri? Nahici yameuliwa na Shigongo.
Pia kulikuwa na gazeti Family Mirror, sijui limeishia wapi.
Kulikuwa na gazeti moja la kila wiki JITAMBUE! Lilikuwa lina habari nzuri za kufungua watu
Hilo jina JITAMBUE limekaa kiuamsho uamsho hivi...
Mimi nililipenda "WAKATI NI HUU" la Kajubi Mukajanga!
Pia lilikuwepo "HEKO" nadhani lilikuwa la yule mwandishi mahiri: Marehemu Stanley Kamana, baada ya "kusogezwa" ikulu na rafikiye Mkapa, akapotelea huko huko!
Nasikia Tanzania Daima na Mwanahalisi R.I.P ni magazeti ya viongozi wa Chadema.