Haya Magari Yanauzwa Na TRA Kwa Mnada Yana Ubora Kiasi gani

markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
12
Ndugu wana JF, Napenda kuwauliza wenye uzoefu kuhusu magari yanauzwa na TRA kwenye Mnada wao unaofanyika kila tarehe ya mwisho wa mwezi yana ubora gani? Je yanapatikana kwa bei nafuu kidogo au? Yeyote mwenye detailed information anaweza kunisaidia mimi na wengine ambao hawana information
 
hayo magari ndio wanayo wanyang'anya walala hoi kwa kodi za ajabu bandarini + storage charges. Watu wakisusa ndio wanauza kwa unafuu mara nyingi mazuri huwa wanajiuzia wenyewe kwa mujibu wa wahusika (walio dhulumiwa) na hawa wahuni tena kama wanajipa bure na kulipa taifa hasara.

Si ajabu watu wanahamua kuwaletea mikweche kwa sababu ya ushuru wa jabu if im honest wa kukomoana.
 
Na TRA ndo wanasuka dili nyingi za wizi wa magari na kuyatafutia usajili kisha kuyauza tena.
 
haya magari yanakuwa kwenye ubora sana kwani ni mapya kabisa watu wanakuwa wameshindwa kulipa ushuru au watu wanacheza mchezo akitajiwa ushuru mkubwa+storage wanachofanya wanacheza dili linaingizwa kwenye mnada kisha anakuja kununua kwa bei poa kabisa ya kupanga mezani na pia wateja wakubwa ni wahindi na wenye mashow room ndio wanunuzi wakubwa yale yolochoka sana ndio ukienda utayakuta mengine utakuta yameshabandikwa sold siku ya mnada na ukiwa na mtu pale unapanga bei unachagua kabla ya siku ya mnada
 
mkuu shukrani kwa taarifa hii, nami ngoja nijikongoje mnada ujao. itakuwa lini mkuu mnada ujao na huwa unafanyikia wapi na je ni ruksa kwenda kukagua kabla ya siku ya mnada na jee ni vipi kuhusu ushuru na mazagazaga mengine?
 
Asante, sana kwa ushauri wenu. Mnada utakuwa tarehe 31 march 2011 bond 270. Naomba wenye ufahamu na hiyo bond mahali ilipo watuelekeze.
 
Kama una hela nunua tu mkuu maana hayo magari bwana yaliagizwa na watu kwa ajili ya kuyatumia wao au kwa ajili ya biashara ila kutokana na wao kushidwa kuyaKomboa kwa sababu za kusababishwa na wao wenyewe au TRA inafika point yanapigwa mnada.Hawa jamaa bwana wanamifumo mibovu sana unaweza ukaagiza gari ukawa na hela yako ya kukombolea lakini ukazungushwa weeee mpaka mwisho wa siku unakuta peneti kibao unatakiwa kulipa na gharama inakua hata mara mbili ya bei uliyonunulia hilo gari lenyewe ,basi walala hoi wanakubali yaishe kwa kuyaacha hayo magari hapo TRA.Kimsingi mengi nimazuri since mtu huwezi agiza gari baya.
 
mkuu shukrani kwa taarifa hii, nami ngoja nijikongoje mnada ujao. itakuwa lini mkuu mnada ujao na huwa unafanyikia wapi na je ni ruksa kwenda kukagua kabla ya siku ya mnada na jee ni vipi kuhusu ushuru na mazagazaga mengine?

mnada hujao utakuwa mwisho wa mwezi huu unafanyikia kule bandarini ,kukagua kabla ya mnada mpaka uwe na m2 wa kukushika mkono, ukishanunua umemaliza akuna ushuru kwani hyo bei unayouziwa inakuwa na kila kitu ata ukiuziwa 2m
 
thanks mkuu
 
TRA ni sababu kubwa ya watu kutotoa magari yao na kuyatelekeza. Huwa wanachelewesha kwa makusudi kuwapatia watu tax liabilities zao ili walipe na kutoa mizigo kwa kula dili na watu wa storage nao wapate chao I think TICTS. Sasa inapotokea mtu anataka kutoa mzigo wake(Including gari) on time wanamzunguusha sana, ninakumbuka niliwahi agiza gari ilikuwa balaa yaani kama si kuwa na mtu ninaye mfahamu TRA aliyeweza kunisimamia kwa misingi ya haki kama itakiwavyo kwa wateja wote baada ya kuona jamaa wananiumiza ili niwapatie kitu, jamaa anasema walikuwa walifiche file langu na lingeonekana baada ya miezi mitatu gari bandarini, yaani niliogopa sana nikasema Tanzania tunahitaji reform ya hali ya juu kwenye sheria za forodha.

Kwa kuwa bunge letu ni rubber stamp ila kama ingekuwa nchi za kidemokrasia mtu unapeleka muswada binafsi wa kutaka mtu aanze kuwa charged storage siku tano za kazi baada ya kukabidhiwa Tax liability estimate na kusign kuwa kaipata toka TRA. Hii itawafanya TRA kufanya kazi kwa kasi ya ajabu na bila urasimu hata kama watamchelewesha mtu kwa mwaka haitakuwa tatizo. Ila hii minada tunayoinona ni abuse ya sheria za ushuru wa forodha.
 
TRA ni sababu kubwa ya watu kutotoa magari yao na kuyatelekeza. Huwa wanachelewesha kwa makusudi kuwapatia watu tax liabilities zao ili walipe na kutoa mizigo kwa kula dili na watu wa storage nao wapate chao I think TICTS. Sasa inapotokea mtu anataka kutoa mzigo wake(Including gari) on time wanamzunguusha sana,.

Hii jambo ni kawaida kabisa pale TRA mara utaambiwa mhusika kafiwa yuko Mwanza atarudi baada ya wiki....Je ina maana mhusika ni mtu mmoja mtu TRA nzima?....Utaona vijana wengi watumishi TRA pale longroom wengi wao ni wafanya biashara na kila mmoja wao anataka ajenge Ghorofa kwa muda mfupi anayeumia ni sisi wanyonge tunao anza alif kwa kidole.

.... Tanzania tunahitaji reform ya hali ya juu kwenye sheria za forodha.
Kwa kuwa bunge letu ni rubber stamp ila kama ingekuwa nchi za kidemokrasia mtu unapeleka muswada binafsi wa kutaka mtu aanze kuwa charged storage siku tano za kazi baada ya kukabidhiwa Tax liability estimate na kusign kuwa kaipata toka TRA. Hii itawafanya TRA kufanya kazi kwa kasi ya ajabu na bila urasimu hata kama watamchelewesha mtu kwa mwaka haitakuwa tatizo. Ila hii minada tunayoinona ni abuse ya sheria za ushuru wa forodha.

Ukiangalia bunge letu la leo ni la kibiashara tu....Nimejiuliza kwa nini mbunge antumia mamilioni ya pesa ili apate ubunge?...Jibu ni kuwa zile pela ni investment ambayo ina high returns...kwa hiyo baada ya miaka mitano huyo mbunge anahakikisha amerudisha gharama zake na faida maradufu.

Kwa hiyo saa ngapi atakuwa na muda wa kutuangalia siye tuliyempa hio kazi? Mpaka hapo tutakapo pata viongozi,watumishi wenye maadili ya kazi na siyo ubinafsi.
 
jamani hii CCM ni lini tu Mungu itaondoka madarakani< really! its painfull to watch this! very sad!
 
mwanatanu; [FONT="Tahoma" said:

[/FONT]

nadhani faida mara tano mkuu
 
Nimeshindwa pakuweka wapi hii taarifa ila naomaba niiweke hapa
''ENEO LENYE NYUMBA, FREM NA KONTENA MOJA LINAUZWA.
PIA LINA HATI YA MAKAZI NA BIASHARA'' Eneo lipo Tabata bima
iliopo shule ya St. Marry's. tuwasiliane kwa 0713852625. Ahsante!
 
jamani hii CCM ni lini tu Mungu itaondoka madarakani< really! its painfull to watch this! very sad!

Aah, kila kitu ccm, hata uzembe wa watumishi unawatupia ccm, acha hizo. Lawama nyingine elekeza kwa wahusika moja kwa moja ccm inahusika nini na TRA, kama sio ndugu zako wanaofanya kazi huko?
 
mnada hujao utakuwa mwisho wa mwezi huu unafanyikia kule bandarini ,kukagua kabla ya mnada mpaka uwe na m2 wa kukushika mkono, ukishanunua umemaliza akuna ushuru kwani hyo bei unayouziwa inakuwa na kila kitu ata ukiuziwa 2m

Du na kama milioni 4 kwenye akaunti je naweza nikapata gari bomba?
 
Tafadhalini Wadau walio wahi kununua plz tupeni data zaidi, mfano aina ya gari, mwaka wa kutengenezwa, bei etc.maana hata mimi napango wakutafuta kausafiri kadogo kama duet
 
Back
Top Bottom