Haya madini yanafanya kazi gani kubwa, mpaka kupewa thamani kubwa?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,483
40,498
Huwa najiuliza, haya madini kama: almasi, dhahabu, Tanzanite n.k ni kitu gani kinayapa thamani au yanafanya kazi gani kubwa yanayoendana na thamani ya mauzo?

Kwa ufahamu wangu mdogo, najua yanatumika kwa mapambo, kukatia vioo na miamba (almasi); lakini, kwa nini yanathaminishwa kwa gharama kubwa?

Au yana matumizi makubwa mengine yaliyojificha?

Ukiniuliza ni madini gani ningependa yawe na thamani kubwa kuliko dhahabu, almasi n.k, ningependekeza 'copper', 'aluminium', chuma n.k kwa sababu mahitaji na matumizi yake makubwa yanajulikana.

Wakuu, tujadili; kwa nini yanapewa thamani kubwa wakati yanafanya kazi za kawaida sana.
 
Kutokupatikana kwa urahisi na gharama kubwa ya uchakataji wake, hayo yote yamepelekea binadamu tangu enzi na enzi kukubaliana kuyapa thamani
 
Kutokupatikana kwa urahisi na gharama kubwa ya uchakataji wake, hayo yote yamepelekea binadamu tangu enzi na enzi kukubaliana kuyapa thamani
Unamaanisha, walithaminisha kutokana na upatikanaji wake, na si kwa matumizi yake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom