Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,978
- 5,025
Nilikuwa nachukizwa sana na waandishi wa habari namna walivyokuwa wanaandika vitu vya uongo kuhusu lile sakata la madaktari na hatma ya Ulimboka. Hasa waandishi wa tz daima na washabiki wengine wa jf. Kila siku kuulizia,dr atasema lini? Wengine wakaja kusema kalipwa hela kama walikuwa wanataka kuchukua hatua zozote. Kuna wengine walimchangia matibabu, tunashukuru na werevu walishajua baada ya madaktari kuacha wenzao wakifukuzwa na wao kurudi kazi hakuna cha muhimu kingefanyika. Sasa, tumechukua hatua gani baada ya kuambiwa mara tatu ighondu ndo mtekaji wake? Kuna aliyejitokeza kupigia kelele hata tume ya kova itoe majibu? Nani anaweza kwenda kumkamata ighondu? Inabidi tujipange upya katika kila mmoja kupigania haki zake. Hili la watu kutojua haki na wajibu wao ndo linasababisha viongozi kila siku wanatoa majibu ya uongo ili mradi muda upite. Wanajua watanzania hatujui haki na wajibu wetu hivyo yote yatapita tu.