Your assesment is so all inclusive to be meaningless. Of course kuna kitu kimefanya tuwepo. Uki include " nature au kitu au mtu au mungu" hujaacha kitu, na ni pointless kuongea hivi. Swali linakuja, kilichotufanya tuwepo ni nini? Wengine wanasema ni mungu (watu wa dini) wengine wanasema dini haiwezi kuonyesha kwamba mungu aliumba ulimwengu, na mpaka sasa the best explanation ni kwamba kuna kanuni za nature ndizo zilizoumba, lakini tunafika sehemu tunashindwa kuelewa hizi kanuni za nature zimetoka wapi, kwamba katika singularity iliyoanzisha time and space katika universe hii palitokea nini, kwani by definition katika singularity kanuni zetu zote zinavunjika na kunakuwa na 0 space and 0 time wakati kuna infinite mass, lakini kushindwa kuelewa huku hakuna maana kwamba ulimwengu umeumbwa na mungu. Kuna wengine ( kama kina Leonard Susskind katika "The Cosmic Landscape") wanaamini kwamba universe yetu ime branch off kutoka katika universe nyingine, na kwamba kuna universes nyingi katika "multiverse". Na sasa Hawking anatuambia mambo yanaweza kujiendea yenyewe bila mungu.
Tatizo unasema "kwa uwezo wake wa ajabu", wanasayansi wanaamini ulimwengu haujaumbwa kwa uwezo wa ajabu (supernatural powers) bali umeumbwa kwa kanuni za nature ambazo zinaweza kueleweka, na tatizo ni kwamba hatujaweza kuzielewa tu.
Unachosema ni kama vile watu wa zamani walivyosema kwamba radi ni jinsi ambavyo mungu "kwa uwezo wake wa ajabu" anaongea na binadamu. Baadaye wakaja kugundua kwamba radi ni umeme tu ambao hata binadamu anaweza kutengeneza, wala si kitu cha ajabu, ni kitu kinachofuata kanuni za nature.
Kama ulimwengu unaonekana wa ajabu, hili linatokana na upungufu wa elimu yetu tu. Lakini ukiusoma ulimwengu unaeleweka na unafuata kanuni, wala hauna ajabu in the sense ya vitu kufuata supernatural powers, ndiyo maana sayansi inaweza kutufunua macho kila tunavyozidi kuusoma ulimwengu.