Hawa wenzetu Wa-Asia wanatuzidi nini?

Hawa wenzetu Wa-Asia wanatuzidi nini?

Hawa jamaa hawataki masihara kabisa..[emoji23]
Ila mkuu muda mwengine hutumia njia za panya hawa na sio wao tu hata baadhi ya wabongo nililifahamu hilo rais alipoita wafanyabiashara ikulu kuzungumza nao na hawa wa makodikodi Hawa ni sehemu moja wapo ya kufanya watu watumie njia za panya..
Sisi hata hizo njia za panya hatuzioni....
 
Haujawahi kujiuliza hili swali Malcom!!

Unaanza nao biashara tena kwa kimtaji kiduchu ila wanakuacha unaangalia.

Mifano ninayo mingi.(nisitaje majina)...Kuna huyu mwamba ametoka Pakstan 2010. Akaanza kuuza CD tu leo anamiliki maduka ya spare parts jijini.
Rejea bandiko langu, nimeongezea mengi tu.
 
Hawa jamaa hawataki masihara kabisa..😂
Ila mkuu muda mwengine hutumia njia za panya hawa na sio wao tu hata baadhi ya wabongo nililifahamu hilo rais alipoita wafanyabiashara ikulu kuzungumza nao na hawa wa makodikodi Hawa ni sehemu moja wapo ya kufanya watu watumie njia za panya..
Hakuna njia za panya: Njia za panya dunia nzima ???
Wahindi hata wakienda Marekani au Ulaya wanakuwa matajiri tu.
Leo hii matajiri wakubwa London ni wahindi, mmoja wapo aliwahi kuwa Mtanzania.
 
Wakubwa wanazijua ndugu sema ndo huwezi tafuniwa mkate.. sometimes ona tu Kuna visherehe vya Uma na wakubwa wapo hapo kuwafumbafumba ila picha ya nyuma pazia..[emoji28]

Mkuu ukweli ni huu biashara haramu zinahela sana na angalia huku kwetu mfano wanaoshikwa na hizo haramu wako wapi..? Pesa huenda na wa pesa. Inatupasa tutumie akili kubwa. Mzee baba kufanya mvuto wa chama chake na yeye aligusa vituvitu si unaona vilivyonuka.. he know somethings..[emoji28]
Unalosema linaukweli kwa asilimia ndogo saana mkuu.

Kama Malcom anavyokuambia hawa watu hawatajirikii hapa Bongo tu......Dunia nzima hawa jamaa wanatusua.

Lingine ambalo wanalo ni hawa rudi nyuma wakishatoka kwao.

Wahindi wakishatoka India akaenda Canada, Canada ni kwao.

Sisi tukifika miaka 5 ya mwanzo unajiuliza niishi hapa au nirudi nyumbani...unaishia kuwa na maisha mawili.
 
Hakuna njia za panya: Njia za panya dunia nzima ???
Wahindi hata wakienda Marekani au Ulaya wanakuwa matajiri tu.
Leo hii matajiri wakubwa London ni wahindi, mmoja wapo aliwahi kuwa Mtanzania.
Mkuu najua sio wote wana njia za panya nimegusia hilo Kama njia moja wapo.. ukijaribu kufikiri vizuri hapo unaweza kuona kuna ka mnyororo fulani..😅
 
Unalosema linaukweli kwa asilimia ndogo saana mkuu.

Kama Malcom anavyokuambia hawa watu hawatajirikii hapa Bongo tu......Dunia nzima hawa jamaa wanatusua.

Lingine ambalo wanalo ni hawa rudi nyuma wakishatoka kwao.

Wahindi wakishatoka India akaenda Canada, Canada ni kwao.

Sisi tukifika miaka 5 ya mwanzo unajiuliza niishi hapa au nirudi nyumbani...unaishia kuwa na maisha mawili.
Nalifahamu hilo mkuu biashara huhusisha mengi sikuzote mtu huwa anatengeneza mkakati mzuri ila kuufata sasa! Waafrika tuna tabu zetu
 
Biashara kwa muhindi na mwarabu ni sehemu ya utamaduni. Wenzetu kufanya biashara kumekuwa ni sehemu ya maisha na siyo tu shughuli ya kujiingizia kipato cha kila siku. Leo mtoto wa kihindi hata kama atakuwa yuko shule mnasoma naye, lakini ni lazima atakuwa anapata muda wa kutosha kushinda kwenye duka au ghala la wazazi wake huku akifanya kazi ndogo-ndogo.

Mwisho wa siku huyu mtu anakuwa anapata elimu za aina mbili (Formal and Informal Education), akija kuwa mkubwa atakachokuwa anafanya sehemu kubwa ni marudio ya alichojifunza kutoka kwa wazazi wake. Hili nimelishuhudia sana hata kwa Wachagga wengi. Lakini kubwa zaidi ambalo huwa linakuwepo kwa wenzetu ni utayari wa wanafamilia kutoa mitaji kwa watoto ambao wanaonekana kuweza kufanya biashara.

Lakini sasa wewe ndugu Daby unaweza ukawa ni Massai, lakini sehemu kubwa ya maisha yako umejikita kwenye kusoma (Formal Education) ambayo matokeo yake yanaweza kuja baada ya miaka 14 ya kumaliza shule. Baadae umekosa ajira ndiyo unakumbuka kama wewe ni Massai hivyo unaamua kununua ng'ombe ukitegemea utaweza kufuga, ilhali huna ujuzi wowote wa kufuga (Ulimwacha mzazi wako akafa nao).

Lakini ungekuwa ni massai wa mjini na kijijini naamini kuna vitu vikubwa kuhusu ufugaji ungekuwa unavifahamu kuliko hata mtu wa PhD aliyetoka Sokoine University of Agriculture: AND WHY, it's a generational thing for Massai to be excellent in Pastoralism and Ranching. Hivyo hakuna miujiza, waswahili husema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Kujifunza kwa muda mrefu tena kwa vitendo huku wakisimamiwa na familia: Hii huzaa kijiamini na nidhamu kwasababu huwezi kutumia vibaya fedha ya familia.

KITU KIKUBWA: Utajiri wa kundi la watu (Kabila au dini) mara nyingi huwa ni vizazi (A Genereational thing). Katika matajiri wakubwa hapa Tanzania hasa waashia, utajiri wao unakuwa na mizizi mirefu ya urithi. Watoto hurithishwa kutoka wazazi. Pia huo urithi hauji moja kwa moja, lakini inabidi mtoto autolee jasho na kuupambania kuupata tokea akiwa mtoto ili usije ukapotea.

Marehemu mama yangu aliwahi kuwa rafiki mkubwa sana wa familia ya wakina ABRI ambao ni familia moja na wenye ASAS MILK. Kuna ndugu yao moja hivi alikuwa inabidi apewe sehemu kubwa ya urithi lakini akakosea akaenda kuoa binti wa familia nyingine ya kiarabu: Mama yake aling'aka sana akimwambia mama yangu kwamba yule mtoto hatarithi sehemu kubwa kwasababu anaona mwanamke ambaye siyo ndugu yao. Hii ilikuwa miaka zaidi ya thelathini nyuma na nilivyosimuliwa nikaona nifanya uchunguzi haraka.

Nikagundua wale watoto waarabu mbali na kuzaliwa kwenye familia za kitajiri, sehemu kubwa ya maisha yao ni kufanya biashara za familia. Watu kama Mohamed na Fatma Dewji, ASAS, Freeman Mbowe & The Mengi's wachunguze vizuri maisha yao na utatambua kwamba hawakuanzisha vyao bali waliendeleza walivyovikuta baada ya kufundishwa vizuri na wazazi wao. Sasa sisi weusi mzazi hata viwanja anaficha, mapato yake anaficha na anakuwa na familia mitala ya wake nane hadi tisa: Sehemu kubwa ya malezi anaachiwa mwanamke, hapo utategemea kizazi kifike mbali ? Halafu akifa anakuachia urithi anategemea uundeleze! Uendeleze kwenda wapi ????

Biblia Takatifu inasema hivi: "Fedha na Mali mtu hurithi kutoka kwa baba yake"
Sasa wewe Mkurya mtoto akifika miaka 18 unafukuza nyumbani unasema akatafute zake nishakusomesha.
Tutalalamika sana kuwachukia Wahindi, Waarabu na Wachagga lakini ukweli wenyewe ndiyo huu, wametushinda.
Mkuu umemaliza kila kitu , mama angu alikuwa anapenda kulima mpunga tukitoka shule anatupeleka shamba mzee mpak unachukia , shamba likichanganya Sana anawapiga stop hata kwenda skul sku mbili mnaenda shamba .,... Nikamaliza chuo ajira ikazingua mzee , nikaona fursa ya kulima , nilikichafua mpak kijiji kizima wakahs natumia ndumba , nilikuwa kwenye top five ya watu walioscore mpunga mwingi huku Mimi peke yangu ndo kijana ......
Uzoefu ambao mama alinipatia siwez kuusahahu kamwe na hapo ndo nilipata mtaji wa kufanyia harakat zingine town ....

Sisi waafrica akli za kurithishana hatuna yaan Baba hatak mwanae ajue kiundani what is going on kuhus maswala ya uchumi wa familia , akifa na uchumi unakufa , kongole Kwa wachaga na watu wa Asia
 
Waahidi, wapakistani na WaBangladesh wanatuzidi nini kwenye biashara?

Ni nini ambacho sisi weusi tunakosea. Wengi wao wakifungua tu biashara unaiona hiyo inanyanyuka mdogomdogo.

Na sio kama wanaanza biashara kubwa.

Nimekuwa najiuliza saana ni wapi sisi tunapokosea....kuna mmoja nilisoma naye akafaulu lakini akasema siendi chuo...akaanza kununua n'gombe nami nikaanza ila leo hii jamaa humgusi.

Hata huko Canada na Ulaya...hawa jamaa wanaanza biashara kiutani utani tu baada ya miaka kadhaa wanaanza kuajiri wabeba box.

Kuna mwenye kujua hawa jamaa wanatuzidia wapi kwenye biashara??

Ipo kwenye damu?

Wana loga?

Wananidhamu na wanachokifanya?

Wanatumiwa mitaji kutoka kwao?
Nidhamu katika Biashara
Wanapanga Bajeti ya familia ndani ya siku
Wapate faida kubwa katika biashara yao,Bajeti ya nyumbani haivuki,kisa eti wamepata faida mara dufu

Hawamuamini mtu katika pesa,wanapenda kuhakiki kila kitu katika baishara

Wana mengi sana ya kujifunza kwao
 
Mkuu najua sio wote wana njia za panya nimegusia hilo Kama njia moja wapo.. ukijaribu kufikiri vizuri hapo unaweza kuona kuna ka mnyororo fulani..😅
Bwana bwana! Kiufupi hakuna mfanya biashara ambaye hatumii njia za panya hapa duniani,
Iwe kupitia Tax Avoidance, Tax Evasion, Bribery, Extortion, Black-Mail and Murder.

Hebu soma alichokiandika mkuu Slowly hapa chini: Hakuna miujiza.
Mkuu umemaliza kila kitu , mama angu alikuwa anapenda kulima mpunga tukitoka shule anatupeleka shamba mzee mpak unachukia , shamba likichanganya Sana anawapiga stop hata kwenda skul sku mbili mnaenda shamba .,... Nikamaliza chuo ajira ikazingua mzee , nikaona fursa ya kulima , nilikichafua mpak kijiji kizima wakahs natumia ndumba , nilikuwa kwenye top five ya watu walioscore mpunga mwingi huku Mimi peke yangu ndo kijana ......
Uzoefu ambao mama alinipatia siwez kuusahahu kamwe na hapo ndo nilipata mtaji wa kufanyia harakat zingine town ....

Sisi waafrica akli za kurithishana hatuna yaan Baba hatak mwanae ajue kiundani what is going on kuhus maswala ya uchumi wa familia , akifa na uchumi unakufa , kongole Kwa wachaga na watu wa Asia
Naam! Mama yako alifanikiwa kuweka uwiano baina ya (Formal Education & Informal Education). Sasa wewe nawe ukijakuwa mkulima mkubwa, komaa na watoto wako walime. Tumia hata mbata na viboko walime, tena fanya mechanization (Use of Tractors and Machinery) kabisa. Ikiwezekana somesha hata mtoto moja mambo ya kilimo ili hata ukimuachia kitu basi una uhakiaka kitadumu.

Daby njoo umsome bwana Slowly: Ukiona vyaelea ujue vimeundwa.
 
Siri kubwa ni ushirikiano. Ukiona jamii nzima inainuka jua imeungana. Wahindi kila siku wanaitana na kupeana michongo Canada. Wamekuwawengi balaa. Sisi wabantu hatuna hii kitu ya kushirikiana.

Niliona familia moja ya kiarabu walianzisha mgahawa. Unapewa mwaka mmoja uendeshe na kupata mtaji kisha anakuja mwingine. Wote wanatokea hapo kwenye mgahawa.

Ushirikiano ndiyo nguzo na ndiyo maana yule jamaa aliandika Capitalist nigger, kasisitiza sana ushirikiano mule. Nimeona wakinga wanajitahidi sana kushirikiana na ndiyo maana jamii nzima inainuka. Wameanzisha SACCOS zimekuwa kubwa kama benki.

Wayahudi ndiyo usiseme kabisa kwa kushirikiana. Kitabu cha methali kinawaambia kuwa "usimkopeshe ndugu yako kwa riba". Wakiamua wanashika biashara nzimanzima. Biashara yote ya almasi duniani ipo mikononi mwao. Hilo haliwezekani bila kushirikiana.

Kitu kingine ni utamaduni, wabantu ni wakulima, wengine hawa ni wafugaji na wengine ni wafanyabiashara, kuna mafundi nk. Katika wote hawa mfanyabiashara ndiye huwa tajiri kuliko wote na mkulima ni wa mwisho. Kwahiyo kiasili wabantu siyo wafanyabiashara, hufanya biashara eneo lake lisipofaa kilimo au ikiwa ngumu kufanya kilimo. labda iwekwe kwenye silabasi shuleni, tufundishane namna ya kufanya biashara.
 
Wayahudi ndo wanaongoza Kwa kugeuza biashara kuwa taasisi kubwa..

Partnership..ndo siri ilipo..

Sisi hatujaweza Sana hii partnership..
Patnership za kibongo huwa hazidumu, mnaanza struggle hela ikianza ingia tu anaestahili kupata 40% anaona anaepata 50% anafaidi sana wakati walikubaliana hayo toka awali...Hapo tu yani kuheshimu mikataba ni ngumu.

Mtu anaona bora aanzishe nayeye ofisi yake ili apate 100% zote asijue kuwa kufanikiwa kunaweza changiwa na network ya mwenzake mwishowe anafeli mazima.
 
Ukitaka kuamini hili....waambie hata ndugu zako. Kaka zako...

Waaambie tufungueni biashara....watakuambia unataka watoto wako wakikua wachukue kila kitu tubaki hatuna kitu.

Ila tunazaa saana pia....mtu ana watoto 9 wote atawarithisha nini!
 
Acha tu yani mie patnership za kibongo siziaminigi kabisa sababu hatuwezi.

Sasa hao ndugu unawaanzishia biashara hawakawilii kufilisi biashara zenyewe wakati wenzetu wanainuana kupitia biashara za familia hizo hizo.
 
Waahidi, wapakistani na WaBangladesh wanatuzidi nini kwenye biashara?

Ni nini ambacho sisi weusi tunakosea. Wengi wao wakifungua tu biashara unaiona hiyo inanyanyuka mdogomdogo.

Na sio kama wanaanza biashara kubwa.

Nimekuwa najiuliza saana ni wapi sisi tunapokosea....kuna mmoja nilisoma naye akafaulu lakini akasema siendi chuo...akaanza kununua n'gombe nami nikaanza ila leo hii jamaa humgusi.

Hata huko Canada na Ulaya...hawa jamaa wanaanza biashara kiutani utani tu baada ya miaka kadhaa wanaanza kuajiri wabeba box.

Kuna mwenye kujua hawa jamaa wanatuzidia wapi kwenye biashara??

Ipo kwenye damu?

Wana loga?

Wananidhamu na wanachokifanya?

Wanatumiwa mitaji kutoka kwao?
Nyota + uchawi.
Muhindi na mwarabu hafanyi business bila uchawi.
 
Siri kubwa ni ushirikiano. Ukiona jamii nzima inainuka jua imeungana. Wahindi kila siku wanaitana na kupeana michongo Canada. Wamekuwawengi balaa. Sisi wabantu hatuna hii kitu ya kushirikiana.
Niliona familia moja ya kiarabu walianzisha mgahawa. Unapewa mwaka mmoja uendeshe na kupata mtaji kisha anakuja mwingine. Wote wanatokea hapo kwenye mgahawa.
Ushirikiano ndiyo nguzo na ndiyo maana yule jamaa aliandika Capitalist nigger, kasisitiza sana ushirikiano mule. Nimeona wakinga wanajitahidi sana kushirikiana na ndiyo maana jamii nzima inainuka. Wameanzisha SACCOS zimekuwa kubwa kama benki.
Wayahudi ndiyo usiseme kabisa kwa kushirikiana. Kitabu cha methali kinawaambia kuwa "usimkopeshe ndugu yako kwa riba". Wakiamua wanashika biashara nzimanzima. Biashara yote ya almasi duniani ipo mikononi mwao. Hilo haliwezekani bila kushirikiana.

Kitu kingine ni utamaduni, wabantu ni wakulima, wengine hawa ni wafugaji na wengine ni wafanyabiashara, kuna mafundi nk. Katika wote hawa mfanyabiashara ndiye huwa tajiri kuliko wote na mkulima ni wa mwisho. Kwahiyo kiasili wabantu siyo wafanyabiashara, hufanya biashara eneo lake lisipofaa kilimo au ikiwa ngumu kufanya kilimo. labda iwekwe kwenye silabasi shuleni, tufundishane namna ya kufanya biashara.
Wakinga inaonekana wapo serious sana na kuinuana kiuchumi. Good spirit indeed.
 
Hata zikichukuliwa hela zote kisha tukagawiwa sote sawa kwa sawa basi waliokua matajiri watarudi kua matajiri na Masikini watarudi kua masikini,
Nidhamu,Mipango,kujituma na kuifanya kazi kwa waledi ni muhimu sana kisha kutomsahau Mungu hata pale unapokua umesha fanikiwa.
 
Hivyo kwa wingi sisi hatuna nidhamu, mipango, hatujitumi na tunamsahau Mungu??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom