Hawa wenzetu Wa-Asia wanatuzidi nini?

Hawa wenzetu Wa-Asia wanatuzidi nini?

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
34,954
Reaction score
80,256
Waahidi, wapakistani na WaBangladesh wanatuzidi nini kwenye biashara?

Ni nini ambacho sisi weusi tunakosea. Wengi wao wakifungua tu biashara unaiona hiyo inanyanyuka mdogomdogo.

Na sio kama wanaanza biashara kubwa.

Nimekuwa najiuliza saana ni wapi sisi tunapokosea....kuna mmoja nilisoma naye akafaulu lakini akasema siendi chuo...akaanza kununua n'gombe nami nikaanza ila leo hii jamaa humgusi.

Hata huko Canada na Ulaya...hawa jamaa wanaanza biashara kiutani utani tu baada ya miaka kadhaa wanaanza kuajiri wabeba box.

Kuna mwenye kujua hawa jamaa wanatuzidia wapi kwenye biashara??

Ipo kwenye damu?

Wana loga?

Wananidhamu na wanachokifanya?

Wanatumiwa mitaji kutoka kwao?
 
Biashara kwa muhindi na mwarabu ni sehemu ya utamaduni. Wenzetu kufanya biashara kumekuwa ni sehemu ya maisha na siyo tu shughuli ya kujiingizia kipato cha kila siku. Leo mtoto wa kihindi hata kama atakuwa yuko shule mnasoma naye, lakini ni lazima atakuwa anapata muda wa kutosha kushinda kwenye duka au ghala la wazazi wake huku akifanya kazi ndogo-ndogo.

Mwisho wa siku huyu mtu anakuwa anapata elimu za aina mbili (Formal and Informal Education), akija kuwa mkubwa atakachokuwa anafanya sehemu kubwa ni marudio ya alichojifunza kutoka kwa wazazi wake. Hili nimelishuhudia sana hata kwa Wachagga wengi. Lakini kubwa zaidi ambalo huwa linakuwepo kwa wenzetu ni utayari wa wanafamilia kutoa mitaji kwa watoto ambao wanaonekana kuweza kufanya biashara.

Lakini sasa wewe ndugu Daby unaweza ukawa ni Massai, lakini sehemu kubwa ya maisha yako umejikita kwenye kusoma (Formal Education) ambayo matokeo yake yanaweza kuja baada ya miaka 14 ya kumaliza shule. Baadae umekosa ajira ndiyo unakumbuka kama wewe ni Massai hivyo unaamua kununua ng'ombe ukitegemea utaweza kufuga, ilhali huna ujuzi wowote wa kufuga (Ulimwacha mzazi wako akafa nao).

Lakini ungekuwa ni massai wa mjini na kijijini naamini kuna vitu vikubwa kuhusu ufugaji ungekuwa unavifahamu kuliko hata mtu wa PhD aliyetoka Sokoine University of Agriculture: AND WHY, it's a generational thing for Massai to be excellent in Pastoralism and Ranching. Hivyo hakuna miujiza, waswahili husema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Kujifunza kwa muda mrefu tena kwa vitendo huku wakisimamiwa na familia: Hii huzaa kijiamini na nidhamu kwasababu huwezi kutumia vibaya fedha ya familia.

KITU KIKUBWA: Utajiri wa kundi la watu (Kabila au dini) mara nyingi huwa ni vizazi (A Genereational thing). Katika matajiri wakubwa hapa Tanzania hasa waashia, utajiri wao unakuwa na mizizi mirefu ya urithi. Watoto hurithishwa kutoka wazazi. Pia huo urithi hauji moja kwa moja, lakini inabidi mtoto autolee jasho na kuupambania kuupata tokea akiwa mtoto ili usije ukapotea. Familia pia huwa tayari kutoa mitaji na ajira kwa wanandugu ambao wanataka kufanya biashara au kujiendeleza.

Marehemu mama yangu aliwahi kuwa rafiki mkubwa sana wa familia ya wakina ABRI ambao ni familia moja na wenye ASAS MILK. Kuna ndugu yao moja hivi alikuwa inabidi apewe sehemu kubwa ya urithi lakini akakosea akaenda kuoa binti wa familia nyingine ya kiarabu: Mama yake aling'aka sana akimwambia mama yangu kwamba yule mtoto hatarithi sehemu kubwa kwasababu anaona mwanamke ambaye siyo ndugu yao. Hii ilikuwa miaka zaidi ya thelathini nyuma na nilivyosimuliwa nikaona nifanya uchunguzi haraka.

Nikagundua wale watoto waarabu mbali na kuzaliwa kwenye familia za kitajiri, sehemu kubwa ya maisha yao ni kufanya biashara za familia. Watu kama Mohamed na Fatma Dewji, ASAS, Freeman Mbowe & The Mengi's wachunguze vizuri maisha yao na utatambua kwamba hawakuanzisha vyao bali waliendeleza walivyovikuta baada ya kufundishwa vizuri na wazazi wao. Sasa sisi weusi mzazi hata viwanja anaficha, mapato yake anaficha na anakuwa na familia mitala ya wake nane hadi tisa: Sehemu kubwa ya malezi anaachiwa mwanamke, hapo utategemea kizazi kifike mbali ? Halafu akifa anakuachia urithi anategemea uundeleze! Uendeleze kwenda wapi ????

Biblia Takatifu inasema hivi: "Fedha na Mali mtu hurithi kutoka kwa baba yake"
Sasa wewe Mkurya mtoto akifika miaka 18 unafukuza nyumbani unasema akatafute zake nishakusomesha.
Tutalalamika sana kuwachukia Wahindi, Waarabu na Wachagga lakini ukweli wenyewe ndiyo huu, wametushinda.
 
Waahidi, WaPakstani na WaBangladesh wanatuzidi nini kwenye biashara?

Ni nini ambacho sisi weusi tunakosea. Wengi wao wakifungua tu biashara unaiona hiyo inanyanyuka mdogomdogo.

Na sio kama wanaanza biashara kubwa.

Nimekuwa najiuliza saana ni wapi sisi tunapokosea....kuna mmoja nilisoma naye akafaulu lakini akasema siendi chuo...akaanza kununua n'gombe nami nikaanza ila leo hii jamaa humgusi.

Hata huko Canada na Ulaya...hawa jamaa wanaanza biashara kiutani utani tu baada ya miaka kadhaa wanaanza kuajiri wabeba box.

Kuna mwenye kujua hawa jamaa wanatuzidia wapi kwenye biashara??

Ipo kwenye damu?

Wana loga?

Wananidhamu na wanachokifanya?

Wanatumiwa mitaji kutoka kwao?
Mkuu daby unaposema huyo jamaa humgusi maana yake ana maendeleo na amepiga hatua kubwa kwenye biashara?
 
Kwanza Wana discipline na pesa
Umewahi waona bar wakitoa offa?..

Pili ni watu wanaojali Imani za makafara
Na kinga za kichawi..
Maduka yote ya wahindi nenda asubuhi kabla
Hawajafungua..wanachoma ubani openly
Wala hawaoni aibu wala kujifungua
Utakuta vibarua wa Swahili ndo wanatumwa
Leta moto ..na kadhalika..

Tatu wanasaidiana..wanakopeshana bila riba kubwa ..na kupeana biashara Kwa Mali kauli..

Nne wakikopeshwa wanalipa mikopo bila usumbufu..

Tano..hawapotezi mda kulalamikia serikali..
Wanacheza nayo Tu hadi kieleweke..

Sio Tu wahindi..tazama wayahudi huko Europe na waarabu na wasomali...same thing
 
Biashara kwa muhindi na mwarabu ni sehemu ya utamaduni. Wenzetu kufanya biashara kumekuwa ni sehemu ya maisha na siyo tu shughuli ya kujiingizia kipato cha kila siku.
Haujawahi kujiuliza hili swali Malcom!!

Unaanza nao biashara tena kwa kimtaji kiduchu ila wanakuacha unaangalia.

Mifano ninayo mingi.(nisitaje majina)...Kuna huyu mwamba ametoka Pakstan 2010. Akaanza kuuza CD tu leo anamiliki maduka ya spare parts jijini.
 
Nidhamu ya pesa, Mhindi akianza biashara budget yake ya chakula kama ni wali biringanya hata akiwa na milioni tano ataendelea kula wali biringanya.

Mswahili akipata milion tatu, mtaa mzima utajua kwanza jioni mke wake ataacha kupika, muuza chips atapewa order ya chips maini chips kuku tena na bodaboda wa kupeleka nyumbani.
 
Umefanya nijiulize Kama walianzaga kutuuza sisi tu wakati wa biashara ya utumwa watashindwaje kutoboa..?!

Wana experience ya kutosha tulishawahi kuwa bidhaa kwao Sasa ulishaona wapi bidhaa inamzidi muuzaji..😂
 
Saana mkuu hatua kubwa saana.

Kinachonishangaza ni akili yao ya kuigeuza biashara ndogo na kuwa taasisi kubwa.

Tunafeli wapi sisi?
Ukweli they are very creative and tolerants,ila sis wabongo tunadharau biashara ndogondogo et mpaka tukakope mitaji mikubwa bank mwisho wake tunajilimbikizia madeni na biashara inakufa,pili thamani ya pesa zao ni tofauti za zetu huwa wakiwa na kiasi kidogo cha pesa huku kibakuwa kikubwa,je ng'ombe alionunua ni wa nyama au maziwa?.mwisho wanasapotiana
 
Umefanya nijiulize Kama walianzaga kutuuza sisi tu wakati wa biashara ya utumwa watashindwaje kutoboa..?!
Wana experience ya kutosha tulishawahi kuwa bidhaa kwao Sasa ulishaona wapi bidhaa inamzidi muuzaji..[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mkuu unanichekesha jibu tunalo hapo
 
Kwanza Wana discipline na pesa
Umewahi waona bar wakitoa offa?..

Pili ni watu wanaojali Imani za makafara
Na kinga za kichawi..
Maduka yote ya wahindi nenda asubuhi kabla
Hawajafungua..wanachoma ubani openly
Wala hawaoni aibu wala kujifungua
Utakuta vibarua wa Swahili ndo wanatumwa
Leta moto ..na kadhalika..

Tatu wanasaidiana..wanakopeshana bila riba kubwa ..na kupeana biashara Kwa Mali kauli..

Nne wakikopeshwa wanalipa mikopo bila usumbufu..

Tano..hawapotezi mda kulalamikia serikali..
Wanacheza nayo Tu hadi kieleweke..

Sio Tu wahindi..tazama wayahudi huko Europe na waarabu na wasomali...same thing
Umenena ukweli...na wana ishirikiano mkubwa saana. Na hawa waEthiopia na Wasomali wanainuka saana miaka ya karibuni.

Ukiacha Kaburu Jozi kwasasa inamilikiwa na Msomali na MuEthiopia....wenzao wanawatumia pesa kutoka Marekani na Ulaya Retailers wakubwa ni wao.

Unajua kuanzisha biashara ni jambo dogo saana ambalo kila mmoja anaweza kulifanya??

Shida ni kuikuza na kuifanya taasisi kubwa...hapa ndipo weusi tuna shida napo...
 
Umefanya nijiulize Kama walianzaga kutuuza sisi tu wakati wa biashara ya utumwa watashindwaje kutoboa..?!
Wana experience ya kutosha tulishawahi kuwa bidhaa kwao Sasa ulishaona wapi bidhaa inamzidi muuzaji..[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenena ukweli...na wana ishirikiano mkubwa saana. Na hawa waEthiopia na Wasomali wanainuka saana miaka ya karibuni.

Ukiacha Kaburu Jozi kwasasa inamilikiwa na Msomali na MuEthiopia....wenzao wanawatumia pesa kutoka Marekani na Ulaya Retailers wakubwa ni wao.

Unajua kuanzisha biashara ni jambo dogo saana ambalo kila mmoja anaweza kulifanya??

Shida ni kuikuza na kuifanya taasisi kubwa...hapa ndipo weusi tuna shida napo...

Wayahudi ndo wanaongoza Kwa kugeuza biashara kuwa taasisi kubwa..

Partnership..ndo siri ilipo..

Sisi hatujaweza Sana hii partnership..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mkuu unanichekesha jibu tunalo hapo
Hawa jamaa hawataki masihara kabisa..😂
Ila mkuu muda mwengine hutumia njia za panya hawa na sio wao tu hata baadhi ya wabongo nililifahamu hilo rais alipoita wafanyabiashara ikulu kuzungumza nao na hawa wa makodikodi Hawa ni sehemu moja wapo ya kufanya watu watumie njia za panya..
 
Nidhamu ya pesa, Mhindi akianza biashara budget yake ya chakula kama ni wali biringanya hata akiwa na milioni tano ataendelea kula wali biringanya.

Mswahili akipata mikioni tatu, mtaa mzima utajua kwanza jioni mke wake ataacha kupika kuuza chips atapewa order ya chips maini chips kuku tena na bodaboda wa kupeleka nyumbani.
Kuzishinda tamaa za mwili ni tatizo hata mimi ninalo.

Nilishaajiriwa na boss mhindi...nilijifunza mengi kwake...alitokea kunipenda saana akienda manunuzi ataniita.

Atasimama akodolee screen kuona bei ya kila bidhaa na kama hajaelewa sehemu atauliza ni shilingi ngapi hata kama ni lighter.

Weusi waliopo kwenye mstari watalalamika anawachelewesha...lakini mimi nikiwa kwenye manunuzi binafsi...nachukua hiki naweka kwa kikapu ...fika kwa malipo narushia kwa kikapu hata siangalii kama bidhaa zote zimetimia. Nikifika nyumbani siku zingine unakuta kuna vitu ulilipia lakini hauvioni.

Lakini mimi ndiye maskini nilitakiwa niwe mwangalizi saana kumzidi bilionaire.
 
Hawa jamaa ni wamoja sana kwenye biashara na wanasaidiana sana ndio maana biashara zao nyingi zinasimamiwa na kuendeshwa na wanafamilia karibia wote.

Sisi wabongo biashara ikiwa ya familia basi kuna asilimia kubwa ya mifarakano na kuigawanya biashara baada ya wakubwa kutangulia mbele za haki, hii inaturudisha sana nyuma.

Wahindi na hao wengine tajwa wakianza biashara wote wanaanzia kwa kukaa nyumbani hadi wafanikiwe kujenga au kufikia level flani na hii huwasaidia kuepukana au kupunguza gharama nyingine kama kodi ya nyumba+matumizi mengine ambayo akiishi nyumbani anayapata for free while saving more and invest more.

Kwetu sisi kijana akianzisha biashara hata kama ni karibu na nyumbani awezi kukaa anataka uhuru(ni jambo jema) anahama anaenda kupangisha mwisho wa siku gharama za maisha zinaongezeka na kuathiri maendeleo yake kibiashara.
 
Ukweli they are very creative and tolerants,ila sis wabongo tunadharau biashara ndogondogo et mpaka tukakope mitaji mikubwa bank mwisho wake tunajilimbikizia madeni na biashara inakufa,pili thamani ya pesa zao ni tofauti za zetu huwa wakiwa na kiasi kidogo cha pesa huku kibakuwa kikubwa,je ng'ombe alionunua ni wa nyama au maziwa?.mwisho wanasapotiana
Nyama....ila amekuwa na matawi ya biashara na chanzo ni hicho tu mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom