Hawa wenzetu Wa-Asia wanatuzidi nini?

Kwa kweli hawa jamaa ni wa kupigwa mfano wahindi,waarabu,wasomali,wahabesh,wayahudi kongole kwa kweli wanadisclipne sana kwenye kazi.....kuna mahali nilikuwa naishi nao ,yan inàtia raha sana familia inakaa sebuleni inapanga bajeti kila baada ya miezi sita, bajeti ya chakula na mambo mengine ya familia yan hadi vitoto vidogo vya miaka kumi na mbili pia vinashiriki na kuangalia kinachoendelea,wanathamini hata shilingi mia moja na kuhakikisha kila pesa haitumiki ndivyo sivyo ,inatumika kama ilivyopangwa.......

Biashara sasa ndo balaa,kama mahali pa biashara ni karibu na home yan panafikika kwa gari kwa dk kadhaa tu basi habari ya kununua msosi haipo yy anakula home hukooo ....watoto wakitoka shule wana sehemu mbili za kwenda kucheza mahali pa biashara yao ilipo au kutuli a nyumbani kusomasoma na kusaidia kazi au kwa wale waislamu naona wanaenda kusoma dini.mfano wayahudi wao watt wadogo kabisa hata kama ni familia ya kawaida wana tabia moja nzuri sana wanawafundisha watt wao kuwa kuna pesa ya kusave,kuspend na kutoa sadaka na pia pesa ya kuinvest so MTT anakua ktk mazngira hayo hadi utu uzima...........

Nilipenda sana hayo maisha ya namna ambayo kwetu ni tofauti kabisa yan ni matatizo kabisa baba anamiliki ardhi,nyumba kadhaa lakin family wala haijui chochote kisa utasikia mke wangu Huyu namuona ka mshirikina flani iv,na ndiyo maana haya makundi tajwa hapo juu huwa wanaoana wenyewe tu
 
Biashara ni fani....ina utaratibu na vigezo maalumu...ukivijua na kuvifuata....hakuna biashara itakushinda duniani.... wahindi na baadhi ya jamii zilizofanikiwa kibiashara wanalijua hilo na ndio msingi wao mkuu wa mafanikio.... hakuna biashara ambayo hailipi duniani... ki uumbaji dunia na viumbe vyake vyote.... ili viendelee kuwepo vinaitaji matumizi ya bidhaa mbali mbali...zikikosekana dunia yote itaangamia...vitu hivi vimegawanyika katika hali ya kwingine vipo na kwingine havipo.....hapo ndio dhana ya biashara inapokuja..,. ndoto... wahindi wenzetu wako vizuri kwenye hili....mtu yuko shule ya msingi tayari ana ndoto ya kuja kuwa mfanyabiashara

Mkubwa....Elimu...baada ya kuwa na ndoto wanawekeza kwenye elimu hasa elimu ya biashara....hata ukiwafatilia wameiva Sana kwenye dhana ya kutambua asset na liabilities...biashara inahitaji uzijue hizi vizuri....ndio maana huwezi kuta mhindi anatumia pesa zake hovyo...hata nyumba wanakaa za msajili au appartment karibu na biashara yake....hapo anaokoa nauli...muda....na pesa ya kula hotel...hata wakienda beach huwa wanaenda na chakula chao...tofauti na jamii yetu....biashara ikianza kukua tu...anajisahau na kuanza kununua vitu ambavyo sio asset...badala ya kukuza biashara...utafiti....

Kabla hawajaanza biashara wanafanya utafiti kujua kama bidhaa hiyo itahitajika sokoni...mfano ni kama barafu ya ukwaju ya Azam.....mtaji...wanatafuta mtaji unaolingana na aina ya biashara anayotaka kufanya....sio unanza kufanya biashara kubwa kwa mtaji mdogo....mbeleni utashindwa tu.... uaminifu...hata Kama biashara sio yake ni waamifu Sana...sio wizi Kama jamii yetu....nidhamu...wana nidhamu ya pesa na muda... mhindi akipanga duka litafunguliwa saa tatu ni saa tatu....vitu vingine Kama ushirikiano.....bidii... customer care....mipango ya kukuza biashara...wako vizuri sana hawa jamaa.... lakini la mwisho kale kautamaduni kao ka- kuoana ndugu kamewasaidia sana kufanya utajiri wao uweze kudumu vizazi na vizazi.
 
Wabongo tuna matatizo mengi sana.

1. Kuchukiana sisi kwa sisi yaani haoa hadi ndugu wa tumbo moja kabisa hii kwa wenzetu sio rahisu uikute

2. Tamaa, nazani tuna tamaa mno ya kutaka kuonekana, show off, hizi zinatufanya tupoteze sana focus

3. Hatukupitia kwenye shida sana, ujue watu kama Somalia kule wakiangalia nchi zao wabapata nguvu sana ya kupambana, India kule lazima upambane kufa na kupona, hakuna Free Lunch kule, Bongo mtu anaweza rudi kwa wazazi wake na akawa anakula na kulala, Bongo kuna hadi mashamba ya bure, maji ya bure, hivi vinafanya tuwe wajinga ziadi na legelege,

4. Tumerithi mfumo mbaya sana wa Ujamaa, Ujamaa unafanya watu wawe legelege sana, make wanajua Serikali itafanya, wewe fikiria Mmasai ana Ng'ombe 3000 ila unakuta analamamika Serikali haijengi Josho, Wasukuma wana ng'ombe ila bado wanalalamikia Serikali,

Hii mifumo ya kutegemea Serikali ni mibaya sana

5.
 
Biashara kwa muhindi na mwarabu ni sehemu ya utamaduni. Wenzetu kufanya biashara kumekuwa ni sehemu ya maisha na siyo tu shughuli ya kujiingizia kipato cha kila siku. Leo mtoto wa kihindi hata kama atakuwa yuko shule mnasoma naye, lakini ni lazima atakuwa anapata muda wa kutosha kushinda kwenye duka au ghala la wazazi wake huku akifanya kazi ndogo-ndogo.

Mwisho wa siku huyu mtu anakuwa anapata elimu za aina mbili (Formal and Informal Education), akija kuwa mkubwa atakachokuwa anafanya sehemu kubwa ni marudio ya alichojifunza kutoka kwa wazazi wake. Hili nimelishuhudia sana hata kwa Wachagga wengi. Lakini kubwa zaidi ambalo huwa linakuwepo kwa wenzetu ni utayari wa wanafamilia kutoa mitaji kwa watoto ambao wanaonekana kuweza kufanya biashara.

Lakini sasa wewe ndugu Daby unaweza ukawa ni Massai, lakini sehemu kubwa ya maisha yako umejikita kwenye kusoma (Formal Education) ambayo matokeo yake yanaweza kuja baada ya miaka 14 ya kumaliza shule. Baadae umekosa ajira ndiyo unakumbuka kama wewe ni Massai hivyo unaamua kununua ng'ombe ukitegemea utaweza kufuga, ilhali huna ujuzi wowote wa kufuga (Ulimwacha mzazi wako akafa nao).

Lakini ungekuwa ni massai wa mjini na kijijini naamini kuna vitu vikubwa kuhusu ufugaji ungekuwa unavifahamu kuliko hata mtu wa PhD aliyetoka Sokoine University of Agriculture: AND WHY, it's a generational thing for Massai to be excellent in Pastoralism and Ranching. Hivyo hakuna miujiza, waswahili husema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Kujifunza kwa muda mrefu tena kwa vitendo huku wakisimamiwa na familia: Hii huzaa kijiamini na nidhamu kwasababu huwezi kutumia vibaya fedha ya familia.

KITU KIKUBWA: Utajiri wa kundi la watu (Kabila au dini) mara nyingi huwa ni vizazi (A Genereational thing). Katika matajiri wakubwa hapa Tanzania hasa waashia, utajiri wao unakuwa na mizizi mirefu ya urithi. Watoto hurithishwa kutoka wazazi. Pia huo urithi hauji moja kwa moja, lakini inabidi mtoto autolee jasho na kuupambania kuupata tokea akiwa mtoto ili usije ukapotea. Familia pia huwa tayari kutoa mitaji na ajira kwa wanandugu ambao wanataka kufanya biashara au kujiendeleza.

Marehemu mama yangu aliwahi kuwa rafiki mkubwa sana wa familia ya wakina ABRI ambao ni familia moja na wenye ASAS MILK. Kuna ndugu yao moja hivi alikuwa inabidi apewe sehemu kubwa ya urithi lakini akakosea akaenda kuoa binti wa familia nyingine ya kiarabu: Mama yake aling'aka sana akimwambia mama yangu kwamba yule mtoto hatarithi sehemu kubwa kwasababu anaona mwanamke ambaye siyo ndugu yao. Hii ilikuwa miaka zaidi ya thelathini nyuma na nilivyosimuliwa nikaona nifanya uchunguzi haraka.

Nikagundua wale watoto waarabu mbali na kuzaliwa kwenye familia za kitajiri, sehemu kubwa ya maisha yao ni kufanya biashara za familia. Watu kama Mohamed na Fatma Dewji, ASAS, Freeman Mbowe & The Mengi's wachunguze vizuri maisha yao na utatambua kwamba hawakuanzisha vyao bali waliendeleza walivyovikuta baada ya kufundishwa vizuri na wazazi wao. Sasa sisi weusi mzazi hata viwanja anaficha, mapato yake anaficha na anakuwa na familia mitala ya wake nane hadi tisa: Sehemu kubwa ya malezi anaachiwa mwanamke, hapo utategemea kizazi kifike mbali ? Halafu akifa anakuachia urithi anategemea uundeleze! Uendeleze kwenda wapi ????

Biblia Takatifu inasema hivi: "Fedha na Mali mtu hurithi kutoka kwa baba yake"
Sasa wewe Mkurya mtoto akifika miaka 18 unafukuza nyumbani unasema akatafute zake nishakusomesha.
Tutalalamika sana kuwachukia Wahindi, Waarabu na Wachagga lakini ukweli wenyewe ndiyo huu, wametushinda.
u nail it.full stop.tizama mtoto anayekulia kwenye businesses ya familia.mfano wakulima wafugaj.huyu atakuja pata shida kujua kazi gan afanye?
 
Kwanza Wana discipline na pesa
Umewahi waona bar wakitoa offa?..

Pili ni watu wanaojali Imani za makafara
Na kinga za kichawi..
Maduka yote ya wahindi nenda asubuhi kabla
Hawajafungua..wanachoma ubani openly
Wala hawaoni aibu wala kujifungua
Utakuta vibarua wa Swahili ndo wanatumwa
Leta moto ..na kadhalika..

Tatu wanasaidiana..wanakopeshana bila riba kubwa ..na kupeana biashara Kwa Mali kauli..

Nne wakikopeshwa wanalipa mikopo bila usumbufu..

Tano..hawapotezi mda kulalamikia serikali..
Wanacheza nayo Tu hadi kieleweke..

Sio Tu wahindi..tazama wayahudi huko Europe na waarabu na wasomali...same thing
Aisee kweli.nimeingia dukan pale jizingitin kuna mshumaa ule upo kwenye sahan mnauruka
 
Waahidi, wapakistani na WaBangladesh wanatuzidi nini kwenye biashara?

Ni nini ambacho sisi weusi tunakosea. Wengi wao wakifungua tu biashara unaiona hiyo inanyanyuka mdogomdogo.

Na sio kama wanaanza biashara kubwa.

Nimekuwa najiuliza saana ni wapi sisi tunapokosea....kuna mmoja nilisoma naye akafaulu lakini akasema siendi chuo...akaanza kununua n'gombe nami nikaanza ila leo hii jamaa humgusi.

Hata huko Canada na Ulaya...hawa jamaa wanaanza biashara kiutani utani tu baada ya miaka kadhaa wanaanza kuajiri wabeba box.

Kuna mwenye kujua hawa jamaa wanatuzidia wapi kwenye biashara??

Ipo kwenye damu?

Wana loga?

Wananidhamu na wanachokifanya?

Wanatumiwa mitaji kutoka kwao?

Jibu ni Dogo tu,

Uelewa mdogo juu ya Biashara.

Sisi hatupendi kujifunza, hatupendi kusoma

Tujiulize tu, ni wangapi kati yetu huwa tunajisomea vitabu vya jinsi ya Kuanzisha, kumsimamia na kukuza biashara?

Unaweza kuniambia mbona hata waAsia hawasomi vitabu

Ni kweli, ila...

.. Wao hupata Uzoefu kutoka kwa wazazi wao ambao wanajua na wameshapitia katika hayo wanayofundisha

Sisi wa shauri wetu ni nani?

Mjomba, baba, shangazi n.k

Ambao nao wote ni masikini! Tutajifunza nini kutoka kwao?

Biashara inamisingi yake, leadership and management, finance & accounting, marketing & sales n.k

Je, sisi tuna tumia muda wetu mwingi kujifunza nini kati ya hivo juu?
 
Mkuu umemaliza kila kitu , mama angu alikuwa anapenda kulima mpunga tukitoka shule anatupeleka shamba mzee mpak unachukia , shamba likichanganya Sana anawapiga stop hata kwenda skul sku mbili mnaenda shamba .,... Nikamaliza chuo ajira ikazingua mzee , nikaona fursa ya kulima , nilikichafua mpak kijiji kizima wakahs natumia ndumba , nilikuwa kwenye top five ya watu walioscore mpunga mwingi huku Mimi peke yangu ndo kijana ......
Uzoefu ambao mama alinipatia siwez kuusahahu kamwe na hapo ndo nilipata mtaji wa kufanyia harakat zingine town ....

Sisi waafrica akli za kurithishana hatuna yaan Baba hatak mwanae ajue kiundani what is going on kuhus maswala ya uchumi wa familia , akifa na uchumi unakufa , kongole Kwa wachaga na watu wa Asia

..huenda tatizo letu ni "kuasi" kilimo, ufugaji, na uvuvi.

..Waafrika tuna ujuzi wa muda mrefu wa kilimo, ufugaji, na uvuvi, sasa kwanini hatuboreshi maarifa ya mababu na wazazi wetu ili tuwe matajiri?

..Binafsi naamini waafrika tukijikita kuboresha maarifa yetu tunaweza kuwa matajiri ktk sekta za kilimo, ufugaji, na uvuvi.

..Waasia wametuzidi ktk biashara kwasababu hilo ni eneo ambalo wazee wao wamekuwepo kwa muda mrefu kutuzidi Waafrika. Na huenda tamaduni[kuishi kwa wazazi hata baada ya kuoa...] zao zinawapa advantage ya wao kufanikiwa ktk biashara kuliko Waafrika.

..Huenda wapo Waasia wanaulizana, " mbona ktk jamii zetu hakuna wakulima na wafugaji " ?

..Ushauri wangu ni kwamba Mmaasai anapopata mtaji asianzishe duka, bali arudi kwenye ufugaji wa kisasa. Mhehe akipata mtaji arudi akaanzishe mradi wa kilimo, na jamii nyingine kulingana na maarifa ya muda mrefu waliyonayo.

..Pamoja na hayo Waafrika hatupaswi kuogopa kuingia ktk biashara isipokuwa tutambue kwamba ili tufanikiwe tunapaswa kuzingatia NIDHAMU inayotakikana ktk biashara husika.
 
Umefanya nijiulize Kama walianzaga kutuuza sisi tu wakati wa biashara ya utumwa watashindwaje kutoboa..?!
Wana experience ya kutosha tulishawahi kuwa bidhaa kwao Sasa ulishaona wapi bidhaa inamzidi muuzaji..
Enzi za utumwa zenyewe bado Zina prove kuwa sisi blacks hatukujiatambua
Mwarabu mmoja aliwezaje kutoka na kundi la watumwa kutoka Tabora Hadi bagamoyo ? Hatukuwa hata na means ya kumtoroka ?
 
Enzi za utumwa zenyewe bado Zina prove kuwa sisi blacks hatukujiatambua
Mwarabu mmoja aliwezaje kutoka na kundi la watumwa kutoka Tabora Hadi bagamoyo ? Hatukuwa hata na means ya kumtoroka ?

..Waafrika walikuwa wakikamata watumwa na kumuuzia Muarabu.

..Na huko njiani walilinda misafara ya watumwa kwa kutumia BUNDUKI na walikuwa na wasaidizi wa Kiafrika.

..Kwa kifupi biashara wa Watumwa ilikuwa hivi: kabila X lilikamata watumwa toka kabila Y kwa kutumia bunduki walizopewa na Waarabu. Na walishirikiana na Waarabu kusafirisha watumwa hao kwa malipo mbalimbali ikiwemo bunduki na risasi nyingi zaidi.
 
..Waafrika walikuwa wakikamata watumwa na kumuuzia Muarabu.

..Na huko njiani walilinda misafara ya watumwa kwa kutumia BUNDUKI na walikuwa na wasaidizi wa Kiafrika.

..Kwa kifupi biashara wa Watumwa ilikuwa hivi: kabila X lilikamata watumwa toka kabila Y kwa kutumia bunduki walizopewa na Waarabu. Na walishirikiana na Waarabu kusafirisha watumwa hao kwa malipo mbalimbali ikiwemo bunduki na risasi nyingi zaidi.
Asante kwa kunielewesha !!
 
Enzi za utumwa zenyewe bado Zina prove kuwa sisi blacks hatukujiatambua
Mwarabu mmoja aliwezaje kutoka na kundi la watumwa kutoka Tabora Hadi bagamoyo ? Hatukuwa hata na means ya kumtoroka ?
Duh Aisee,kaka umepiga msumri moyoni,hii inauma sana sababu ni kweli. Yaani hatukuwa na hata kaujanja cha kuwakimbia au kuwabadirishia kibao.Afadhali hata wahindi wekundu(Native Americans) wa America walizichapa na hawakukubali kuwa watumwa.
 
Asante kwa kunielewesha !!

..Asante.

..kwa uelewa wangu MGENI hawezi kufika mahali popote akafanya jambo jema au baya bila msaada wa WENYEJI.

..Wageni waliokuja kueneza dini walisaidiwa na wenyeji wa maeneo waliyofikia.

..Wageni waliokuja kutafuta watumwa nao walisaidiwa na wenyeji ktk unyama huo.

..Hata serikali za Wakoloni zilikuwa na maaskari polisi, na wanajeshi, ambao ni Waafrika wenzetu.
 
Nafanya kazi na wahindi. Sio wote ni wafanya biashara. Na wafanya biashara wengi wanatokea kwenye maeneo ya Kasikazini, wakina Patel. Ukija kusini, kuna wahindi wa Ki-talegu. Wao na biashara ni vitu mbalimbali. Wengi wanapenda kazi za kuajiriwa.

Pili biashara za waarabu na wahindi ni za kifamilia. Hivyo maarifa mengi ya biashara yanapatikana kwa kufanya biashara ndani ya familia toka ukiwa mtoto.

Familia zetu nyingi ni za kilimo, uvuvi na ufugaji. Unapopelekwa shule, unapewa elimu ya kukimbia kilimo, uvuvi na ufugaji. Na unapewa elimu ambayo haina maarifa ya kufanya biashara ya kifamilia.

Swali linakuja je wewe utakuwa na maarifa gani zaidi ya kutafuta kazi ya kaajiriwa?
 
Waahidi, wapakistani na WaBangladesh wanatuzidi nini kwenye biashara?

Ni nini ambacho sisi weusi tunakosea. Wengi wao wakifungua tu biashara unaiona hiyo inanyanyuka mdogomdogo.

Na sio kama wanaanza biashara kubwa.

Nimekuwa najiuliza saana ni wapi sisi tunapokosea....kuna mmoja nilisoma naye akafaulu lakini akasema siendi chuo...akaanza kununua n'gombe nami nikaanza ila leo hii jamaa humgusi.

Hata huko Canada na Ulaya...hawa jamaa wanaanza biashara kiutani utani tu baada ya miaka kadhaa wanaanza kuajiri wabeba box.

Kuna mwenye kujua hawa jamaa wanatuzidia wapi kwenye biashara??

Ipo kwenye damu?

Wana loga?

Wananidhamu na wanachokifanya?

Wanatumiwa mitaji kutoka kwao?


Hao wajanja kitambo sana, wakati waafrica na wabongo included wakiishi kwenye mapangohaojamaa waliwageuza bidhaa.
Sasa utashindana na watu waliofikia kumuuza babu yako mzaa babu yako iliwapate mshiko...ukizubaa jamaa wanaweza uza hata dunia kwa wenye uhutaji wa hii dunia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom