Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,919
- Thread starter
- #21
Ndo sisi tunakutana sokoni nanunua dagaa, nyanya chungu n.k
nahemea vitumbua vya kunywea chai pale kwa bibi athumani
ila huku ntaandika natoka shopping supermarket nimenunua fillet na hapo kwenye vitumbua ntasema nimekula baga
Mupenzi anaishi nyumba ya pili kutoka hapa uswazi kwetu anazurura tu ila huku ntasema yupo nje kikazi
rahaaa utamuuuuu
Hahahahaaa
Na ukisema hivi mtu anakuchukulia kama vile mtu fulani hivi wa maisha ya kati kumbe ni wewe tunakutana uswazi kila uchao
Kazi inakuwa kubwa pale kunapotokea sababu ya mimi na wewe tunaewasiliana mtandaoni kuonana
Itabidi ukope ili ukanunue nguo za kufanana na ile hadhi yako ya mtandaoni na utaniambia tukutane kwenye vle viwanja vya bei
Baada ya kukutana na mimi unaanza kukimbizana na wanaokudai
Kaaazi kweli kweli!