Hawa wanaitwajwe kwa kiswahili na kidhungu?

tulizoea kuwaita karunguyeye lakini sidhani kama ndo jina sahihi!!

Hilo ndo jina lake sahihi. Tatizo waswahili mnataka vitu vingine tofauti na vile mnavyovitumia. Lugha ni sauti za nasibu, kile jamii iitacho ndicho sahihi. Jina la huyo mnyama ni karunguyeye, kama ana jina lingine basi nalo silikatai ila hili ndilo jina lake
 
mkuu hivi wanaliwa hawa!!
 
2f1b78a478b2cd4820cc3c47c6ef0b9d_720x560.jpg

Huyu anaitwa kalunguyeye.
Kalunguyeye ni mnyama wa familia Erinaceidae wenye miiba.
Kiingereza: hedgehog.
 
Viumbe wana nyama tamu sana kama sungura. Porcupine/kalunguyeye/nungunungu. Miba yake pia ni dawa.
 
Mkuu porcupine wapo huku africa wengi tu. Hawa kwa kiswahili wanaitwa Nungunungu.

Mkuu hao pichani sio Nungunungu, japo ni kweli wanapatikana Africa, ukiwa Moshi na Arusha utawaona wengi tu mashambani na hata karibu na nyumba.

Nungunungu ni mnyama mkubwa kuliko paka na hao pichani hawakui kumfikia domestic cat. Huko kaskazini wanawaita Kalunguyeye na ni wapole sana. Nungunungu

porcupine_rctb-9975.jpg

huyu ndie nungunungu, na unaweza kuona miba yake ilivyo mikubwa na picha ya chini ndio kitu kinaweza kukupata endapo ukimkimbiza nungunungu kienyeji

porcupine2_sm.jpg

Huyo mbwa umbea umemuisha.

Kalunguyeye ni kamnyama jamii ya panya na miba yake haitoki. Ukimgusa kalunguyeye anajikunja kama tairi kwa kujikausha lkn ukimgusa nungunungu yatakupata yaliyompata huyo mbwa.

Miba ya nungunungu hii hapa, wabunifu hutengenezea vito. Miaka fulani nikiwa sekondari nilikuwa na kalamu ya mwiba wa nungunungu

porcupinequill.jpg
 
nawapenda sana hawa wadudu aani nikiwaona nahisi raha ya ajabu sana nikikuta kagogwa na gari huwa nasikitika sana kuna wakati sijui walijua ninavyowapenda wakahamia hapo nyumbani wengi sana nikuwa wakutoka kwenye maficho yao haswa nyakati za usiku natoka hapo nje kuwaangalia tatizo mbwa walinisaidia kuwauwa sana kwasasa huwa namwona moja moja wa bahati nahiaji kuwafuga hawa
 
Mkuu hao pichani sio Nungunungu, japo ni kweli wanapatikana Africa, ukiwa Moshi na Arusha utawaona wengi tu mashambani na hata karibu na nyumba.

Nungunungu ni mnyama mkubwa kuliko paka na hao pichani hawakui kumfikia domestic cat. Huko kaskazini wanawaita Kalunguyeye na ni wapole sana. Nungunungu

porcupine_rctb-9975.jpg

huyu ndie nungunungu, na unaweza kuona miba yake ilivyo mikubwa na picha ya chini ndio kitu kinaweza kukupata endapo ukimkimbiza nungunungu kienyeji

porcupine2_sm.jpg

Huyo mbwa umbea umemuisha.

Kalunguyeye ni kamnyama jamii ya panya na miba yake haitoki. Ukimgusa kalunguyeye anajikunja kama tairi kwa kujikausha lkn ukimgusa nungunungu yatakupata yaliyompata huyo mbwa.

Miba ya nungunungu hii hapa, wabunifu hutengenezea vito. Miaka fulani nikiwa sekondari nilikuwa na kalamu ya mwiba wa nungunungu

porcupinequill.jpg

hawa kalungu yeye kwa imani za kwetu ni kwamba wakija hapo nyumbani wankuletea hela ya hatari na hao nungunungu miiba yake huwa tunaitumia kuweka kwenye mlango ili mwizi asiweze kuingia ndani hii ni kwa mujibu wa mila mbofumbofu
 
ha ha ha ha!mkuu nitaning'iniza na mimi mlangoni!!
 
...wakija hapo nyumbani wankuletea hela ya hatari ...
mkuu wakati wamehamia kwako kwa wingi kabla ya kuwindwa na mbwa vipi uchumi wako ulikuwaje na sasa uko vipi!!!
 
mkuu hivi wanaliwa hawa!!

Mkuu, hawaliwi na ni wapole sana. Ukiwagusa tu wanajiviringisha na kuficha vichwa vyao na kuwa kama jiwe la mviringo. Wenyewe wanafanana kwa kiasi fulani na panya, isipokuwa tu wao nywele zao ni miiba
 
mkuu wakati wamehamia kwako kwa wingi kabla ya kuwindwa na mbwa vipi uchumi wako ulikuwaje na sasa uko vipi!!!

aisee ulikuwa poa kinyama yaani kwasasa sijui kama ndio uchumi umeyumba au matumizi yameongezeka
 
ha ha ha ha!mkuu nitaning'iniza na mimi mlangoni!!

sio kuninginiza mlngoni unatakiwa uichomeke kwenye kizingiti cha mlango kwa kuelekeza ule upande wenye makali chini au kutoka kona moja ya mlango kwenda kona nyingine yaani mwizi akija anaishia hapo nje hii nayo imework sana nyumbani aliwahi kuja mwizi wakati fulani tukamkamata kama kuku
 
Hilo ndo jina lake sahihi. Tatizo waswahili mnataka vitu vingine tofauti na vile mnavyovitumia. Lugha ni sauti za nasibu, kile jamii iitacho ndicho sahihi. Jina la huyo mnyama ni karunguyeye, kama ana jina lingine basi nalo silikatai ila hili ndilo jina lake
Na nungunungu ni yupi???
 
Back
Top Bottom