Zamaulid
Kalunguyeye ni wanyama wenye miiba wa nusufamilia Erinaceinae katika familia Erinaceidae. Wanyama wengine ambao wana miiba ni nungunungu na ekidna, lakini hawa hawana mnasaba na kalunguyeye.
Nungunungu wamo katika oda ya wagugunaji (Rodentia) na ekidna katika oda ya mamalia wanaotaga mayai (Monotremata), ambapo kalunguyeye ni wanyama wanaokula wadudu (oda Erinaceomorpha au oda ya zamani Insectivora).
Spishi za Afrika
Kalunguyeye Tumbo-jeupe au wa Kawaida (Four-toed hedgehog) Atelerix albiventris,
Kalunguyeye Kaskazi (North African hedgehog) Atelerix algirus,
Kalunguyeye Kusi (Southern African hedgehog) Atelerix frontalis,
Kalunguyeye Somali (Somali hedgehog) Atelerix sclateri,
Kalunguyeye Masikio-marefu (Long-eared hedgehog) Hemiechinus auritus,
Kalunguyeye-jangwa (Desert hedgehog) Paraechinus aethiopicus,
Spishi za mabara mengine
Erinaceus amurensis (Amur hedgehog)
Erinaceus concolor (Southern white-breasted hedgehog)
Erinaceus europaeus (European hedgehog)
Erinaceus roumanicus (Northern white-breasted hedgehog)
Hemiechinus collaris (Indian long-eared hedgehog)
Mesechinus dauuricus (Daurian hedgehog)
Mesechinus hughi (Hugh's hedgehog)
Paraechinus hypomelas (Brandt's hedgehog)
Paraechinus micropus (Indian hedgehog)
Paraechinus nudiventris (Bare-bellied hedgehog)