Hawa Waha wanaokopesha vyombo ni wachawi kweli kweli

Dah Mleta mada umenikumbusha enzi zangu... Kumbe nyie ndo Huwa mnatusumbua eeh
Ngoja nikwambie kitu kidogo usiojua, Pamoja na kuwa mim muha lakini sio wote wanatumia uchawi na wakat nafanya hiyo kazi na vijana Wangu wote hatukuwahi tumia uchawi ata punje na Bado unasema na wateja Kama kawa.

Huwa ipo hiv
Mim napo nunua mzigo Huwa najua kabisa katika pisi hizi kumi Nane ndio tapata pesa hizi mbili zinaweza kutana na wezi au matapeli kama nyie kwahiyo hata ikitokea siwezi toka mchezoni.

Pia iko hivii Huwezi kopesha Sehem moja Kila siku naweza kopesha Vingunguti miezi mitatu Nikahamia Ubungo Kimala nikaenda Mbagala then Nikaludi Vingunguti tena. Sas Kuna ile mtu umemkopeshea Buza akahia Ubungo na Mungu alivyo Mkubwa Ile Nahamishia Kambi Ubungo Mala paa tunabambana uso kwa uso Apo ndo shoo Panakuwaga hapatoshii.
Hasa dada zangu wauza Bar anakumbia bila kukwambia Alafu ile Bar aliyo hamia kumbe ndo maeneo yako ya kujidai unawateja Kama wote , ukimkuta anakuwa mpole kinoma so mnafanya kuanzia mlipo ishia.

Yote kwa yote Ni kazi ambayo ukizoea kudai watu raha sana asee
 
Ivi kwanini mtu anakua na roho ya utapeli,kwanini mtu anachukua kitu Cha mtu unajua kabisa sitomlipa.

Aisee tubadilike.
Mkuu unapokopa wala hupangi kua hutolipa , na unakua na mipango hasa kua mtalipa hivi au vile. Sasa Kwa kua kukopa ni Pepo , hivi ukipata hela ya kulipa linakuja wazo ngoja nimpe robo wakat mfukoni ipo yote . Hapo ndio shida huanzia mkuu
 
Kununua kitu kwa kulipa kidogo kidogo ni hasara.
Simu ya 300000 mtu hulipia 700000
 
Nilijaribu kukopa begi la elfu 65 huku nikilipishwa bukumbili kila siku hadi itimie yote, kwa thamani ya lilie begi Kariakoo imezidi sana 35 ndio nikapanga kumlipa 40 kwa huruma yangu.

Sasa hawa jamaa huwezi kuwadhurumu aseee, hata ukisafiri mwaka ukirudi utamkuta anakusubiri.

Kuna jamaa yangu bingwa wa kutapeli lakini amefeli mission zote, yeye alichukua feni sasa kila chocho atakayopita muha huyu hapa, na siku akiwa job muha hatokei ila akiwa home tuh Muha anaoteshwa huko chap amefika na daftari lake, jamaa bila kudaiwa yeye mwenyewe anatoa pesa yake.

Hawa jamaa ni hatari kwa mambo ya mikopo usijaribu kuwakopa kama huna uhakika maana kazi ya kukopeshana na kudaiana ilivyo ngumu lakin kwao wanaimudu kwelikweli.
Ukijua ni kukopa ujue na kulipa ukiweza kukopesha na kudai uweze
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom