Hawa viumbe wa namna gani?!

Hawa viumbe wa namna gani?!

displayname

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,972
Reaction score
1,091
Wanabodi ni siku kadhaa sasa nimeona hawa wadudu nyumbani kwangu tena chumbani pa kulala! Kila nikiwaona nawafagia na kuwatupa nje.

Mwanzo hawakuwepo wala sikuwahi wona ila walipoanza kujitokeza pamoja na kuwafagia nawakuta tena na tena ukutani na chini ya uvunguni mwa kitanda!

Wajuzi wa mambo naomba nifahamishwa ni wadudu wa namna gani hawa wanaitwaje na wanamaanisha nini kwenye maisha mwetu aidha maana ya kimwili na hata kiroho pia kama ipo!

Wamekuwa wananikera saana sasa badala ya kuwafagia na kuwatupa nje sasa nawachoma moto!

Mshana Jr and others msiache kupita hapa!View attachment 1872524
Screenshot_20210729-095537_Gallery.jpg
View attachment 1872523
View attachment 1872547View attachment 1872548View attachment 1872549
 
Chonde chonde mkuu usiwachome Moto hao ndio baraka zko ole wako! Narudia ole wako uwachome!
 
Nifanyie takeaway ukiwaanda!!
Mimi hua nawachukua na kuwaweka sehemu mzuri wajae na majirani zangu hua wananiletea, nikiwaandaa ntakufungia fungu kwa 3500
Sidhani kama ukipata muda wa kufikiria upya, unaweza comment hivi tena.

U seem to be smart, sasa unakwama wapi broh?
Hapo ndo nimemaliza mkuu hakuna point of return.
 
Siku ya kwanza nilipowaona nilijua ni maganda ya iliki ila nikajiuliza yamefikaje chumbani? Hadi nilipoona kichwa ndio nikajua mdudu, hata hivyo najitahidi sana usafi na napiga deki kwa deto kidogo nachanganya kwenye maji inasaidia
 
Jamii Forum ya sikuhiz daah,unaweza ukawa na Jambo lakini ukifikiria majibu ya humu unabaki nalo Tu Jambo lako...Mkuu mwenyewe nawaonaga sijui wanaletwa na nini ngoja tusubiri Kwa wenye ufahamu zaidi,kuwa mvumilivu na majibu ya Wananzengo humu.
Msaada unaotarajia Wapata Masihara usiyoyafikiria!!
 
Siku ya kwanza nilipowaona nilijua ni maganda ya iliki ila nikajiuliza yamefikaje chumbani? Hadi nilipoona kichwa ndio nikajua mdudu, hata hivyo najitahidi sana usafi na napiga deki kwa deto kidogo nachanganya kwenye maji inasaidia
Usafi wafanyika lakini hawaishi! Labda ni opt kufanya fumigation!
 
Google case bearing moth uwajue usije ukashikisha watu uchawi [emoji1787][emoji1787] na hyo ni stage Yao ya ukuaji Tu chief huwa mara nyingi wanakuwaga kwenye kuta

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Wanakuwa kuelekewa wapi mfano nakumbuka buu sijui bua ni stage ya kukua kuwa kipepeo.

Thanks ngoja ni google
 
Wanabodi ni siku kadhaa sasa nimeona hawa wadudu nyumbani kwangu tena chumbani pa kulala! Kila nikiwaona nawafagia na kuwatupa nje.

Mwanzo hawakuwepo wala sikuwahi wona ila walipoanza kujitokeza pamoja na kuwafagia nawakuta tena na tena ukutani na chini ya uvunguni mwa kitanda!

Wajuzi wa mambo naomba nifahamishwa ni wadudu wa namna gani hawa wanaitwaje na wanamaanisha nini kwenye maisha mwetu aidha maana ya kimwili na hata kiroho pia kama ipo!

Wamekuwa wananikera saana sasa badala ya kuwafagia na kuwatupa nje sasa nawachoma moto!

Mshana Jr and others msiache kupita hapa!View attachment 1872524View attachment 1872525View attachment 1872523
View attachment 1872547View attachment 1872548View attachment 1872549
Wanaitwaje aiseee na onyo lako lamaanisha nini chief?!
Imani imani...kibwetere
 
Back
Top Bottom