Hawa SHILAWADU wa Kenya ni kiboko

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
59,409
119,108
Ramadhan Mubarak
Kuna kipindi cha televisheni huwa naangalia kwa jirani yangu mama Imma. Wale wenye ving'amuzi vya startimes kuna channel inaitwa St swahili.... Basi bwana siku ya Alhamisi na ijumaa kuna kipindi kinarushwa kinaitwa ANIKWA

Kwenye hiki kipindi kunakuwa na watu wawili wanaoshea mpenzi inaweza kuwa wanawake wawili au wanaume wawili, wanaandaa kitu kama fumanizi bila mhusika anayewachanganya kujua ila wenyewe wanakuwa wanajua kinachoendelea.

Aisee huwa kunatokea viroja vya kufa mtu, wengi wanaokutwa na maswahibu hayo ni wanaume, huwa wanakuwa na reaction tofauti....mwingine anaweza kutimua mbio, mwingine anachagua mmoja anambembeleza na kuondoka nae.

Kuna huyo mmoja aliniacha hoi akawaambia mimi nina mke na watoto watatu naomba msinisumbue mwingine anakuwa dilemma hajui achague yupi.

Huwa kila siku najiuliza hivi kitu kama hiki kikifanyika hapa kwetu kwa hawa kaka zangu wabongo yule dada anayetangaza kile kipindi wangemteka au ipo siku angechezea kichapo heavy maana kaka zangu kwa kuhusudu michepuko hawana mpinzani, mbaya zaidi hawakubali kuwa ni kosa yaani wanaona ni haki yao na ni hawatakiwi kuhojiwa wala kulaumiwa kwa hilo

Naomba nirudi kwenu wadau, ungekuwa wewe unafanyaje? Ghafla bin vuu unaona umekutanishwa na wapenzi wako wawili mbele ya makamera utafanyaje? Je huyo mpenzi aliyekuletea hayo makamera utaendelea naye? Wewe unaweza kutumia njia hiyo kumuanika mpenzi wako unayehisi anakusaliti? Na ukishamuanika unaendelea nae au ndio kwa heri?

Uzi tayari
 
Wanaume wa kenya kumbe nao amna kitu tu.
udakutz_-20181221-0001.jpeg
 
Naamini watakuwa na vibali maalumu.

Kenya ni wabunifu, ila waliiga ulaya.
Kwa wale wanaotumia Dstv watanielewa zaidi. Ila kwa mara ya kwanza nilikiona kupitia StarTimes.

Huwa najiuliza hata mimi bila majibu. Tena wanafuatilia matukio mengi mno ili kukamilisha fumanizi moja. Tena linakuwa fumanizi kabambe.

Tena kwa wazungu kuna wakati wanakuwa na polisi kabisa.
 
Naamini watakuwa na vibali maalumu.

Kenya ni wabunifu, ila waliiga ulaya.
Kwa wale wanaotumia Dstv watanielewa zaidi. Ila kwa mara ya kwanza nilikiona kupitia StarTimes.

Huwa najiuliza hata mimi bila majibu. Tena wanafuatilia matukio mengi mno ili kukamilisha fumanizi moja. Tena linakuwa fumanizi kabambe.

Tena kwa wazungu kuna wakati wanakuwa na polisi kabisa.
Duuh polisi wanafuata nini sasa
 
Kuna kipindi nilkuwa nakiangalia sana ila siku hizi sikifuatilii sana ila huwa kinachekesha sana asee!
Vipindi vya kikenya huwa navipenda sana
Anikwa
Kaa rada
Naswa
Vioja mahakamani
Churchill Show
Nk!
By the way Khantwe msalimie sana mama Imma
 
Back
Top Bottom