Hawa Nghumbi amrudisha John Mnyika Mahakamani...

Huyu Mama Hanakazi ya Kufanya?kwanini Pale Lumumba wasianzishea Councelling Session kwa watu kama hawa?
 
ni nani kamtuma huyu dada anahangaika namna hii ?
my take ni kwamba kama anatakiwa alipe fedha kiasi
fulani baada ya kukata rufaa atalipa fedha nyingi zaidi?

halafu kama ni mpenda maendeleo ya jimbo la ubungo kwa nini aendelee
kumsumbua mbunge wa jimbo hilo ili hali anajua hawezi kumshinda?
 
Huyu mama gharama za kulipia kesi ndio zinampa stress halafu na zile gharama alizotumia wakati wa kampeni lazima achanganyikiwe na atupwe mirembe
 
wakubwa!nadhani kinacho msumbua huyu mama ni kujalibu kutafuta namna ya kukwepa kumlipa Mnyika gharama za kesi.Anatapatapa tu lakini ukweli utabaki palepale,wapo watu wakustail rufaa ambao wakikata rufaa mpaka umma ukasema yes lakini si huyu mama,kachemsha asubiri aibu ya pili
 
Huyu mama gharama za kulipia kesi ndio zinampa stress halafu na zile gharama alizotumia wakati wa kampeni lazima achanganyikiwe na atupwe mirembe

atalipa tu!hana ujanja,anambwelambwela tu,kutafuta aibu ya pili
 
Mahakimu wa kushughulikia kesi za kifisadi hakuna, wanacheza makidamakida na kesi za uchaguzi! Hata kama atashinda in 2013, aapishwe, ashukuru wananchi, azoee mjengo, muda wa kazi umeisha. Anarudi kuaga wananchi!

Next time hata wanaccm hawatampigia kura hata moja, a-appeal on zero votes against the massive!
 
Hawa Nghumbi kwani maisha bila ubunge hayawezekani ki ukweli jimbo la Ubungo huwezi kushinda...jipange na kazi zingine.
kwa mara ya kwanza mkuu tangu nijiunge jf leo ndio nimeona umenena
 
Kama kweli sisi tunaheshimu utawala wa sheria na demokrasia pia lazima tukubali kuwa ni haki yake kikatiba kukata rufaa! Acheni aende huko mahakamani tena haki ndio itapatikana huko!
Ninakubaliana nawe kabisa Mkuu, kama katiba inmruhusu, mwacheni aende hata Mahakama ya Kimataifa. Ikiwa anakimbia kulipa gharama, na akifika huko akashindwa tena na bila ya shaka atashindwa, gharama zitaongezeka na aibu juu. Sikio la kufa.

Hawa Nghumbi kwani maisha bila ubunge hayawezekani ki ukweli jimbo la Ubungo huwezi kushinda...jipange na kazi zingine.
Ninakubaliana kabisa na wewe Mkuu.

kwa mara ya kwanza mkuu tangu nijiunge jf leo ndio nimeona umenena
Tena kwa kuwa ritz1 amesema kile anachoamini, isipokuwa hapa kamsema wa CCM, leo amenenaik, lakini siku akisema anachoamini kwa kuisema CDM, huwa hasemi, anapayuka tu. Uhuru wa kutoa maoni haushii katika kusifia chako na kukosoa cha wenzako tu.
 
Hongera Mama HAWA N'GUMBI hakika umefanya lile nilikuwa nataraji ufanye Ni ukweli usiopingika kama huyu jamaa mnyika hakushinda pale ubungo inawezekana kabisa wewe ulishinda kuna ushahidi wa kimazingira hata kesi chadema walitoa rushwa.
HALAFU JAMANI HUYU MNYIKA MBONA MIMI SIJAONA UWEZO WAKE KILA NIKIMUONA ANAONGEA NAONA ANAONGEA KWA JAZBA CHUKI KIKANISAKANISA HIVI!!!HANA HATA TONE YA KIUONGOZI NITLFAUTI KABISA NA KAKA NAPE.:A S 12:
 
endapo mlalamikaji hakuridhika ....Kwa lengo la kudai haki ni haki yake kikatiba na kisheria kudai haki katika ngazi ya juu ya mahakama
 
Mnyika tunaomba umsamehe huyu mama zile gharama anazotakiwa kukulipa ili uendelee na mchakato wakuleta maendeleo Jimboni kwako asikupotezee muda bwana! Kwan Niniii??
 
Back
Top Bottom