Hawa ndiyo Marais pekee waliokuwa na Intelligence kubwa katika lugha

Kuna machizi uingereza au South Africa wanaongea kingereza saaafi tuu
Kwetu huku kuna haja ya kuilemisha jamii ya kwamba kujua kuongea kingereza sio alama ya kuwa msomi mtajika au mtu ulostaarabika
 
Miaka hii imekuwa ngumu sana kuwapata wasomi kama wewe. Wenye uelewa.
Kwa ujumla kipimo cha intelligence ni pamoja na uwezo wa kufundishika.

Kama umefundishwa kitu kwa miaka 7 hukuelewa, miaka 4 hukuelewa, miaka 2 hukuelewa, miaka 3 hukuelewa, miaka 2 hukuelewa. Basi ni dhahiri una low IQ.

Tanzania ina two official languages:

1) English - ndiyo maana hata sheria zetu zote zinatungwa kwa kutumia lugha ya Kiingereza, kisha zinatafsiriwa kwa Kiswahili

2) Kiswahili - ni lugha ya pili rasmi baada ya Kiingereza.

Tuna hizo lugha mbili tu ambazo ni official. Ikitokea huzijui hizo zote mbili, kwa kweli ni tatizo maana siyo kitu kinachotazamiwa.

English na Swahili - ukilinganisha na enzi za Jesus Christ, ni sawa na Greek na Hebrew. Kigiriki ilikuwa ni official language ya kwanza, lugha ya wasomi na mambo yote yaliyoonekana ya kitaalam. Kiebrania ilikuwa ni lugha iliyotumika zaidi kwenye mawasiliano ya watu wa kawaida, au tuseme ni lugha ambayo iliongewa zaidi na watu ambao hawakuwa wameenda shule.

Wasomi walishangazwa na uwezo wa Yesu kuongea Kigiriki na wakati hakwenda shule. Uwezo wa kumudu lugha na mpangilio wa kuongea ndiyo ishara ya mwanzo ya kumtofautisha mtu mwenye weledi na ambaye hana maana hatutembei tukiwa tumebeba makaratasi ya mitihani bali vichwa vyetu ambavyo hutoa tulivyo navyo vichwani mwetu kwa vinywa kwa kunena kwa ufasaha lugha zinazoeleweka kwa wenzetu.

Hata ungekuwa physist wa hali ya juu kiasi gani lakini unaenda conference unaanza na ze ze ze nani hii, hakuna atakayekuona unacho hicho ulicho nacho.

Tuwahimize watoto wetu kujifunza kwa bidii na kuzimudu lugha zetu hizi mbili maana wakishindwa kuwasiliana, hata maarifa waliyo nayo, hayataweza kuonekana.
 
Kitu kingine ambacho wenzetu wanazingatia mbali na ku master lugha ni uwezo wa kuwasilisha mada au mawazo yako ndani ya muda mchache na kueleweka, ndo maana kuna hadi mashindano ya kuwasilisha ndani ya dakika 3. Mtu ambae ana misamiati ya kutosha kwenye lugha ana uwezo wa kucheza na maneno na akaongea kwa kujiamini kabisa na akaweza ku master hata muda anaohitaji kuwasilisha mawazo yake na kila mtu akamwelewa.
Watanzania wengi hata kuongea Kiswahili hawawezi!

Hawawezi kuzungumza haraka na kuzungumza vitu vyenye mantiki kwa sababu ya tatizo la msamiati hafifu na upeo mdogo wa kufikiri.
 
Akili zimegawanyika katika makundi kadhaa. Sitopenda kuzungumzia hayo makundi. Ila leo naweza kidogo kutambua Marais wawili kati ya watano ambao wamewahi kuongoza Tanzania.

Kwa upande wa ku master lugha vizuri au kuwa na intelligence kubwa katika lugha za kigeni wa kwanza alikuwa Mw.Julius Kambarage Nyerere na wa Pili ni Benjamin William Mkapa.

Hawa walikuwa wazuri sana katika lugha ya kiingereza. Tunasema walikuwa competent in english language. Baada ya hapo hatukuwahi tena kupata marais ambao sisi tunaoifaham lugha tulikuwa tuna enjoy.

Hawa jamaa walikuwa na akili. Mkapa kama angekuwa tu na uangalizi mzuri asingejichanganya na mafisadi alikuwa mmoja ya marais wenye akili.sure alikuwa na akili akaitumia vibaya.

Mwinyi alikuwa mzuri kwenye lugha mama...hii alizaliwa akiizungumza hakuna jipya sana.

Ukija kwa mzee wangu Mwinyi ,Kikwete na Dr. Magufuli. Hawa kiingereza chao ni cha ugoko.kinagonga gonga hivyo hivyo. Ze... Ze ze ze... Ndo hivyo tena.nliwahi msikiliza mara kadhaa kikwete akihojiwa kwa kiingereza ni aina ya kiingereza anachozungumza mtoto wangu wa standard 5.

Hamna kitu...alipata shida siku ile amekuja Obama anahojiwa suala la yule mfanyakzi wa ubalozini kule ughaibuni... Nikamwonea huruma.

Mwinyi hakuwa na makuu. Yeye alizoea kugonga kiswahili na was ok with that.
Kwa hiyo nawe unaona umeleta uzi wa maana ktk JF. Fara mkubwa we! Inaonekana hata hujui unachokifanya. Watu kama wewe ni wale ambao walipata majina ya bandia utotoni kwa kuramba kamasi, uliyerithi kichwa na mwili mkubwa matokeo yake biolojia ikashindwa kukupa la kujivunia. Ukitaka kujua ubovu wa akili yako Sikiliza kiingereza cha Einstein, jipime nini umefanya dunia hii kama siyo wizi wa penseli na sasa unahangaika wapi upate pesa.

Jutia kuwaambukiza watoto wako hiyo akili ndogo ya kufurahia kiingereza wakati hata wewe mwenyewe hakipandi. Utakapojibu message hii tumia kiingereza maana sitakujibu kwa kiswahili.
 
Look at the nature of the person who gives ideas.mbwa naye ni mnyama wa kufugwa ila hatunywi maziwa yake. So ukigundua kuwa ni mnyama wa aina gani then now you wont talk about mbwa's maziwa. Unamzungumzia mbwa mwenyewe.


argue against the topic not the giver of topic! shame on you DUDE!!!!😁😁😂😂
 
Mkapa ana Miaka 81 bado matamshi yake yako vyema

Nyerere alifikia Miaka hii ya Mkapa?

Ukipenda hata Chongo utaita kengeza

Mzee Mkapa hata Kiswahili chake hakina mashimo

umewahi kusikiliza debate ya Nyerere na panel iliyoinclude mke wa raisi Rosevelt mwaka 1960?,Nyerere alikuwa na Kiingereza kizuri zaidi na alikuwa na substance za kifalsafa zaidi. Mkapa anatumia zaidi misamiati migumu lakini substance density ndogo
 
umewahi kusikiliza debate ya Nyerere na panel iliyoinclude mke wa raisi Rosevelt mwaka 1960?,Nyerere alikuwa na Kiingereza kizuri zaidi na alikuwa na substance za kifalsafa zaidi. Mkapa anatumia zaidi misamiati migumu lakini substance density ndogo
kiingereza nyerere alifundishwa na waingereza,akaishi huko masomoni,akakaa nao muda mwingi..mkapa kiingereza ni masomo yake
 
Hakika,lugha ni kitu muhimu kwani hutumika kuwasiliana na wengi.Kadiri mtu ujuavyo zote mbili (au hata zaidi),kwa ufasaha na maneno ya kutosha,ni rahisi kupenyeza hoja za msingi na ukavutia wasiikilizaji wengi zaidi na kueleweka kiurahisi na hata kuweza kuathiri utendaji/utekelezaji wao kirahisi pia,japo si mara zote,maana wengine huishia kufurahia tu kusikia lugha nzuri.

Bahati mbaya,hii lugha ya kingereza haijaacha watu wengi salama nchini hata licha ya kusoma hadi viwango vya juu kabisa kwa baadhi.Sababu ya hili labda ni nyingi na hili si la kuchekana sana,japo pia,sio la kujitetea nalo ama kulifagilia sana.Hivyo vema kukazania watoto na kujiendeleza binafsi pia.

Sababu ya madhara haya ya udhaifu wa lugha ni kwa wengi na ndio hawa hawa tulio nao lakini pia ndio kusema,wapo wenye ujuzi mkubwa la lugha,lakini dhaifu sana katika mengi mengine,kama uadilifu,umakini katika mambo mengi (isipokuwa lugha tu) kukosa utashi kisiasa kukwamua nchi na wananchi n.k..Wengine wakishapata uongozi tu,wameshamaliza haja zao.Nyie wengine na mengine ni ziada tu.

Nadhani vema kuchagua yupi ama wepi wana afadhali zaidi:Yaani,wataalamu wa kuongea lugha,kupangilia maneno na hoja na wenye mvuto wakiwa majukwaani au wakijibu maswali, au wenye udhaifu wa lugha lakini labda wana afadhali kwenye mengine ya muhimu zaidi.Sababu,hasa katika kizazi hichi na kwa mfumo wetu huu wa elimu (japo haujawadhuru wote),lazima tutakuwa na wadhaifu wa lugha.

Hakika,kupata kiongozi mwenye kuvutia akiongea lugha ya kiswahili na kingereza,ni jambo jema sana na la kuvutia.Na huyo akitokea akawa pia na uadilifu na uthabiti katika uongozi na kujua kutatua shida za nchi na wananchi wake,huyo atakuwa ni baraka ya aina yake kwa nchi.Lakini je,ni rahisi kupata wa namna hiyo mwenye vyote kwa pamoja?

Nachelea tu tusije kuishia kuvutiwa na utaalamu wa lugha na mipangilio mizuri ya maneno tukajiaminisha huyo/hao ndio wanafaa kuongoza,japo pia sisemi hawafai.Na hakika,sifa hizo ni muhimu sana kwa kiongozi.Ila, si ajabu hawa wataalamu wa kingereza kuja kuishia kwenda kuzungumza hizo lugha za kingereza na wenye hiyo lugha huko nje na safari kwenda nje kutoisha kila kukicha-japo lakini,si lazima ni sababu tu ya hizo safari labda.

Hakika lugha zote ni muhimu TENA SANA.Ila,nadhani kuna vya muhimu zaidi hasa pale kunapokuwa na wingi wa mapungufu tofauti katika wengi.Si ajabu wenye hizi sifa nzuri za lugha na mengine tunao lakini ndio hawajitokezi wakajulikana katika tasnia ya kisiasa na hatimae labda wakachaguliwa kwa kura na kuja kuwa viongozi.

Ila,lugha zote mbili hakika ni muhimu sana ilimradi ndio inahitajika kutumika kiserikali.
 
Tuache ujinga na kutetea upuuzi. Kiingereza ni lugha yetu,tunaanza kufundishwa tukiwa darasa la tatu halafu kuanzia kidato cha kwanza hadi digrii ya uzamivu lugha ya kufundishia ni kiingereza. Ni mojawapo ya lugha rasmi ya uendeshaji wa serikali na pia ni lugha rasmi ya mahakama na sheria zetu. Sasa usilete nye nyee zako hapa! Kama kuna nchi huko ambayo ni Anglophone na ni member wa commonwealth halafu mkuu wake wa nchi hajui kiingereza hilo ni tatizo.
mabwege muko wengi! Nawe unaamini ni tatizo! Uko JF! Unaamini ukijua english matatizo huna! Tuanzie kwako. Unakiweza kiingereza? Eti common wealth! Mozambique wanazungumza Kiingereza? Au hujui kwamba ni member wa common wealth? Trush!
 
Una kiwango gani cha Elimu wewe? Nyie ndo wale wale wenye Elimu za kuunga na super glue.
Huwezi kuwa PHD Holder halafu Kiingereza kikutese hayo ni maajabu makubwa mno ya Dunia.
Uwezo wako wa fikra ni mdogo mno, yaani Nyerere unamfananisha na Magufuli? Kwa lipi hasa? unasifia manunuzi ya ndege ,unajua mkataba uliotumika kununua ndege?
Kama serikali tajiri ya Marekani inanunua ndege Kwenye makampuni yake ya ndani kwa mkopo, wewe unasifia ujinga usiojua lolote, hizo ndege skrepa za mitumba nyie wajinga eti mnadanganywa ni ndege mpya, wewe unajua process za kupata ndege mpya inachukua miaka mingapi baada ya purchasing order?
Unasifia maendeleo wakati nchi ipo Kwenye recession ya kiuchumi, mchele, sukari vipo bei juu, inflation ipo zaidi ya 8%,serikali huwa haifanyi biashara, sasa ATCL ilitakiwa iwe privatized na Siyo serikali ikomae kufanya biashara.
Ajira hakuna ni 0% employment rate, halafu unasema Magufuli kaleta maendeleo, nyie ndo wale ambao Prof James Watson aliwafananisha na nyani akili zenu.
Maendeleo huwa hayaandikwi magazetini, bali huonekana kwa watu, sisi tunaoishi ktk mataifa yaliyoendelea hatuoni magazetini maendeleo ya hapa bali tunayaona kwa macho.
Una akili timamu kweli wewe kusema Tanzania ina maendeleo?

Siwezi kubishana na wewe kwani umeisha sema kuwa wewe unaishi nje ya Tanzania kwenye chi iliyoendelea !!! Sisi tunaoishi Tanzania ndio tunaojua tofauti ya maisha kati ya awamu hii na hizo zilizopita!!
 
Back
Top Bottom