Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,601
- 46,244
Nchi yetu imekuwa na Marais wachache tangu kupata uhuru hivyo ni rahisi kupima legasi zao mahususi kwa upekee wa kila mmoja
Tukianza na Rais wa kwanza Mwl Nyerere anakumbukwa kwa mengi ila kwa legasi kubwa zaidi ya Uhuru na kuunda taifa moja kutoka makabila na jamii nyingi. Kwa legasi hiyo anatmbulika baba wa Taifa mpaka leo.
Rais wa Pili, Ali Hassan Mwinyi anakumbukwa kwa legasi kubwa ya kuufungua uchumi wetu na kuupeleka kwenye soko huria kutoka uchumi wa kijamaa. Kwa legasi hiyo amepewa jina maarufu la mzee wa ruksa.
Rais wa watu, Benjamin Mkapa yeye anakumbukwa kwa mambo mawili makubwa ambayo ni ubinafsishaji na uundaji wa Taasisi. Legasi yake kubwa baada ya ubinafsishaji ni serikali kuendeshwa kitaasisi.
Rais wa nne, Jakaya Mrisho Kikwete anakumbukwa kwa upanuzi wa demokrasia ndani ya bunge, vyombo vya habari na ujenzi wa barabara. Katika awamu yake hakukuwa na hofu ya watu kusema na barabara zilijengwa kuliko wakati mwingine wowote.
Rais wa Tano legasi yake kubwa ni ipi wanajukwaa?