Marais Bora wa muda wote wa Tanzania ni Nyerere halafu Kikwete

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,872
48,222
Narudia tena na tena hatutakuja kupata Marais wanaojua siasa, Uongozi na utawala Kama Rais Hayati Nyerere na mstaafu Kikwete.

Nyerere pamoja na misukosuko yote ya vita ila alisimama na watanzania na Tanzania ilibaki kuwa moja.

Nyerere alikataa uchawa Kama ilivyokuwa kwa Kikwete mambo ya kusifiwa sifiwa Hawa watu walikuwa hawataki kabisa!!

Nyerere alikuwa ni zaidi ya kiongozi ndiye alijenga viwanda karibia kila mkoa halafu mkapa akaja kuviuza vyote.

Kuna watu wanamtukana Kikwete naweza sema ni wakurupukaji tu Kikwete mambo yote ya Rushwa na ufisadi yaliasisiwa na Mwinyi na Mkapa Hawa ndio waasisi wa ushenzi na ufisadi wa kupindukia unaitafuna Tanzania.

Rais Kikwete alitaka kila mtanzania ajue kinachoendela kwenye nchi yake na hakuwa na watetezi ndio maana alionekana fala wakati rais mzuri ni yule anayeweka transparent Ili yeye aje achukue maamuzi mwishoni.

Kikwete Kama asingekuwa Samia, Sita na Mkapa now toka 2015 tungekuwa na Katiba mpya.

Hizo IPTL, Dowans, Richmond, Buzwagi na uchafu mwingine ni zao la utawala wa Mwinyi na Mkapa sema watu tunaangalia matokeo lakini hatuangalii chanzo Cha hayo matokeo. Mkataba wa IPTL kwa mfano ulisainiwa mwaka 1994 kea Mara ya kwanza.

Kikwete alikemea udini kwa vitendo na hakuwa mnafiki aliwachana waislamu waziwazi kwamba hawawezi kuwa sawa na Wakristo.

Nyerere vile vile alikemea udini waziwazi kwa kusema yeye hateui kwa kuangalia dini ya mtu ila uwezo wake na Wala dini zao hazijui.

Rais Samia hawezi kukemea udini ambao unasambaa kwenye serikali yake.

Pia Magufuli alishindwa kukemea udini na ukabila na ukanda uliokuwa ukisambaa kwenye serikali yake.

Mkapa aliua watu zanzibar kiuni Sana na hapa alionyesha udini wa Hali ya juu sana!

Samia Kama ilivyokuwa Mkapa, Magufuli na wote hawataki kushauriwa kwa mtazamo wa ndani wanaonekana.

Mnaojua historia mkumbuke uhuru wa mahakama na uendeshaji wa kesi kwenye utawala wa Nyerere na Kikwete.

Rais Samia anahubiri utawala wa sheria halafu anawakumbatia watu wasiyofuata sheria ndani ya bunge na serikali.

Rais lazima awe wa watu, aruhusu bunge huru, akosolewe na awe mzalendo asiwe na makando kando ya wizi na ufisadi, asiwalinde majambazi na kuwatukana raia wake. Ndiyo maana kwenye utawala wa Nyerere watu wengi walijiuzulu na pengine utawala wa Kikwete ulivunja record ya watu kujiuzulu.

Sio mtu anajiuzulu kwa shinikizo la kumkosoa Rais.

Kwa Sasa hatuna Uongozi huu ni ukweli mchungu! Rais hapanic.

Mpaka kesho rais Bora ni Kikwete na Nyerere R.I.P.
 
Hakutaka tubaguane katika ukabila.
JamiiForums920307679.jpg
 
Shida hata mnaotaja Nyerere Wengi hamku feel utawala wake.

Nyerere kulikuwa na magazeti ya serikali Tu na redio ya serikali.

Kila mnachoambiwa kiko edited Kwa lengo la kupamba serikali...hakuna TV wala internet.

Chochote anacho agiza Rais ni sheria hapo hapo...hata aliagiza uchapwe fimbo.... inasemekana kina Samuel Sitta aliwachapa fimbo walipogoma Udsm.....

Sisemi haya kupinga Kuwa alikuwa Rais Bora... natamani wanaosema Rais huyu Bora na Yule sio Bora wapime Kwa mizania sawa.

Binafsi Mkapa nimekuja kumpa thamani zaidi baada ya kifo chake ...Kikwete thamani yake ilionekana baada ya kuondoka Ikulu.....sisemi yupi Rais Bora but hata Samia thamani yake itaongezeka akisha toka Ikulu naamini
 
Hata Samia thamani yake itaongezeka akisha toka Ikulu naamini
Samia hana chochote anachojua. Anaamini sana kuambiwa.

Kwa kauli yake, mwenyewe alisema anataka kuunda serikali ya kitaasisi.

Maana yake wateule wake wote amewapa uhuru wa kufanya maamuzi, ili yeye asijiumize kichwa AISHI Kama MALIKIA.

Wateule wenyewe ni takataka kabisa kina Mwigulu Nchemba, January Makmba, Mchengerwa, Nape Nnauye.

Kwasasa kila mmoja anashindana KUIBA tu.

Genge lote la wizi la awamu ya Kikwete kina Karamagi, Abbas Mtemvu, limerudi kwa Kasi KUU.

Nchi hii Sasa hivi itabaki SKELETON tu.

Samia hana MAAMUZI kabisa, yupo yupo Bora kumekucha. Hana DIRA anaongoza Kama Kama vile ni RAIS wa MPITO tu.

Hata yeye anajua ameshapuyangq, ndio maana amaekuwa Muoga wa kutisha hata mikutano ya kisiasa anaogopa, anatembelea zuio la Magufuli.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom