hawa ndio wanaume wanaoongoza kuvunja ndoa za watu

hawa ndio wanaume wanaoongoza kuvunja ndoa za watu

Umewasahau wale wanaoteuwa wabunge wa viti maalumu, n.k
 
Paw kasafiri, hajakuaga??

Beach ya mto ubungo yaweza kufaa kwa shughuli hizi, hasa chini ya daraja.

Kha! Hebu usimtaje shetwani aside akatokea. Ngoja nika-msurprise PAW wangu na lunch na a quickie garini. Can u suggest a deserted beach?
 
Hao wauza duka na wauza genge mimi naona sababu ni mwanaume mwenyewe, haya mambo ya kuwaambia akina mama hebu fanya maarifa baada ya kuona mambo yamekwama, ndio mnaishia huku. The Boss , atakuwa na ya zaidi kutokana na thread ya fanya maarifa.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu wapendwa dunia imetawaliwa na tamaa za shetani, kumbukeni alipomwambia Bwana Yesu kuwa ukinisujudia nitakupa fahari yote ya ulimwangu huu wote, jamani hakuna awezae kuushinda mwili ila yeye aliyempokea Kristo kama Bwana na mwokozi wake, na kwa msaada wa Roho Mtakatifu pekee.
 
Madam Nakshi, hebu nisaidie mimi hapo nifanyeje ikitokea mke wangu amezoeana na muuza genge? Niizibe pochi ya mke/mpenzi wangu au nifanye nini? Maana nijuavyo mimi ni kwamba hata nikisema nichimbe biti, si watapanga tu namna ya kukutana!

ktk zama hizi za ukimwi, ni kuishi kwa matumaini tu!
 
Hao wauza duka na wauza genge mimi naona sababu ni mwanaume mwenyewe, haya mambo ya kuwaambia akina mama hebu fanya maarifa baada ya kuona mambo yamekwama, ndio mnaishia huku. The Boss , atakuwa na ya zaidi kutokana na thread ya fanya maarifa.

Wazima moro!
 
Hata sie wauza urembo (rangi za kucha, chupi, sidiria, shanga, vibanio vya nywele), wauza mboga za majani majumbani na samaki wabichiii tumo ingawa hatuvumi...
 
Madam Nakshi, hebu nisaidie mimi hapo nifanyeje ikitokea mke wangu amezoeana na muuza genge? Niizibe pochi ya mke/mpenzi wangu au nifanye nini? Maana nijuavyo mimi ni kwamba hata nikisema nichimbe biti, si watapanga tu namna ya kukutana!

ktk zama hizi za ukimwi, ni kuishi kwa matumaini tu!

binaadamu hafugwi anajilinda mwenyewe cha msingi angalia pesa ya matumizi unayoacha sio umeacha hela ya bamia unakuta kuku unakula tu bila ya kuhoji zimetoka wapi hapo utakuwa umepigwa changa la macho baba
 
Na hao walioolewa na wanapata kila 'material thnigs they need' lakini bado wanaendelea 'kuliwa' na wasukuma mikokoteni shida yao nini?
 
Ongeza na hawa:
Wanamuziki
Wacheza mpira -footballers
Wabunge , hasa wa CCM

tena kwa awanamuziki huw tunajipeleka wenyewe tena tunachukua pesa tunazopewa na waume zetu tunaenda kuwahonga wanamuziki yaani hii tabia inakera sana, wacheza mpira sijuhi kwa kweli ila hapo kwa wabunge mmmh ngoja ninyamaze tu!:yawn::flypig:
 
Hao wauza duka na wauza genge mimi naona sababu ni mwanaume mwenyewe, haya mambo ya kuwaambia akina mama hebu fanya maarifa baada ya kuona mambo yamekwama, ndio mnaishia huku. The Boss , atakuwa na ya zaidi kutokana na thread ya fanya maarifa.

tena anamwambia fanya maarifa huku kajiliza kwenye sofa akiletewa mapochochopo anachekelea kabisa teh teh teh na kumalizia 'mke wangu bwana hapo ndio ninapokupendea'!
 
Umewasahau wale wanaowapaka rangi na kuwaosha miguu, looh! wanawatafuna sana wake zetu wale jamaa, ukitaka kushuhudia hili nenda mwenge pale wanapooshaga miguu wake zetu utakayoyaona utafakari mwenyewe kumkichwa! Sasa pata picha wale wanaopitaga majumbani mida ya saa 4 asubuhi, watoto wako shule yupo mkeo tu home, ha ha ha. Ukirudi mama kachooooka
 
NDUGU zangu, katika maisha ya sasa kuna watu flani ambao ukiona wana ukaribu uliopitiliza kwa mke wako, jua kuna jambo nyuma ya pazia na ukishangaashangaa unaweza kujikuta unamegewa penzi lako hivihivi.
Hiki nitakachokielezea leo nimekifanyia uchunguzi wa muda mrefu na kwa wale waliokumbana na hali halisi ya mambo, watakubaliana nami kwa asilimia zote. Juzi nilipata bahati ya kusuluhisha ugomvi wa rafiki yangu ambaye yeye na mkewe ni wafanyabiashara.
​
​
Chanzo cha ugomvi wao ni daktari mmoja ambaye inaonekana kwa muda mrefu amekuwa ‘akiitafuna’ ndoa yao na siku hiyo ndiyo ule msemo wa za mwizi arobaini ulipotimia. Rafiki yangu huyo alinasa sms kutoka kwa dokta huyo akitaka wakutane na mkewe siku hiyo.
Bahati ni kwamba, mwanaume huyo alikuwa akimpenda sana mke wake na hata nilipomshauri amsamehe waanze ukurasa mpya, alinielewa.
Lakini wakati hilo likitokea, jana yake nilisoma habari ya mke wa mtu aliyefumaniwa na kijana mmoja ambaye ni muuza genge mtaani kwao. Aibu ilioje kwa mwanamke huyo! Hivi inakuwaje mpaka mke wa mtu ambaye mume wake anahangaika juani kutafuta noti kisha mkewe huku nyuma anatoa penzi kwa muuza genge kirahisi? Hii inauma sana!
Matukio hayo mawili yalinifanya nifikie hatua ya kuandika makala haya juu ya watu wanaongoza kwa kusambaratisha ndoa za watu.​
Muuza genge
Kuna tabia ambayo baadhi ya wanawake walio katika ndoa wanayo ya kubana matumizi yao ya kila siku kwa lengo la kuweka fedha za kufanyia mambo mengine baadaye.
Katika mazingira hayo wapo wanaojiweka karibu sana na watu hao wakiamini watapewa vitu vya bure kama vile nyanya, vitunguu nk. Wanawake wa sampuli hii wakikutana na wauza genge viwembe hawawezi kupona na ndiyo maana mwanaume anashauriwa kuwa makini sana na wauza magenge.​

Mwalimu
Hapa nazungumzia zaidi walimu wa vyuoni. Baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wanawake kwa kuwaahidi kuwafaulisha kwenye mitihani na wamekuwa wakiwatishia kuwafelisha endapo watawachomolea. Hilo limekuwa likiwafanya baadhi ya wanawake wasio na msimamo kuwa tayari kwa lolote ili mradi wafaulu.​

Dereva bajaji, teksi
Nani asiyejua kuwa baadhi yao wanaongoza kwa ukware? Kwa kifupi hawa ni miongoni mwa watu ambao mwanaume hatakiwi kukubali ukaribu uliopitiliza kwa wake zao kwani historia inaonesha wengi wao wamekuwa wepesi wa kuomba penzi hasa mazoea yanapovuka mipaka.​

Muuza duka
Mama mmoja ambaye mume wake anafanya biashara za kusafiri mikoani alinaswa na mpangaji ambaye kwenye nyumba anayoishi mwanaume huyo ana duka. Baada ya tukio hilo ilibainika mama huyo alikuwa na tabia ya kuchukua vitu dukani hapo na siku hiyo alipotakiwa kulipa alimwambia kimasihara kuwa, yeye hana fedha kama vipi wamalizane kwa njia nyingine.
Kama mwanamke huyu alivyosema, wapo wake za watu ambao wamekuwa wakijirahisi sana kwa wauza duka wakijua itakuwa rahisi kwao kuambulia vitu vidogodogo na fedha. Kwa maana hiyo mkeo si wa kumruhusu kuwa na uhusiano wa karibu sana na wauza duka.​

Mganga wa kienyeji
Wapo waganga wa kienyeji ambao ni wasanii tu. Katika hawa wanaodaiwa kuwa wasumbufu kwa wake za watu ni wale wanaojidai kutibu magonjwa ya kinamama.​
​

Hapo kwenye red :A S 13::A S 13::A S 13:.. Huo urafiki na mume wa mtu unatia mashaka..:confused2::confused2::confused2:
 
Back
Top Bottom