hawa ndio wanaume wanaoongoza kuvunja ndoa za watu

Rapunzel

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
1,079
597
NDUGU zangu, katika maisha ya sasa kuna watu flani ambao ukiona wana ukaribu uliopitiliza kwa mke wako, jua kuna jambo nyuma ya pazia na ukishangaashangaa unaweza kujikuta unamegewa penzi lako hivihivi.
Hiki nitakachokielezea leo nimekifanyia uchunguzi wa muda mrefu na kwa wale waliokumbana na hali halisi ya mambo, watakubaliana nami kwa asilimia zote. Juzi nilipata bahati ya kusuluhisha ugomvi wa rafiki yangu ambaye yeye na mkewe ni wafanyabiashara.
Chanzo cha ugomvi wao ni daktari mmoja ambaye inaonekana kwa muda mrefu amekuwa ‘akiitafuna’ ndoa yao na siku hiyo ndiyo ule msemo wa za mwizi arobaini ulipotimia. Rafiki yangu huyo alinasa sms kutoka kwa dokta huyo akitaka wakutane na mkewe siku hiyo.
Bahati ni kwamba, mwanaume huyo alikuwa akimpenda sana mke wake na hata nilipomshauri amsamehe waanze ukurasa mpya, alinielewa.
Lakini wakati hilo likitokea, jana yake nilisoma habari ya mke wa mtu aliyefumaniwa na kijana mmoja ambaye ni muuza genge mtaani kwao. Aibu ilioje kwa mwanamke huyo! Hivi inakuwaje mpaka mke wa mtu ambaye mume wake anahangaika juani kutafuta noti kisha mkewe huku nyuma anatoa penzi kwa muuza genge kirahisi? Hii inauma sana!
Matukio hayo mawili yalinifanya nifikie hatua ya kuandika makala haya juu ya watu wanaongoza kwa kusambaratisha ndoa za watu.
Muuza genge
Kuna tabia ambayo baadhi ya wanawake walio katika ndoa wanayo ya kubana matumizi yao ya kila siku kwa lengo la kuweka fedha za kufanyia mambo mengine baadaye.
Katika mazingira hayo wapo wanaojiweka karibu sana na watu hao wakiamini watapewa vitu vya bure kama vile nyanya, vitunguu nk. Wanawake wa sampuli hii wakikutana na wauza genge viwembe hawawezi kupona na ndiyo maana mwanaume anashauriwa kuwa makini sana na wauza magenge.

Mwalimu
Hapa nazungumzia zaidi walimu wa vyuoni. Baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wanawake kwa kuwaahidi kuwafaulisha kwenye mitihani na wamekuwa wakiwatishia kuwafelisha endapo watawachomolea. Hilo limekuwa likiwafanya baadhi ya wanawake wasio na msimamo kuwa tayari kwa lolote ili mradi wafaulu.

Dereva bajaji, teksi
Nani asiyejua kuwa baadhi yao wanaongoza kwa ukware? Kwa kifupi hawa ni miongoni mwa watu ambao mwanaume hatakiwi kukubali ukaribu uliopitiliza kwa wake zao kwani historia inaonesha wengi wao wamekuwa wepesi wa kuomba penzi hasa mazoea yanapovuka mipaka.

Muuza duka
Mama mmoja ambaye mume wake anafanya biashara za kusafiri mikoani alinaswa na mpangaji ambaye kwenye nyumba anayoishi mwanaume huyo ana duka. Baada ya tukio hilo ilibainika mama huyo alikuwa na tabia ya kuchukua vitu dukani hapo na siku hiyo alipotakiwa kulipa alimwambia kimasihara kuwa, yeye hana fedha kama vipi wamalizane kwa njia nyingine.
Kama mwanamke huyu alivyosema, wapo wake za watu ambao wamekuwa wakijirahisi sana kwa wauza duka wakijua itakuwa rahisi kwao kuambulia vitu vidogodogo na fedha. Kwa maana hiyo mkeo si wa kumruhusu kuwa na uhusiano wa karibu sana na wauza duka.

Mganga wa kienyeji
Wapo waganga wa kienyeji ambao ni wasanii tu. Katika hawa wanaodaiwa kuwa wasumbufu kwa wake za watu ni wale wanaojidai kutibu magonjwa ya kinamama.
 
hivi kwani hao wanawake hawawezi kusema NO, nimeolewa au kuna ladha tofauti nje ambayo mumewe hana
 
Dereva bajaji, teksi
Nani asiyejua kuwa baadhi yao wanaongoza kwa ukware? Kwa kifupi hawa ni miongoni mwa watu ambao mwanaume hatakiwi kukubali ukaribu uliopitiliza kwa wake zao kwani historia inaonesha wengi wao wamekuwa wepesi wa kuomba penzi hasa mazoea yanapovuka mipaka.


are we serious about this? hivi tunataka kusema kwamba mwanamke ni kama mdoli tu ambao hauna akili wala utashi binafsi na ambao mwanaume anapaswa kuwa karibu muda wote kuulinda ili usidanganywe na wauza genge, madereva wa bajaj, waganga wa kienyeji etc? itakuwa ni kujidhalilisha kama wanawake wa JF mtashabikia hii concept
 
wanawake wana matatizo....muuza genge,mganga, dereva tax? Me nikihisi tu hao watu nakudelete mazima.. sitaki mchezo
 
are we serious about this? hivi tunataka kusema kwamba mwanamke ni kama mdoli tu ambao hauna akili wala utashi binafsi na ambao mwanaume anapaswa kuwa karibu muda wote kuulinda ili usidanganywe na wauza genge, madereva wa bajaj, waganga wa kienyeji etc? itakuwa ni kujidhalilisha kama wanawake wa JF mtashabikia hii concept

And do you agree that there are men who choose their friends wife to have them na je kwa hiyo mume hapaswi kumzuia mkewe asiwe na ukaribu wa mtu fulani?
 
Mganga wa kienyeji
Wapo waganga wa kienyeji ambao ni wasanii tu. Katika hawa wanaodaiwa kuwa wasumbufu kwa wake za watu ni wale wanaojidai kutibu magonjwa ya kinamama.


kwenye hili una ushahidi? Najua kuwa gynos wengi wanapima pima sana maeneo ya kina mama (nadhani ni sehemu a wajibu - wito kupima maeneo ya kike)
 
Mada yako umeiweka vizuri Nakshi. Ni kweli hao wote wananyemelea wake za watu.Naomba kuongezea. Kuna mama mmoja mke wa mtu alikuwa anajenga nyumba yake bila mumewe kufahamu. Alikuwa hamlipi fundi anayemjengea. Kila hatua fulani ya ujenzi ikiisha anamwambia fundi wakamalizane kwenye baa fulani ilokuwa jirani na ujenzi. Baa hiyo ilikuwa na gesti. Wakiingia huko fundi analipwa na deni linafutwa! Nyumba ikamalizika kwa dizaini hiyo ya mama.
Swala hapa ni jinsi baadhi ya wanawake (kama ilivyo kwa baadhi ya wanaume) walivyo na low morals! Waukumbuka ule wimbo wa 'kisa cha Mpemba?' Na baadhi ya sisi wanaume tuwe macho. Umeacha sh. 5000 nyumbani asubuhi ukija jioni unatengewa pilau ya kuku wee wabugia tu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom