hawa ndio wanaume wanaoongoza kuvunja ndoa za watu

acha nijipitie tu mie.....

Maana nikishangaa mke wa mtu kutembea na muuza genge itabidi nishangae mume wa mtu kutembea na hausi girl...

na ipo siku utakuja shangaa zaidi baba akatembea na mkwewe, mke wa mwanae.
 
Duh we NAKSHI kama ulikuwepo kwenye historia ya maisha yangu.Lakini pia na sisi wanaume je?
 
kwenye hili una ushahidi? Najua kuwa gynos wengi wanapima pima sana maeneo ya kina mama (nadhani ni sehemu a wajibu - wito kupima maeneo ya kike)

dunia ni watu na watu ndio sisi, kuna kila aina ya vituko ambavyo binadamu anavifanya, kwa hiyo usihitaji ushahidi wa mganga wa kienyeji vituko anavyovifanya kwa wanawake, pendelea kusoma magazeti, kusikiliza taarifa za habari za ndani na nje ya nchi utaamini kwamba haya yapo.
 
NDUGU zangu, katika maisha ya sasa kuna watu flani ambao ukiona wana ukaribu uliopitiliza kwa mke wako, jua kuna jambo nyuma ya pazia na ukishangaashangaa unaweza kujikuta unamegewa penzi lako hivihivi.
Hiki nitakachokielezea leo nimekifanyia uchunguzi wa muda mrefu na kwa wale waliokumbana na hali halisi ya mambo, watakubaliana nami kwa asilimia zote. Juzi nilipata bahati ya kusuluhisha ugomvi wa rafiki yangu ambaye yeye na mkewe ni wafanyabiashara.
Chanzo cha ugomvi wao ni daktari mmoja ambaye inaonekana kwa muda mrefu amekuwa ‘akiitafuna' ndoa yao na siku hiyo ndiyo ule msemo wa za mwizi arobaini ulipotimia. Rafiki yangu huyo alinasa sms kutoka kwa dokta huyo akitaka wakutane na mkewe siku hiyo.
Bahati ni kwamba, mwanaume huyo alikuwa akimpenda sana mke wake na hata nilipomshauri amsamehe waanze ukurasa mpya, alinielewa.
Lakini wakati hilo likitokea, jana yake nilisoma habari ya mke wa mtu aliyefumaniwa na kijana mmoja ambaye ni muuza genge mtaani kwao. Aibu ilioje kwa mwanamke huyo! Hivi inakuwaje mpaka mke wa mtu ambaye mume wake anahangaika juani kutafuta noti kisha mkewe huku nyuma anatoa penzi kwa muuza genge kirahisi? Hii inauma sana!
Matukio hayo mawili yalinifanya nifikie hatua ya kuandika makala haya juu ya watu wanaongoza kwa kusambaratisha ndoa za watu.
Muuza genge
Kuna tabia ambayo baadhi ya wanawake walio katika ndoa wanayo ya kubana matumizi yao ya kila siku kwa lengo la kuweka fedha za kufanyia mambo mengine baadaye.
Katika mazingira hayo wapo wanaojiweka karibu sana na watu hao wakiamini watapewa vitu vya bure kama vile nyanya, vitunguu nk. Wanawake wa sampuli hii wakikutana na wauza genge viwembe hawawezi kupona na ndiyo maana mwanaume anashauriwa kuwa makini sana na wauza magenge.

Mwalimu
Hapa nazungumzia zaidi walimu wa vyuoni. Baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wanawake kwa kuwaahidi kuwafaulisha kwenye mitihani na wamekuwa wakiwatishia kuwafelisha endapo watawachomolea. Hilo limekuwa likiwafanya baadhi ya wanawake wasio na msimamo kuwa tayari kwa lolote ili mradi wafaulu.

Dereva bajaji, teksi
Nani asiyejua kuwa baadhi yao wanaongoza kwa ukware? Kwa kifupi hawa ni miongoni mwa watu ambao mwanaume hatakiwi kukubali ukaribu uliopitiliza kwa wake zao kwani historia inaonesha wengi wao wamekuwa wepesi wa kuomba penzi hasa mazoea yanapovuka mipaka.

Muuza duka
Mama mmoja ambaye mume wake anafanya biashara za kusafiri mikoani alinaswa na mpangaji ambaye kwenye nyumba anayoishi mwanaume huyo ana duka. Baada ya tukio hilo ilibainika mama huyo alikuwa na tabia ya kuchukua vitu dukani hapo na siku hiyo alipotakiwa kulipa alimwambia kimasihara kuwa, yeye hana fedha kama vipi wamalizane kwa njia nyingine.
Kama mwanamke huyu alivyosema, wapo wake za watu ambao wamekuwa wakijirahisi sana kwa wauza duka wakijua itakuwa rahisi kwao kuambulia vitu vidogodogo na fedha. Kwa maana hiyo mkeo si wa kumruhusu kuwa na uhusiano wa karibu sana na wauza duka.

Mganga wa kienyeji
Wapo waganga wa kienyeji ambao ni wasanii tu. Katika hawa wanaodaiwa kuwa wasumbufu kwa wake za watu ni wale wanaojidai kutibu magonjwa ya kinamama.
Ongeza........... Maafisa Mikopo! katika taasis za fedha!
 
sasa hapo mbona kila kundi la watu wanaweza kula mke wa mtu? sababu si kuzoeana bali ni moral decay kwenye jamii!! Kumbuka, hata ukimlinda vipi mkeo, kama anataka kuliwa uroda ataliwa tu. Hivi unajua wanaumwe wakware cku hizi wanataka kula wake za watu zaidi kuliko single ladies? Yaan ni balaa humu duniani. halafu wake zetu nao wanataka kutest vitu nje ya ndoa kwa hiyo ni kama unasukuma mlevi!! Bora usioe kabisa utakuwa salama lakini ukishaoa unaweza kukumbana na Gonjwa bila kujua limefikaje home!!
 
Hakuna formula.

Mke akiwa karibu na mwanaume yeyote yule hata kama ni boss wake uwezekano wa ku cheat ni mkubwa.

Sioni uhusiano kati ya kazi ya mwanaume na tabia ya kutembea na wake za watu...suala hapo ni ukaribu

Nyumba Kubwa, vipi kuhusu hawa vijana wapaka rangi za miguu hawa, mi wananikera sana.ukizingatia maeneo yake ya miguu yako very sentive na miguso.
 
Mada yako umeiweka vizuri Nakshi. Ni kweli hao wote wananyemelea wake za watu.Naomba kuongezea. Kuna mama mmoja mke wa mtu alikuwa anajenga nyumba yake bila mumewe kufahamu. Alikuwa hamlipi fundi anayemjengea. Kila hatua fulani ya ujenzi ikiisha anamwambia fundi wakamalizane kwenye baa fulani ilokuwa jirani na ujenzi. Baa hiyo ilikuwa na gesti. Wakiingia huko fundi analipwa na deni linafutwa! Nyumba ikamalizika kwa dizaini hiyo ya mama.
Swala hapa ni jinsi baadhi ya wanawake (kama ilivyo kwa baadhi ya wanaume) walivyo na low morals! Waukumbuka ule wimbo wa 'kisa cha Mpemba?' Na baadhi ya sisi wanaume tuwe macho. Umeacha sh. 5000 nyumbani asubuhi ukija jioni unatengewa pilau ya kuku wee wabugia tu!

tena naukumbuka sana ule wimbo haya ni baadhi ya mashairi yake:-
Kisa kilichotokea tabata, cha kuchekesha
mpembe kavunja unyumba pale alipoongeza vipimo
cha mchele na sukari kwa mke wa mtu
 
binadamu mwenye akili timamu hachungwi bali anajichunga mwenyewe. usemayo ni kweli kabisa ila huwezi kuwa kauzu kwa watu kuna vitu ni un-kwepable make bila kufahamiana na watu huwez pata vitu. cha muhimu ni kutozidisha mazoea. kwani hujawah ona mtu anajidai kauzu lakin bdo anatoka nje ya ndoa yake, so me naweza kusema kuwa si kwamba mazoea yote huishia kwenye ngono!
 
Wapaka rangi pamoja na wanaowasafisha wanaume kwenye salon wote mi siwafagilii. Haina maana kuwa situmii huduma yao...natumia ila kwa uangalifu bila kuchangia vifaa.

Kinachonishangaza nimeshashuhudia wamama wanaweka miguu kwenye mapaja ya hawa jamaa infront of their husbands...hasa hawa wanaopita kwenye mabaa kutoa hiyo huduma. Mimi siwezi aisee...ntafanya hivyo salon nikijua mume wangu hanioni. Lol....na najijua kuwa mi mgumu hivyo mpaka rangi ataishia ku massage miguu hapati kitu.

Same kwa mume wangu...kuna siku nilimsindikiza akakate nywele...nilichokifanya nilibaki kwenye gari kwa kuwa sitaweza kuvumilia kuona wadada wana mscrub...wadada wa salon walipotoka nje wakakuta nimejaa kwenye gari...nadhani walishangaa kwa nini sikushuka..wale wako kibiashara zaidi kama wauza baa...ukinogewa wanakugeuza buzi.

Hata masalon ya kike ambayo wahudumu ni wanaume ...wanapenda sana kutega wake za watu, wakikuona umekuja na usafiri wa maana wanatamani kukugeuza sugar mummy...nshawasoma sana.

Kikubwa ni kutokuwa na mazoea na hao wote...wewe ni mteja na unalipia service...hakuna story za sijuhi unakaa wapi? Unafanya kazi gani? Sipendi mazoea kabisa yasiyokuwa na sababu.

Ili kujiepusha na vishawishi ni ku stay away from opposite sex. Hakuna dawa zaidi ya hiyo.

Nyumba Kubwa, vipi kuhusu hawa vijana wapaka langi za miguu hawa, mi wananikera sana.ukizingatia maeneo yake ya miguu yako very sentive na miguso.
 
Nyumba Kubwa, vipi kuhusu hawa vijana wapaka langi za miguu hawa, mi wananikera sana.ukizingatia maeneo yake ya miguu yako very sentive na miguso.

Sangarara naomba nikujibu haswaa kabla nyumba kubwa hajajibu,
hawa vijana kwa kweli ni nomaa, kuna siku nilikuwa saloon akaja kijana mpka rangi nikamuomba anisafishe kucha za miguu kisha anipake rangi , alivyonishika tuu miguu kaguna mmh nikamuhuliza kulikoni? akanijibu dada samahani miguu yako mizuri sana tena laini, nikamjibu fanya kazi niliyokutuma sasa basi huko kunisafisha kucha ilikuwa kiuchokozi zaidi ikabidi nisitishe zoezi la kupanga rangi nikamwambia nimepata hudhuru basi rangi, akaondoka .
stori niliyoipata kuhusu mpaka rangi kwamba anachukua wake za watu kupita maelezo kwa ajili ya usafishaji wake miguu na mikono.
ila jamani wanawake tujiheshimu kwa kweli
haya nyumba kubwa karibu.
 
Mbona kuna mkoa fulani baba mkwe kuzaa na mka mwana ni kitu cha kawaida.

Wengine waliyajua madhara mapema ndio maana ni kuna mila zimepiga marufuku kukaa kochi moja na mkweo na ukimuona unapita mbali...

Wale wanaojidai wana act kidhungu ndio kwenye familia unakuta watoto wawili wa mume wawili wa mkwe.

na ipo siku utakuja shangaa zaidi baba akatembea na mkwewe, mke wa mwanae.
 
Jamani naombeni msamaha in advance...inakuwaje mwanaume anakubali mkewe kuwa secretary? Yani navyowaona hawa maboss wetu ..ni ngumu kumesa. SIna maana kuwa ma secretary wote wanatembea na ma boss ila mume anakuwa na amani kweli?
 
Sifanyi kazi ya kumlinda mke wangu na huo muda sina. Naamini ni mtu mzima mwenye utashi na maamuzi sahihi. Ninaamini pia kuwa sikuoa robot au mtoto wa shule ambaye akili hazijakomaa na wala hana utashi. Ila nimeshaweka wazi kuwa msimamo wangu hauna tofauti na ule wa Yesu mnazareti kuwa mambo mengine yote tutasameheana isipokuwa yeye kutafunwa na jamaa mwingine. Kwa hiyo sera yangu kwa hilo ni kuwa atafunwe "at her own risk".
 





Mwalimu
Hapa nazungumzia zaidi walimu wa vyuoni. Baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wanawake kwa kuwaahidi kuwafaulisha kwenye mitihani na wamekuwa wakiwatishia kuwafelisha endapo watawachomolea. Hilo limekuwa likiwafanya baadhi ya wanawake wasio na msimamo kuwa tayari kwa lolote ili mradi wafaulu.



Hapa nakukatalia aisee. Mavyuoni kuna watoto wakali, na walimu wakiamua wanawapata kirahisi sana. Tatizo wamama wanaosoma mavyuoni wanakuwa ovyo sana darasanai, na njia ya kuepuka disco ni kwenda kujichekesha kwa walimu. Sasa ye mwalimu afanyeje... anamaliza mchezo.
 
Back
Top Bottom