Hawa ndio wanaokula mema ya Rais Magufuli

Hawa ndio wanaokula mema ya Rais Magufuli

Uliza wakulima wa Tumbaku ni kilio nchi nzima, tumbaku iko gharan toka mwez wa tano, wanataka wauze hata kwa bei ndogo ili warudishe gharama walizotoa, Wazir wa kilimo sina uhakika kama anaelewa kwa uhakika kuhusu hili
Tumbaku na mazao ya kunde wanaliaje
 
Kuna vijana wanalima Mkonge cha moto wanakipata.Pole usidanganye watu.Mie Mkulima lakini bei ya pembejeo ni moto wa kuotea mbali.
 
Wapiga dili na wavivu ndio wenye kumchukia!
Ww kweli bashite wakulima wamatunda na nyanya wanalia zimoza nakutupwa zimekosa mnunuzi mbaazi inauzwa kilo sh200 kweli ww bashite kabisa sukari ilikuwa inauzwa 1500 sasa ni sh3000
 
Amani itawale.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala..
Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu.

Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa.
Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani.

1. Wamachinga
Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo.
Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote.
Kwa nini wasimpende Magufuli?

2. Wakulima
Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima.
Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!!
Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli??

3. Wafugaji
Kabla ya Rais Magufuli kuwa mfugaji ilikuwa adhabu tosha.
Ukipeleka kuuza Ng'ombe mnadani unakutana na kodi ya kwato na pembe!!

Chini ya Magufuli hizo kodi zote zimefutwa. Sasa wafugaji wanafanya biashara zao kwa raha na kujiongezea kipato.

Pia watu wa vijijini walikuwa wananyanyaswa sana wakienda kwenye huduma za serikali ,lakini sasa hivi wanaheshimika na kuhudumiwa vizuri.

Sasa hutaki wampende Magufuli ili wakupende wewe mtetea mafisadi?

Watetea mafisadi wote wajue kupambana na mtu ambaye siyo Mnafiki inahitaji timing na akili nyingi .

Magufuli siyo mnafiki ,nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi.

Wanasiasa wengi wamezoea kusema nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi.
Nawambieni watapata shida enzi ya Magufuli.

Asante Jakaya Kikwete kwa kutuachia Rais Magufuli mafisadi wanafungasha virago wenyewe na kuiacha Tanzania yetu.
Umeishahau kama mitumba inakaribia kufutwa!
 
Unamsubiri Magufuli akutafutie wateja?
Kwahiyo Wizara ya biashara inafanya nn ktk nchi hii inapewa hela kwaajili ya nn kweli ukiwa ccm lazima uwe mjinga kama rais alivyosema kwa mkuu wa mkoa wa arusha
 
Nilidhani nafasi za u-DC zimeshajazwa zote....naona bado kumbe
 
Hapo kwenye wakulima watu mnaongea shit tu! Unalima alafu unaambiwa uuze hapa hapa kwa gunia 30,000 hadi 40,000 wakati kuna uwezekano wa kupata soko kwa bei nzuri zaidi ya hiyo! Kifupi hajatusaidia kitu sisi wakulima bora angeweka kodi ila angeruhusu kuuza popote mkulima anapopata soko kwa bei nzuri
 
Hapo kwenye wakulima watu mnaongea shit tu! Unalima alafu unaambiwa uuze hapa hapa kwa gunia 30,000 hadi 40,000 wakati kuna uwezekano wa kupata soko kwa bei nzuri zaidi ya hiyo! Kifupi hajatusaidia kitu sisi wakulima bora angeweka kodi ila angeruhusu kuuza popote mkulima anapopata soko kwa bei nzuri
mwaka jana mwezi wa tisa tumeuza mahingi nje kwa debe 10000 kufikia mwezi januar tukaanza kuyanunua hayo mahindi kutoka nje kwa tsh 20000 debe. akili za kuambiwa changanya na za kwako
 
Mkuu,soko la mbaazi liko wapi nikauze zangu? Mwaka huu tumepata pigo kubwa wakulima wa mbaazi. Ni maumivu makali ya hasara kubwa. Mbaazi zimetubwaga na kutupoteza. Maumivu!
Halijarekebishika tu soko la mbaazi???
 
Ongezea na Watu wa Kimara wale waliobomolewa nyumba zao!
 
Wako ware watu wako...wapumbavu sana ....Ndugu wana JF ...hahahaaa haya maspika bwana yanatoa sauti sana
 
u
Mkuu,soko la mbaazi liko wapi nikauze zangu? Mwaka huu tumepata pigo kubwa wakulima wa mbaazi. Ni maumivu makali ya hasara kubwa. Mbaazi zimetubwaga na kutupoteza. Maumivu!
na tani ngapi? na unauza kwa bei gani? ziko wapi?
 
mwaka jana mwezi wa tisa tumeuza mahingi nje kwa debe 10000 kufikia mwezi januar tukaanza kuyanunua hayo mahindi kutoka nje kwa tsh 20000 debe. akili za kuambiwa changanya na za kwako

Akili za nyie msiolima mnazijua wenyewe, sisi tunaowekeza fedha zetu kwenye kilimo tu najua uchungu wake, wewe ulinunua mahindi kwa elfu 20 kwa debe ni kutokana na ujinga wako uliochanganyika na uvivu wa mwili na akili, ninapoweka fedha yangu shamba na Mimi nataka faida kama wafanyabiashara wengine au hufahamu kua kilimo sio huduma?

Kilimo ni biashara Mjomba watu tunawekeza humo na tunataka baada ya kuvuna tupate masoko mazuri ili turudishe fedha zetu zikiwa na faida, binafsi sijauza mahindi yangu mpaka sasa maana siwezi yauza kwa bei ya soko lililopo la sh. 30 elfu mpaka 40 ni hasara kwangu
 
Back
Top Bottom