Hawa ndio wanaokula mema ya Rais Magufuli

Hawa ndio wanaokula mema ya Rais Magufuli

Hizi namba tunasoma bure? Mbona mm sijasikia hata siku moja tunadaiwa ada?
 
Amani itawale.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala..
Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu.

Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa.
Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani.

1. Wamachinga
Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo.
Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote.
Kwa nini wasimpende Magufuli?

2. Wakulima
Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima.
Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!!
Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli??

3. Wafugaji
Kabla ya Rais Magufuli kuwa mfugaji ilikuwa adhabu tosha.
Ukipeleka kuuza Ng'ombe mnadani unakutana na kodi ya kwato na pembe!!

Chini ya Magufuli hizo kodi zote zimefutwa. Sasa wafugaji wanafanya biashara zao kwa raha na kujiongezea kipato.

Pia watu wa vijijini walikuwa wananyanyaswa sana wakienda kwenye huduma za serikali ,lakini sasa hivi wanaheshimika na kuhudumiwa vizuri.

Sasa hutaki wampende Magufuli ili wakupende wewe mtetea mafisadi?

Watetea mafisadi wote wajue kupambana na mtu ambaye siyo Mnafiki inahitaji timing na akili nyingi .

Magufuli siyo mnafiki ,nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi.

Wanasiasa wengi wamezoea kusema nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi.
Nawambieni watapata shida enzi ya Magufuli.

Asante Jakaya Kikwete kwa kutuachia Rais Magufuli mafisadi wanafungasha virago wenyewe na kuiacha Tanzania yetu.
Safi sana bwana Jingajinga bini Mazwazwa
 
Mkuuu akili huna....!!! Hujawahi kufanya biashara yoyote hata kilimo hujui...kaaa kimya..!!
Mmachinga atamuuzia nani kama wateja wake hawana pesa hata wakimruhusu apange bidhaa zake hadi ikulu...!!

Mkulima amenufaika hivi...pembejeo ziko wapi??...bajeti ya mbolea imeongezwa sh.ngapi?? Wapi kuna soko la uhakika hasa mazao ya biashara..!! Mazao ya chakula kila siku yanaporomoka bei!!!?? Unafikiri production cost ikiwa kubwa mkulima ananufahika vipi???

Viazi mbeya wanauza kwa bei ya hasara kila siku wanalalamika kukosa wateja na hii inasababishwa na kudorora kwa uchumi...!!!

Duuuh kuwa mwehu siyo lazima uvue nguo. Juzi tu ulilalamika bei za vyakula zimepanda. Leo zimeshuka unalalamika
 
Wafugaji wasikuckie wanaweza kukuloga jins wanavo pata taabu ya kufukuzwa, rejea maeneo mbalimbalu ya nchi, wakulima wasikusikie hasa wale wa mahindi wamezuiwa kuuza , chunga kauli zako za kuamsha hasira za watuuu
 
Ondoa Wakulima na Wafugaji tatizo unaangalia kwa juu juu tu Wafugaji leo wanaangua Vilio au unamaanisha wenye mifugo 6 na 10 lkn pia mkulima anauza wap hayo mavuno na kwa bei ipi yenye kukudhi gharama zote alizotumiaaaaaa Sio tatizo lako maana unaandika huku ukiwa Sio Mkulima wala Mfugaji
 
Mleta mada ninahakika unakaa kwa shemeji yako kazi yako kutumwa vitafuno, kwenda sokoni na kusindikiza watoto shule hujawahi tafuta ktk kipindi cha jpm ulichoandika ni sawa na zaidi harufu ya mifereji ya vyoo vilivyozibuliwa
 
Huyo unaedai sio mnafki ndo aliahidi milioni 50 kila kijiji tulipomdai akasema yalikua ni maneno ya kampeni tu!
 
Hebu safiri kule kijijini kwa bibi yako afu kaongee hivyo mbele ya wakulima kama hawatakutengua matendegu shwaini
 
Issue ya wamachinga nadhan kuna umuhimu wa kuwatafutia sehemu rasmi waache kusababisha kero barabarani
 
Mkuu,soko la mbaazi liko wapi nikauze zangu? Mwaka huu tumepata pigo kubwa wakulima wa mbaazi. Ni maumivu makali ya hasara kubwa. Mbaazi zimetubwaga na kutupoteza. Maumivu!

Wewe tegemeo laki lilikuwa soko la INDIA, india mwaka jana NA huu wanepata mazao mazuri sana ya mbaazi, mahitaji ya kuagiza mbaazi njee limeshuka. Pia bei ya mbaazi India uko chini sana, bei ya 1kg ilifikia IR 150/- NA leo imeanguka hadi IR 35/-

Serekali ya Magufuli inahisikaje hapo, hata world bank hai wezi kukusaidia hapo. Lima chakula kinacho tumiwa NA waafrica utapata soko kubwa.
 
Amani itawale.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala..
Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu.

Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa.
Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani.

1. Wamachinga
Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo.
Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote.
Kwa nini wasimpende Magufuli?

2. Wakulima
Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima.
Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!!
Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli??

3. Wafugaji
Kabla ya Rais Magufuli kuwa mfugaji ilikuwa adhabu tosha.
Ukipeleka kuuza Ng'ombe mnadani unakutana na kodi ya kwato na pembe!!

Chini ya Magufuli hizo kodi zote zimefutwa. Sasa wafugaji wanafanya biashara zao kwa raha na kujiongezea kipato.

Pia watu wa vijijini walikuwa wananyanyaswa sana wakienda kwenye huduma za serikali ,lakini sasa hivi wanaheshimika na kuhudumiwa vizuri.

Sasa hutaki wampende Magufuli ili wakupende wewe mtetea mafisadi?

Watetea mafisadi wote wajue kupambana na mtu ambaye siyo Mnafiki inahitaji timing na akili nyingi .

Magufuli siyo mnafiki ,nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi.

Wanasiasa wengi wamezoea kusema nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi.
Nawambieni watapata shida enzi ya Magufuli.

Asante Jakaya Kikwete kwa kutuachia Rais Magufuli mafisadi wanafungasha virago wenyewe na kuiacha Tanzania yetu.
Umesahau kuweka mawasiliano.
 
Back
Top Bottom