Hawa ndio wanaokula mema ya Rais Magufuli

Hawa ndio wanaokula mema ya Rais Magufuli

Anaye kula pipi awamu hii ya masolex ni king wa dar tu huo ndiyo ukweli ....
Mambo ya kusema Sijui wakulima,wafugaji,mama ntilie,wamachinga etc that's bllshyt ....
King wa dar ndiyo anapetaaa usawa huuu tena Kuliko hao ma ministers wote

Ova
 
Mda n msema kwel mzur sana, wenye hekma na busara huwa wanakaa kmy kusubr mda, msije kataa vibandko vyenu siku za usoni
 
Sijawahi kuona mtu muongo na mnafiki kama mleta mada. Wamachinga wapi? Wakulima wapi? Na wafugaji wapi? Labda wewe tu na itabidi tukuulize unatokea wapi? Kama ni callmej sawa. Otherwise wengine wote siyo
 
Kati ya hayo uliyotaja hakuna hata moja unalojishughulisha nalo
Na hao aliyowataja hakuna hata mmoja anaingia jamii forum. Siyo kama hawataki la hawana huo ubavu hasa watu wa vijijini wengi wao bado wanaishi maisha ya karne ya 16 hawana umeme maji bado ya kisima viwavi jeshi kwenda mbele. Hospitali zao hazina dawa wala waganga nani anataka kwenda kukaa bush halafu hakuna facilities?
Shule ndiyo mmhhh hao lazima wampende kwani wengine hata redio hawana hawajui nini kinaendelea duniani
 
Mleta uzi huu nafikiri upo dar es salaam kitambo hujui yanayojiri mikoani, na hao machinga unaongelea sijui ni jiji gani. Lakini hakuna shida maana kila mmoja na mtazamo wake, kuna wengine ni wapika data wazuri
 
Sisi wakuluma wa tumbaku hatujauza toka mwezi wa tano na inazidi kuharibika kwenye store, msimu mwingine wa kilimo umefika na hatuna pesa ya kuendeshea kimono, tumepoteza pesa nyingi sana pia halmashauri zimekosa mabilioni ya pesa kupitia ushuru, ulizia Kahuna, Tabora, Katavi, Morogoro, Songea na sehemu zingine wanazolima tumbaku nchini
 
Wenye kazi na shughuli zao halali wamerihika na wanafurahia utendaji mzuri wa serikali. Wanaopiga kelele ni wale mafisadi, wezi, wakwepa kodi na majipu waliokuwa wanalipwa mishahara hewa. Wengine ni waliofoji vyeti vya taaluma.

Serikali ya JPM haihitaji wanyonyaji na wapiga dili. Ni Kazi Tu.
Mbona Bashite amefoji vyeti na anafurahia awamu ya tano!
 
Uliza wakulima wa Tumbaku ni kilio nchi nzima, tumbaku iko gharan toka mwez wa tano, wanataka wauze hata kwa bei ndogo ili warudishe gharama walizotoa, Wazir wa kilimo sina uhakika kama anaelewa kwa uhakika kuhusu hili
 
Amani itawale.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala..
Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu.

Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa.
Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani.

1. Wamachinga
Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo.
Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote.
Kwa nini wasimpende Magufuli?

2. Wakulima
Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima.
Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!!
Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli??

3. Wafugaji
Kabla ya Rais Magufuli kuwa mfugaji ilikuwa adhabu tosha.
Ukipeleka kuuza Ng'ombe mnadani unakutana na kodi ya kwato na pembe!!

Chini ya Magufuli hizo kodi zote zimefutwa. Sasa wafugaji wanafanya biashara zao kwa raha na kujiongezea kipato.

Pia watu wa vijijini walikuwa wananyanyaswa sana wakienda kwenye huduma za serikali ,lakini sasa hivi wanaheshimika na kuhudumiwa vizuri.

Sasa hutaki wampende Magufuli ili wakupende wewe mtetea mafisadi?

Watetea mafisadi wote wajue kupambana na mtu ambaye siyo Mnafiki inahitaji timing na akili nyingi .

Magufuli siyo mnafiki ,nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi.

Wanasiasa wengi wamezoea kusema nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi.
Nawambieni watapata shida enzi ya Magufuli.

Asante Jakaya Kikwete kwa kutuachia Rais Magufuli mafisadi wanafungasha virago wenyewe na kuiacha Tanzania yetu.
tapatalk_1503158930139.jpeg
 
Wenye kazi na shughuli zao halali wamerihika na wanafurahia utendaji mzuri wa serikali. Wanaopiga kelele ni wale mafisadi, wezi, wakwepa kodi na majipu waliokuwa wanalipwa mishahara hewa. Wengine ni waliofoji vyeti vya taaluma.

Serikali ya JPM haihitaji wanyonyaji na wapiga dili. Ni Kazi Tu.
Bashite
 
Namba 2
Hao wakulima wanaouza Mbaazi "Bati" kwa kilo
 
Mkuu,soko la mbaazi liko wapi nikauze zangu? Mwaka huu tumepata pigo kubwa wakulima wa mbaazi. Ni maumivu makali ya hasara kubwa. Mbaazi zimetubwaga na kutupoteza. Maumivu!
Lipo hapahapa kilo 50/-
 
Wenye kazi na shughuli zao halali wamerihika na wanafurahia utendaji mzuri wa serikali. Wanaopiga kelele ni wale mafisadi, wezi, wakwepa kodi na majipu waliokuwa wanalipwa mishahara hewa. Wengine ni waliofoji vyeti vya taaluma.

Serikali ya JPM haihitaji wanyonyaji na wapiga dili. Ni Kazi Tu.
IMG_20171010_101456.jpg
IMG_-lliod6.jpg
 
Mkuu,soko la mbaazi liko wapi nikauze zangu? Mwaka huu tumepata pigo kubwa wakulima wa mbaazi. Ni maumivu makali ya hasara kubwa. Mbaazi zimetubwaga na kutupoteza. Maumivu!
Unalimia mbaazi Na kuuzia kwenye Jukwaa la Siasa la Jamiiforums
 
Back
Top Bottom