KACHINJA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 1,263
- 864
Sio kweli mkuu, ujue izo idara ulizozitaja zinahitaji watu wengi sana lakini pia kila mwaka watu wanastaafu. Je, hao viongozi ambao umewataja wanawatoto wangapi wa kuziba pengo hiliHabari ndugu zangu. Kumekuwa na wimbi kubwa sana la ukosefu wa ajira kwa miaka ya hivi karibun hali ambayo inakatisha tamaa na juhud za kuihangaikia elimu hasa kwa watu wenye kipato cha chini kulinganisha na miaka ya nyuma. Kukosekana kwa nafasi nyingi za ajira ni tatizo ambalo limeanza mwaka 2015/2016 ambapo kimbilio la wengi hasa maskini ktk uwalimu, udaktar na uanajeshi wamekosa ajira. Kimbilio la watanzania hasa wa kipato cha chini ilikuwa ni katk hizo nafasi kwan haikuhitaj rushwa wala kujuana ili upate ajira.
Watu wote waliokuwa wanahitim vyuo vikuu bila kujali ni chuo gan, dini gan, anaitwa nani au ni mtoto wa nani walipataajira kwa pamoja. Kila mtoto aliyejitahid ktk masomo alisomeshwa kwa hali na Mali na huku akipewa majukum angali yupo masomoni kuwa maliza uje utukomboe.
Utukomboe hapa ilikuwa kwanza ni kuwajengea wazaz na kuwasomesha wadogo zako na kubadilisha hali ya maisha kw ujumla. Na haya yote yaliwezekana kwa uhakika wa ajira rasmi kutoka serikalin. Huu ni ukweli usioshaka kuwa hakuna mzazi au mlezi yeyote Yule ambae anajnyima ili msomeshe mtoto kisha mtoto wake akose ajira aanze kuhangaika mtaani kujitaftia vi miamia eti kajiajir kw jambo ambalo linafanya na mtu ambae hata shule ya upili haijui. Ukosefu wa ajira unawatesa sana wazazi maskin waliosomesha kwa shida kulikon hata aliekosa ajira.
Baada ya kuyasema haya mm binafsi naona kuwa tulipofikia au tnakoelekea ajira zote ambazo zilikuwa ndio kimbilio la walala hoi maskini zitakuwa ni za watoto wa watu mashuhuri wenye heshma na vyeo. Yan kuanzia WALIMU, madaktar na wanajeshi watakuwa ni watoto wa mawazir, wabunge madiwan wakuu wa mikoa na wilaya wakurugenzi na mfano wa hao.
Yani tulikofikia mtoto wa maskin kupata ajira itakuwa ni ngumu sana na nilazima uwe na mtu unamjua juu la sivyo utabaki kuwa mzee wa busara mtaani. Nasema yote haya mana mm pia ni muhanga wa hili. Mpak saivi mwaka w 4 huu sina ajira mama kila akiskia tu neno ajira kweny radio anaomba sim anapiga. " mwanangu nimeskia wanatangaza ajira redioni hebu fuarltilia" inaniuma sana. Saivi tulipofikia somesha mwanao na umtafutie ajira na Kama huna nafasi ya kufanya hivyo usipoteze hela zako utakuja kumpa mwanao msongo wa mawazo akiwaza namna ya kukuripa fadhila za jitihada zako za kumpa elimu. Badala yake mtengeneze akiwa kijana mdogo aweze kijitegemea mwenyewe hasa akimaliza elimu ya upili ambayo itamfanya ajitambue na kujisimamia.
Usipo amini maneno yangu chukua mifano michache hapa chini
Viongoz wakuu wote watoto wao wana vyeo vikubwa tu nchini hapa kuanzia wastaafu mpaka waliko madarakan. Hata msiba unaotrend saiv wa mtoto wa mabeyo yule dogo nae alikuwa wa majeshi pia. Sasa wakitoka kwenye mi vyeo mikubw kubwa uko wanarudi kwenye ualimu sasa hapo wee kapuku kama Mimi huna chako labda ukalime nyanya na matikit maji ualimu itakuwa kama manager wa benki na hapo maslahi yataboreshwa na matabaka yatatengenezwa. Tabaka tawala na tawaliwa. Yan maskin atazid kuwa maskin na tajir atazid kuwa tajir.
Kikubwa ni kwamba kutokana na sera ya elimu bure serikali huwa inatumia fedha nyingi sana kama ruzuku mashuleni. Kwa hyo inashidwa kuajili watumishi wengi kuhofia cha kuwalipa. Huko mwazo mambo ya elimu bure hayakuwepo na ndiyo maana ajira zilikuwa za kumwanga.
Cha msingi serikali iangalie hili swala la elimu bure maana linawashinda