Hawa ndio walimu, madaktari na wanajeshi watakaoajiriwa

momara

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
391
500
Habari ndugu zangu. Kumekuwa na wimbi kubwa sana la ukosefu wa ajira kwa miaka ya hivi karibun hali ambayo inakatisha tamaa na juhud za kuihangaikia elimu hasa kwa watu wenye kipato cha chini kulinganisha na miaka ya nyuma. Kukosekana kwa nafasi nyingi za ajira ni tatizo ambalo limeanza mwaka 2015/2016 ambapo kimbilio la wengi hasa maskini ktk uwalimu, udaktar na uanajeshi wamekosa ajira. Kimbilio la watanzania hasa wa kipato cha chini ilikuwa ni katk hizo nafasi kwan haikuhitaj rushwa wala kujuana ili upate ajira.

Watu wote waliokuwa wanahitim vyuo vikuu bila kujali ni chuo gan, dini gan, anaitwa nani au ni mtoto wa nani walipataajira kwa pamoja. Kila mtoto aliyejitahid ktk masomo alisomeshwa kwa hali na Mali na huku akipewa majukum angali yupo masomoni kuwa maliza uje utukomboe.

Utukomboe hapa ilikuwa kwanza ni kuwajengea wazaz na kuwasomesha wadogo zako na kubadilisha hali ya maisha kw ujumla. Na haya yote yaliwezekana kwa uhakika wa ajira rasmi kutoka serikalin. Huu ni ukweli usioshaka kuwa hakuna mzazi au mlezi yeyote Yule ambae anajnyima ili msomeshe mtoto kisha mtoto wake akose ajira aanze kuhangaika mtaani kujitaftia vi miamia eti kajiajir kw jambo ambalo linafanya na mtu ambae hata shule ya upili haijui. Ukosefu wa ajira unawatesa sana wazazi maskin waliosomesha kwa shida kulikon hata aliekosa ajira.

Baada ya kuyasema haya mm binafsi naona kuwa tulipofikia au tnakoelekea ajira zote ambazo zilikuwa ndio kimbilio la walala hoi maskini zitakuwa ni za watoto wa watu mashuhuri wenye heshma na vyeo. Yan kuanzia WALIMU, madaktar na wanajeshi watakuwa ni watoto wa mawazir, wabunge madiwan wakuu wa mikoa na wilaya wakurugenzi na mfano wa hao.

Yani tulikofikia mtoto wa maskin kupata ajira itakuwa ni ngumu sana na nilazima uwe na mtu unamjua juu la sivyo utabaki kuwa mzee wa busara mtaani. Nasema yote haya mana mm pia ni muhanga wa hili. Mpak saivi mwaka w 4 huu sina ajira mama kila akiskia tu neno ajira kweny radio anaomba sim anapiga. " mwanangu nimeskia wanatangaza ajira redioni hebu fuarltilia" inaniuma sana. Saivi tulipofikia somesha mwanao na umtafutie ajira na Kama huna nafasi ya kufanya hivyo usipoteze hela zako utakuja kumpa mwanao msongo wa mawazo akiwaza namna ya kukuripa fadhila za jitihada zako za kumpa elimu. Badala yake mtengeneze akiwa kijana mdogo aweze kijitegemea mwenyewe hasa akimaliza elimu ya upili ambayo itamfanya ajitambue na kujisimamia.

Usipo amini maneno yangu chukua mifano michache hapa chini
Viongoz wakuu wote watoto wao wana vyeo vikubwa tu nchini hapa kuanzia wastaafu mpaka waliko madarakan. Hata msiba unaotrend saiv wa mtoto wa mabeyo yule dogo nae alikuwa wa majeshi pia. Sasa wakitoka kwenye mi vyeo mikubw kubwa uko wanarudi kwenye ualimu sasa hapo wee kapuku kama Mimi huna chako labda ukalime nyanya na matikit maji ualimu itakuwa kama manager wa benki na hapo maslahi yataboreshwa na matabaka yatatengenezwa. Tabaka tawala na tawaliwa. Yan maskin atazid kuwa maskin na tajir atazid kuwa tajir.
 
mputa

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
1,079
2,000
Nilishangaa kusikia yule kijana aliye fariki kwenye ajali ya ndege, mtoto wa mkuu wa majeshi kumbe alikua ameshapata ajira ATCL, na hapo kujuana lazima kupo, inafika wakati hata kijana/ndugu yako akiitwa kwenye interview unajua fika hiyo ni geresha tu kwani kuna ambao wameshaandaliwa
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
7,982

ushawahi kuwaza kuna fairness kwenye ajira?
wewe endelea zako kuuza bamia huko mbutu
 
MASAMILA

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
4,813
2,000
Wazazi wanatakiwa kubadilika sababu sasa sio Zama za mkoloni ambae yeye(Mkoloni) aliweza ajiri wahitimu wote kwa sababu alisomesha Waafrika wachache kwa makusudi

Payroll inatoka kwenye kodi wanazolipa wananchi which means Serikali haina na haitakuja kuwa na uwezo wa kuajiri wahitimu wote

Wazazi kwa sasa walitakiwa kuangalia kuwapeleka watoto wao kwenye vyuo vya taaluma ya ufundi stadi (Vocational training education)

Leo hii nchi yetu haina watu waliosomea ufundi wa matrekta, mitambo ya ujenzi na hata magari mafundi waliosomea ni wachache waliopo ni wababaishaji tu lakini wazazi wamekomaa na Taaluma za white-collar jobs
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
7,982
2,000
Nilishangaa kusikia yule kijana aliye fariki kwenye ajali ya ndege, mtoto wa mkuu wa majeshi kumbe alikua ameshapata ajira ATCL, na hapo kujuana lazima kupo, inafika wakati hata kijana/ndugu yako akiitwa kwenye interview unajua fika hiyo ni geresha tu kwani kuna ambao wameshaandaliwa
Kiongozi wa "wanyonge "anasema kiswahili ni lugha kubwa sana, hakuna haja ya kingereza, jiulize tu alafu mtu kama ni mnafki utajijibu mwenyewe, je, yule marehemu kasoma shule za kata, je, amesomea urubani kwa kiswahili?

majibu watag MATAGA WOTE, MWIGULU NA KIBAJAJI
 
Yan inauma sana mkuu. Watu wanaandaliwa na kazi zao zipo Tatar ni kuhitim tu basi
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,803
2,000
Pole sana mkuu, nakumbuka kuna kipindi nasoma chuo mwaka 2012 kwenda kufanya field kupata nafasi tu ilikuwa ni kazi kubwa hadi nikaunganishiwa na mtu, just imagine field unaunganishiwa na mtu.!,

Nikaanza kujiandaa kisaikolojia maana ajira sijui ingekuaje
Ila nilipata tu kazi baada ya miezi 2 kampuni binafsi ya mtu aliyekuwa anafahamiana na mzee kitambo, baada ya mwaka nikapata kazi kampuni nyingine, nikitafakari naona kama nilikuwa na bahati sana maana kuna wengine hawajapata kazi hadi muda huu na walimazliza nyuma yangu
Kuna watu weng wana depression sana wanatamani hata kujiua
 
KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,503
2,000
Kuna siku nilikuwa nimeenda sehemu fulani nilipata shavu la ajira maana nilipigiwa simu na ninayejuana naye niende kupeleka vitu vyangu kwa ajili ya ajira.
kwakuwa ananafasi kidogo nilipofika nilikaa naye ofisini kwake wakaingia na watu wengine kama wanne jambo la kushangaza kulikuwa na nafsi kama zawatu 150 wanatakiwa,
ila hadi nafika mimi karibia nafasi 100 zimejazwa tayari hapo hata tangazo bado halijatoka kwamba kuna watu wanatakiwa kwa ajili ya jambo fulani.

tumetofautiana nlakini nilijisikia vibaya sana ikabidi nimwambie mi nimekua hapo kumwambia sitaweza kufanya hiyo issue kuna issue nyingine nimepata nitaenda mkoa,
alihuzunika sana sababu ilikuwa ni issue inafanyika kwa miezi mitatu then kila siku mtu unaondoka na 40

Niliamua kuahirisha apate mwingine sababu tayari nilikuw ana goli langu naweza jisongesha kimaisha,

Ila inauma sana hasa huko serikalini ajira hadi inatangazwa basi jua wao tayari wamekwisha kujaza watu wao then mnaachiwa nafasi 5 katika 100 na mnaedna interview watu karibia 400
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
10,169
2,000
Wamepata malipo ya dhulma
Nilishangaa kusikia yule kijana aliye fariki kwenye ajali ya ndege, mtoto wa mkuu wa majeshi kumbe alikua ameshapata ajira ATCL, na hapo kujuana lazima kupo, inafika wakati hata kijana/ndugu yako akiitwa kwenye interview unajua fika hiyo ni geresha tu kwani kuna ambao wameshaandaliwa
 
Rodrigo Moreno

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
638
1,000
Habari ndugu zangu. Kumekuwa na wimbi kubwa sana la ukosefu wa ajira kwa miaka ya hivi karibun hali ambayo inakatisha tamaa na juhud za kuihangaikia elimu hasa kwa watu wenye kipato cha chini kulinganisha na miaka ya nyuma. Kukosekana kwa nafasi nyingi za ajira ni tatizo ambalo limeanza mwaka 2015/2016 ambapo kimbilio la wengi hasa maskini ktk uwalimu, udaktar na uanajeshi wamekosa ajira. Kimbilio la watanzania hasa wa kipato cha chini ilikuwa ni katk hizo nafasi kwan haikuhitaj rushwa wala kujuana ili upate ajira.

Watu wote waliokuwa wanahitim vyuo vikuu bila kujali ni chuo gan, dini gan, anaitwa nani au ni mtoto wa nani walipataajira kwa pamoja. Kila mtoto aliyejitahid ktk masomo alisomeshwa kwa hali na Mali na huku akipewa majukum angali yupo masomoni kuwa maliza uje utukomboe.

Utukomboe hapa ilikuwa kwanza ni kuwajengea wazaz na kuwasomesha wadogo zako na kubadilisha hali ya maisha kw ujumla. Na haya yote yaliwezekana kwa uhakika wa ajira rasmi kutoka serikalin. Huu ni ukweli usioshaka kuwa hakuna mzazi au mlezi yeyote Yule ambae anajnyima ili msomeshe mtoto kisha mtoto wake akose ajira aanze kuhangaika mtaani kujitaftia vi miamia eti kajiajir kw jambo ambalo linafanya na mtu ambae hata shule ya upili haijui. Ukosefu wa ajira unawatesa sana wazazi maskin waliosomesha kwa shida kulikon hata aliekosa ajira.

Baada ya kuyasema haya mm binafsi naona kuwa tulipofikia au tnakoelekea ajira zote ambazo zilikuwa ndio kimbilio la walala hoi maskini zitakuwa ni za watoto wa watu mashuhuri wenye heshma na vyeo. Yan kuanzia WALIMU, madaktar na wanajeshi watakuwa ni watoto wa mawazir, wabunge madiwan wakuu wa mikoa na wilaya wakurugenzi na mfano wa hao.

Yani tulikofikia mtoto wa maskin kupata ajira itakuwa ni ngumu sana na nilazima uwe na mtu unamjua juu la sivyo utabaki kuwa mzee wa busara mtaani. Nasema yote haya mana mm pia ni muhanga wa hili. Mpak saivi mwaka w 4 huu sina ajira mama kila akiskia tu neno ajira kweny radio anaomba sim anapiga. " mwanangu nimeskia wanatangaza ajira redioni hebu fuarltilia" inaniuma sana. Saivi tulipofikia somesha mwanao na umtafutie ajira na Kama huna nafasi ya kufanya hivyo usipoteze hela zako utakuja kumpa mwanao msongo wa mawazo akiwaza namna ya kukuripa fadhila za jitihada zako za kumpa elimu. Badala yake mtengeneze akiwa kijana mdogo aweze kijitegemea mwenyewe hasa akimaliza elimu ya upili ambayo itamfanya ajitambue na kujisimamia.

Usipo amini maneno yangu chukua mifano michache hapa chini
Viongoz wakuu wote watoto wao wana vyeo vikubwa tu nchini hapa kuanzia wastaafu mpaka waliko madarakan. Hata msiba unaotrend saiv wa mtoto wa mabeyo yule dogo nae alikuwa wa majeshi pia. Sasa wakitoka kwenye mi vyeo mikubw kubwa uko wanarudi kwenye ualimu sasa hapo wee kapuku kama Mimi huna chako labda ukalime nyanya na matikit maji ualimu itakuwa kama manager wa benki na hapo maslahi yataboreshwa na matabaka yatatengenezwa. Tabaka tawala na tawaliwa. Yan maskin atazid kuwa maskin na tajir atazid kuwa tajir.
Kweli kabisa unachosema ..kujitegemea muhimu ..ukisoma kitabu cha rich dad poor dad kinaongelea mtoto kujengewa akili ya kujitegemea na ku make money mapema
 
Rodrigo Moreno

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
638
1,000
Kiongozi wa "wanyonge "anasema kiswahili ni lugha kubwa sana, hakuna haja ya kingereza, jiulize tu alafu mtu kama ni mnafki utajijibu mwenyewe, je, yule marehemu kasoma shule za kata, je, amesomea urubani kwa kiswahili?

majibu watag MATAGA WOTE, MWIGULU NA KIBAJAJI
Inashangaza kwa kweli
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,816
2,000
nimesomea ualimu na nafanya kazi ya ualimu lakini sijaona mtoto wa tajiri au kigogo ni mwalimu. mimi sijaona jamani. na walimu wengi ni masikini sana kwa sababu ya historia za kimasikini.

ova
Ni wakati sasa wa kuutumia huo ualimu kama daraja tu kama walivyofanya akina Jenista Mhagama, Magufuli, Majaliwa, na wengineo wengi, badala ya kazi. Ukiutumia kama kazi, basi jiandae tu kufa maskini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom