Gwalihenzi
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 5,125
- 1,300
Mkuu Mkandara. asante sana kwa taarifa nzuri na mtazamo wako juu ya maswala haya. Tofauti kubwa kati yangu mimi na wewe ni kwamba mimi siamini uwepo wa Mungu! na kama angekuwepo basi asingekuwa huyo anaye elezwa kwenye vitabu hivi vinavyomsimulia kwani huyu wa kwenye vitabu amekuwa "personfied" mno mpaka anapoteza umungu wake!.Mkuu kwanza shukran kwa kuuliza japo sidhani kama unataka kuelemika au unauliza tu kishabiki maana hata Wakristu wanagombana na nadhani wana madhehebu mengi kuliko Waislaam..
Tatizo la dini zetu sote ni moja tu, pale Culture za wahusika zinapoingizwa ktk imani. Iwe kutetea mila na desturi zao kwa sababu hazikuzungumziwa ktk Kuruan au Biblia. Hivyo basi Uislaam hauna tofauti sana na Ukristu pale mila na desturi zinapochanganywa na imani ya dini. Mungu wa Waislaam ni yule yule wa Wakristu isipokuwa huyu kwa Waislaam hakuzaa wala kuzaliwa, wala hana mfano na alitakalo liwe linakuwa.
Na sijui kama unafahamu ya kwamba Mtume Muhammad (S.A.W)alipotaka kuhubiri dini mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa mkewe kisha Padre mmoja kipofu ambaye ndiye alimhakikishia kuwa ujumbe alokuwa nao sii wake yeye bali wa Mwenyezi Mungu, hivyo nenda kawatangazie watu wako.
Na kuhusu Udini nchini, kwa nini usiishe ikiwa sisi tumeweza kuishi kwa miaka 27 ya Nyerere pasipo Udini?..Kubadilisha tu mfumo wa elimu na Afya udini huoo unachipuka..
Lakini hoja sio hiyo kwani la msingi mimi naheshimu imani za watu ikiwa pamoja na ya kwako. Kwa utofauti mkubwa wa mitazamo kama ilivyo sasa hivi kati ya wanaopambana na mfumo "kristo" hata kama MoU ikaondoka leo, bado tatizo litabaki palepale kwani mpaka sasa kuna watu wanaamini kabisa kuwa mfumo huo uliwekwa na Nyerere! wakati wewe unasema wakati wa Nyerere tuliishi bila udini.
Kuna watu wanaamini adui yao ni ukristo,wengine wanaamini adui yao ni uislam unaokumbatia ughaidi! Kwa watumishi wa serikali wanaogopa hata kutaja majina yao ya kwanza kwa kuogopa wasije wakajulikana dini zao na kwahiyo wakapata madhara!
Mkuu wangu Mkandara, naamini kuna kila sababu kwa taifa kukaa na kuitisha mjadala wa ufafanuzi wa nini maana ya mfumo kristo na namna ya kuuvunja mfumo huu baada ya kupata muafaka na makubaliano ya maana halisi ya mfumo kristo kama kweli upo.