Hawa Ndio Mawaziri wa JK; Waziri Mwinyi asema kwa sasa Madaktari bingwa si muhimu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa Ndio Mawaziri wa JK; Waziri Mwinyi asema kwa sasa Madaktari bingwa si muhimu!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Aug 19, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Sasa napata sababu kwa nini serikali haishtuki hata madaktari wakigoma, na pia napata maana ya kauli ya Mizengo Pinda ya Liwalo na Liwe.

  Waziri mwenye dhamana ya afya Hussein Mwinyi akihojiwa BBC leo asubuhi na mtangazaji wa kipindi cha haba na haba Noel Mwakalindile ambaye alitaka kujua kauli ya serikali juu ya upungufu wa madaktari bingwa, waziri akasema kwa sasa focus yao kubwa ni kusomesha wataalamu wa afya wa ngazi ya cheti na diploma kwa kuwa wao ndio wanahitajika zaidi. Amesema kusomesha daktari bingwa ni gharama kubwa kwani daktari bingwa anasoma miaka minne mpaka mitano. Kwanza huu ni uzushi, vyuo vyote tanzania madaktari bingwa wa fani zote wanasoma kwa miaka mitatu tu, isipokuwa KCMC ambako wanasoma kwa miaka minne. Hakuna hata chuo kimoja ambacho daktari bingwa anasoma kwa miaka mitano. Hii inanipa wasiwasi kuona kuwa waziri wetu hajui hata madaktari bingwa wanasoma miaka mingapi, Je waziri wa aina hii anawezaje kutuambia anajua gharama ya kumsomesha huyu daktari bingwa?

  Hivi kweli huduma bora za afya Tanzania zitaimarika kwa kusomesha maafisa tabibu? Hii serikali inayojali afya ya watu wake inawezaje kweli kuona gharama kusomesha madaktari bingwa na badala yake kusomesha maafisa tabibu. Au inatumia ujinga wa watanzania kwamba mtu yeyote anaevaa koti jeupe ni daktari na hivyo wananchi watajua serikali yao imewapelekea madaktari wakati ni maafisa tabibu ambao tiba yao ni ya huduma ya kwanza?

  Nchini kenya kwa sasa madaktari bingwa wako katika ngazi ya hospitali ya wilaya, na wanamkakati wa kuhakikisha kwamba kila mtu anatibiwa na daktari bingwa ili apate tiba ya uhakika na hivyo afya yake kuboreka. Kwetu hata hospitali za rufaa hazina madaktari bingwa wa kutosha achana na hospitali za mikoa ambazo zenye bahati zina bingwa mmoja tu, na tunawaza kuongeza maafisa tabibu. Hivi kwa nini nchi hii badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma?

  No wonder mwaka jana walipunguza budget ya kusomesha madaktari bingwa na hata wale waliopata udahili walikosa udhamini, nilijua serikali haina pesa kumbe kwa mtazamo wao daktari bingwa si muhimu. Namuomba Hussein Mwinyi akiumwa awe wa kwanza kwenda kwa afisa tabibu kutibiwa aone kama hatapewa ppf injection hata kama ana malaria. Waziri Mwinyi ufikiri kwanza kabla ya kukejeli watanzania.

  Naomba kuwakilisha.
   
 2. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawajali afya ya mwananchi wa kawaida, wao wanatibiwa nje ya nchi,
   
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Hii ndio serikali inayo jali maslahi yake kuliko ya wananchi.
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Lakini hili tumelichochea watanzania wenyewe, kwani hatukuonyesha hisia zetu halisi pale madaktari walipogoma. Nafikiri wao hawawahitaji Madaktari bingwa kwani Apollo wapo wa kutosha.
   
 5. K

  Kiyoya JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  "Ma Dr. Mnajua haki zenu yaan mna shitak had UN hii haikubiliki" Kwa wagonjwa wao wanataka kupata nafuu tu na sio kupona!
   
 6. a

  adolay JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280

  Mkuu Lymo

  Hili lina mwisho wake japo si leo wala kesho.

  Ni matokeo ya kurithishana madaraka, huon kule mjengon? Akina malima, akina kawawa, mwinyi, akina makamba, akina karume na kwa nje kwenye makampun akina mkapa, akina riziwan, nk.

  Kupeana madaraka kwa kujuana hushusha sana nidham ya kazi maana nikubebana kwa kwenda mbele hatakama nikwakuiangamiza inchi.

  Watanzania wa jana sio wa leo ni suala la muda tu.
   
 7. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Dah! siku yangu imeshaharibika
   
 8. T

  TROJUN Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina hakika kama ni kweli wazir anafahamu hata huyo ghalama ya kumsomesha huyo bingwa fahamu haya ndo matatizo ya kupeana nafasi katika uongozi kwa kuzingatia ujamaa zaidi badala ya utendaji na uwezo zaidi matokeo yake mwisho wa siku ndo tunapata wapokea mishahara wasio na faida kama hawa labda kama hawa na kama hajui vitu vya kawaida kama hivyo je atajuaje vile vya ndani?
   
 9. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  mwinyi ni daktar bingwa aliyesomea ugiriki..unfortunantly he z not accustomed with local figures(fees..etc)bt he knwz kusomesha dr bingwa its too expensive bcoz yeye ni dr bingwa..
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuitwa jina la Ibilisi is an abomination, ushindwe kwa Jina La Yesu.
   
 11. a

  artorius JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi sishangai kama mh.mbunge margaret sitta akichangia hotuba ya wizara ya afya alisema "kuwe na crash program kwa vijana waliomaliza form 4 na 6 wakatibu malaria na diarrhoea vijijini".Ndio maana wakenya waliamisha wale majeruhi fasta pale MNH
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndio serikali ya JK...totally disconnected na wananchi. Viongozi wanaongea anyhow wanatoa maamuzi kufuatana na mawazo yao binafsi...hakuna kuwajibika kwa kauli wa matendo yao.
   
 13. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kumbe ujumbe wako mzuri lakini unaanza tena na Mkuu, nawe hee!
   
 14. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndo yale yale, kwamba hutaki kuthamini watu wanaofanya wa chini wawepo. Kwa kiasi kikubwa madaktari bingwa ndio husomesha hawa wa shahada (hasa interns). Hii haina utofauti na dharau ya Jk kwa walimu mwaka 2010, maana kwa kufanya vile alidharau wengi.
   
 15. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,482
  Trophy Points: 280
  viongozi aina ya Mwinyi ni janga la taifa, tatizo wenyewe hawaishi kama watanzania wanajiona miungu watu.!
   
 16. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kwa attitude ya namna hii nategemea yule mtoto wa mkuu wa kaya anayesomea udaktari bingwa wa meno kule uk atafutiwa udhamini wa serikali.
   
 17. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mmmh nimekusoma, kumbe wanatujua. Tanzania hatuthaminiwi kweli, unaweza anza kulia.
  Now I can trust my own saying that the progressive decline of leaders with high IQs leads to progressive increase in partial professionals.
   
 18. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Sioni ajabu kwa mwinyi kusema hayo. hata kwenye milipuko ya mabomu alikuwa analeta mizaha!
   
 19. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mzanzibar aliyeshika wizara isiyo ya muungano.
   
 20. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,004
  Trophy Points: 280
  'SUBIRI NA TUTAONA'....Hayo ni maneno ya mzee mmoja kijijini kwetu aliyoyasema wakati kijana mdogo wa miaka 10 alipopewa zawadi ya baiskeli mpya aina ya Swala ikiwa ni baiskeli ya pili kumilikiwa na mwanakijiji enzi hizo.
  Siku tano baada ya kijana huyo kupata zawadi hiyo alipatwa na mauti yaliyotokana na ajali ya baiskeli hiyo, hakufundishwa sehemu zilipo breki za baiskeli!
  Wana jf subiri muone maafa ya hao half cooked nurses, clinician,nk. UPE ya afya ni mbaya sana.
   
Loading...