Hawa Ndio Mawaziri wa JK; Waziri Mwinyi asema kwa sasa Madaktari bingwa si muhimu!!!

Sasa napata sababu kwa nini serikali haishtuki hata madaktari wakigoma, na pia napata maana ya kauli ya Mizengo Pinda ya Liwalo na Liwe.

Waziri mwenye dhamana ya afya Hussein Mwinyi akihojiwa BBC leo asubuhi na mtangazaji wa kipindi cha haba na haba Noel Mwakalindile ambaye alitaka kujua kauli ya serikali juu ya upungufu wa madaktari bingwa, waziri akasema kwa sasa focus yao kubwa ni kusomesha wataalamu wa afya wa ngazi ya cheti na diploma kwa kuwa wao ndio wanahitajika zaidi. Amesema kusomesha daktari bingwa ni gharama kubwa kwani daktari bingwa anasoma miaka minne mpaka mitano. Kwanza huu ni uzushi, vyuo vyote tanzania madaktari bingwa wa fani zote wanasoma kwa miaka mitatu tu, isipokuwa KCMC ambako wanasoma kwa miaka minne. Hakuna hata chuo kimoja ambacho daktari bingwa anasoma kwa miaka mitano. Hii inanipa wasiwasi kuona kuwa waziri wetu hajui hata madaktari bingwa wanasoma miaka mingapi, Je waziri wa aina hii anawezaje kutuambia anajua gharama ya kumsomesha huyu daktari bingwa?

Hivi kweli huduma bora za afya Tanzania zitaimarika kwa kusomesha maafisa tabibu? Hii serikali inayojali afya ya watu wake inawezaje kweli kuona gharama kusomesha madaktari bingwa na badala yake kusomesha maafisa tabibu. Au inatumia ujinga wa watanzania kwamba mtu yeyote anaevaa koti jeupe ni daktari na hivyo wananchi watajua serikali yao imewapelekea madaktari wakati ni maafisa tabibu ambao tiba yao ni ya huduma ya kwanza?

Nchini kenya kwa sasa madaktari bingwa wako katika ngazi ya hospitali ya wilaya, na wanamkakati wa kuhakikisha kwamba kila mtu anatibiwa na daktari bingwa ili apate tiba ya uhakika na hivyo afya yake kuboreka. Kwetu hata hospitali za rufaa hazina madaktari bingwa wa kutosha achana na hospitali za mikoa ambazo zenye bahati zina bingwa mmoja tu, na tunawaza kuongeza maafisa tabibu. Hivi kwa nini nchi hii badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma?

No wonder mwaka jana walipunguza budget ya kusomesha madaktari bingwa na hata wale waliopata udahili walikosa udhamini, nilijua serikali haina pesa kumbe kwa mtazamo wao daktari bingwa si muhimu. Namuomba Hussein Mwinyi akiumwa awe wa kwanza kwenda kwa afisa tabibu kutibiwa aone kama hatapewa ppf injection hata kama ana malaria. Waziri Mwinyi ufikiri kwanza kabla ya kukejeli watanzania.

Naomba kuwakilisha.

HIvi kweli kasema hvyo ua umemwelewa hivyo?
Kama kasema hivyo basi yale ninayofikiria juu yake ni sahihi.
 
Sasa napata sababu kwa nini serikali haishtuki hata madaktari wakigoma, na pia napata maana ya kauli ya Mizengo Pinda ya Liwalo na Liwe.

Waziri mwenye dhamana ya afya Hussein Mwinyi akihojiwa BBC leo asubuhi na mtangazaji wa kipindi cha haba na haba Noel Mwakalindile ambaye alitaka kujua kauli ya serikali juu ya

upungufu wa madaktari bingwa, waziri akasema kwa sasa focus yao kubwa ni kusomesha wataalamu wa afya wa ngazi ya cheti na diploma kwa kuwa wao ndio wanahitajika zaidi. Amesema kusomesha daktari bingwa ni gharama kubwa kwani daktari bingwa anasoma miaka minne mpaka mitano. Kwanza huu ni uzushi, vyuo vyote tanzania madaktari bingwa wa fani zote wanasoma kwa miaka mitatu tu, isipokuwa KCMC ambako wanasoma kwa miaka minne. Hakuna hata chuo kimoja ambacho daktari bingwa anasoma kwa miaka mitano. Hii inanipa wasiwasi kuona kuwa waziri wetu hajui hata madaktari bingwa wanasoma miaka mingapi, Je waziri wa aina hii anawezaje kutuambia anajua gharama ya kumsomesha huyu daktari bingwa?

Mimi kwa maoni yangu sidhani kama amekosea sana kwani huwezi kuanza kuongela mambo ya madaktari unaowaita bingwa kama huku chini hata hakujatengemaa, hao madaktari wa cheti na Diploma ndio mwokozi wa Watanzania wengi waishio vijijini ambao ni zaidi ya 80% kwa hiyo naamini kama Serikali ikihakikisha wanapata elimu bora watasaidia sana wakati tunaanza kujipanga na hao madaktari unaowaita bingwa.

Mimi nafikiri wewe unaishi mjini tena mji mkubwa na ndio maana unaongelea madaktari unaowaita bingwa kwamba unataka specialist wa kitu fulani wakati watz wengi wanataka tu hata mtu wakuweza kuwapima malaria vizuri hayo mambo ya mafigo na maini ni mbali sana na huwezi ukafika huko kama haujakamilisha hapa chini na kati kati kwanza kwa maoni yangu mimi pia wangeenda mbali zaidi na kutialia mkazo wakunga na kuwafundisha vizuri kabisa na huko vijijini wangeokoa maisha ya mama na watoto wengi sana!
 
Bado uko mbali sana na reality ndugu yangu, hawa matabibu wanatoa first aid, hatuwezi kuwa tunaendelea kutoa first aid kwenye karne hii, hawana uwezo wa kuokoa maisha ya mama endapo mama atashindwa kujifungua kwa kudra za mwenyezi Mungu, hawana uwezo wa kuokoa maisha ya mtoto akiwa na complicated illness.

Ningemwelewa Waziri kama angekuwa anaongeza idadi ya medical officers (MD) na sio hawa clinical officers, hapa ni kufanyia majaribio afya za watanzania. kama kweli wanauwezo mzuri wa kutibu akatibiwe yeye kwanza na familia yake kwa hawa watabibu. Sio kwa kuwa viongozi wana uwezo wa kutibiwa na wataalam wazuri, wananchi wawasubject kwa watu wasio na taaluma ya kutosha, this is not fair by any standards. Sisemi mabingwa wawepo mpaka vijijini lakini angalau basi wale assistant medical officers na sio kuendelea kuwaamini clinical officers kwenye karne hii.
 
HIvi kweli kasema hvyo ua umemwelewa hivyo?
Kama kasema hivyo basi yale ninayofikiria juu yake ni sahihi.
Ningekuwa na uwezo ningemrekodi ndugu yangu, nadhani hivyo unavyomfikiria ndio hivyo. Nimeshtuka sana aliposema kusomesha mabingwa ni ghali na kwamba watajikita kwenye kusomesha wataalamu wa ngazi za cheti na diploma, this is insane!!
 
Tulieni tu, mnalalamika nini, mliingiza ushabiki wa Uislamu na Ukristo kwenye uongozi wa Nchi sasa yanatutokea puani. Mara Dr Slaa Padri, Mara Cdm Cha Wakristo, acha watekeleze sera yao, 2015 tutajua cha kufanya.
 
mwinyi ni daktar bingwa aliyesomea ugiriki..unfortunantly he z not accustomed with local figures(fees..etc)bt he knwz kusomesha dr bingwa its too expensive bcoz yeye ni dr bingwa..

nilikuwa nasikia ma lucifer ni *******, sasa ndo naamisha kwako!
 
Wakiambiwa Serikali ya CCM ina "nguvu kidogo", wanalalamika eti wanadhalilishwa. Kwa kauli hii ya Waziri serikali chini ya CCM utashidwaje kuhalalisha upungufu wa nguvu za CCM.
 
Ndo yale yale, kwamba hutaki kuthamini watu wanaofanya wa chini wawepo. Kwa kiasi kikubwa madaktari bingwa ndio husomesha hawa wa shahada (hasa interns). Hii haina utofauti na dharau ya Jk kwa walimu mwaka 2010, maana kwa kufanya vile alidharau wengi.

nilishajiuliza why did i go to medical school? Mpaka leo sijapata jibu! Mpaka leo washkaji zangu walienda wildlife wako tanapa wanapiga pesa ndefu na wanafurahia kazi hata kama wanakaa porini. Mi nimebaki na stress za kufiwa na wagonjwa, kudharauliwa, kulinganishwa na clinical officers! Yaani ni tabu tupu
 
Ningekuwa na uwezo ningemrekodi ndugu yangu, nadhani hivyo unavyomfikiria ndio hivyo. Nimeshtuka sana aliposema kusomesha mabingwa ni ghali na kwamba watajikita kwenye kusomesha wataalamu wa ngazi za cheti na diploma, this is insane!!

Asante mkuu, nadhani wanataka nguvu ya kuwatawala maana hawatakua na say kama madaktari bingwa.
 
Huyu nae si ni daktari, halafu hajui hata madaktari bingwa wanasoma kwa muda gani. Kazi kweli kweli
 
yale yale ya jk, alipohojiwa na BBC 'kwa nini tz ni maskini?' jk alijibu kuwa hata yeye hajui sababu, hivyo sishangai kusikia haya ya mteule wake kwani kama yeye(jk) hajui uwezekano wa kumteua asiyejua ni mkubwa sana
 
Unategemea nini kutoka kwa Mwinyi ambaye siyo bingwa na MD yake ni questionable??? Hivi alisoma wapi/nchi gani vile???

Alichokisemma ni wivu tu!!
 
Hawa jamaa kuna siku watawaokota wasukuma mikokoteni pale kariakoo sokoni na kuwavalisha makoti meupe na kuwaita madaktari. Subirini muone.
 
Basi, hauna jipya?

Liwalo na Liwe! kwi kwi kwi teh teh teh!

Ulimboka hajambo?
 
Back
Top Bottom