Hawa ndio Chama cha Mapinduzi...

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Salamu wanajamvi,

Leo napenda nizungumzie jambo moja ambalo elimu ya vitabuni imeshindwa kumkomboa Mwafrika miaka na miaka. Kuna wakati unaweza ukadhani tumelogwa na hatujitambui kabisa.

Chama cha mapinduzi kupitia KATIBU mkuu wao wanawaomba watanzania tuiamini serikali yao chini ya Rais Samia kuwa wana nia njema katika hili suala la bandari ya kwamba wana nia njema.

MIMI NASEMA CCM NA SERIKALI YAO HAWAAMINIKI HATA KIDOGO. Kwanini? Tufuatane kidogo kidogo hadi mwisho tutaelewana.

Siku za hivi karibuni CCM na serikali yao hawaaminiki kwasababu wametanguliza mbele maslahi binafsi kuliko maslahi ya Nchi.

Mheshimiwa Magufuli alipo ingia madarakani aliwaondoa wakuu wa wilaya karibu asilimia 70 na kuteua wengine wapya. Akawaondoa Wakurugenzi wa Halmashauri zaidi ya 120 na kuteua wengine wapya kujaza nafasi zao. Vivyo hivyo kwa ma DAS aliwaondoa wa zamani karibu wote na kuwateua wengine kujaza nafasi zao.

Fikiria chama ni kile kile lakini anafanya mabadiko makubwa hivi siyo kwasababu masilahi makubwa ya Nchi ila wana lenga kuwaweka watu wao.

Rais Samia na yeye juzi juzi akaja na mkeka mpyaa wa Wa kuu wa Wilaya na ma DAS, Amewaondoa wa zamani wengi tu siyo kwa udhaifu wa kiutendaji, bali nia ni kuwaweka watu wao ! Wana angalia maslahi binafsi.

Sasa, Kwenye hili sakata la bandari ukifikiria kwa undani unaona nia ovu ama ya Rais Samia yeye binafsi au Chama cha mapinduzi wakilenga kujipatia fedha wao binafsi badala ya serikali.

Kwanini?

Uwekezaji sawa, wote tunapenda lakini siyo kwa namna amba Samia na serikali yake wamefanya. Angalia mapungufu haya ndio utajua nia ovu waliyo kuwa nayo toka Mwanzo.

Kama kweli hawakulenga kujinufaisha binafsi kwanini mchakato haukufuata utaratibu wa kuserikali na Kimataifa Wa kumpata mwekezaji mwenye sifa?

Kwanini wameitenga bodi ya wakurugenzi badala yake wakamtumia mtu nje kabisa ya bodi tena bila idhini ya bodi kimaandishi au kuonesha bodi ya wakurugenzi ilikaa na kumteua yule Mwanasheria kushughulikia mkataba kwaniaba ya bodi?

Kama jambo lenyewe ni jema kwanini wanatumia waandishi wa habari tena kwa kuwahonga kulazimisha watanzania waukubali uwekezaji wa huyu Mwarabu?

Jambo jema hujiuza lenyewe, ila hili lina ukakasi tena mkubwa.

Kwahiyo, binafsi nasema CCMna Rais Samia kwa hili hawaaminiki na hatuta waamini hata kidogo.

Naunga mkono mtu aliye sema kama kuna fedha wamekula wazitapike.
 
Umenena vyema mkuu 'JERUSALEM'.

Hii "nia njema" ina uovu ndani yake, sasa sijui itakuwaje nia njema?

Hawa watu ni kama wanadharau uwezo wa waTanzania kufikiri.
 
Huyu bibi alikuwa anaelekea kujijengea heshima lakini kwa huu mkataba wa kipumbavu amejitumbukiza kwenye kinyesi.

Wazalendo wengi walijaribu kumsaidia lakini wapi... Mpaka hapa alipofika hasaidiki tena.

Akitaka salama basi ajiuzulu awaachie wengine. Akishupaza shingo, basi asubiri nchi iingie kwenye machafuko afurushwe akaishi uhamishoni kwa wajomba zake.
 
Mpuuzi na mjinga ndie atakaye iamini CCM, sisiem sio chama cha siasa kilishatoka huko kitambo, kimebaki kua chama dola chenye kikundi cha mafisadi, walaghai, wezi na wala rushwa wasio na uzalendo ndani yao wenye njaa kali katika suala la raslmali za nchi, wako radhi kuua kuharibu kwa maslahi yao binafsi.

Tunauzoefu na mikataba iliyofanyika zamani walikuja na gia hizi hizi leo kikowapi, gasi ya waliiinadi hadi kusema wananchi watafungiwa mabomba ya gasi majumbani kwao, leo kiko wapi.

Hii la bandari na mikataba mingine waliosaini china ni ufisasi na wizi mkubwa.
 
Back
Top Bottom