Hawa CRDB bank ni bure kabisa

Hawa CRDB bank ni bure kabisa

Mwankole

Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
84
Reaction score
26
inasemekana kuwa CRDB BANK ndio benki yenye mtaji mkubwa kuliko benki zote za kitanzania (1...BILLION USD) cha kushangaza ndio benki yenye network mbovu sijawahi ona hapa TZ, kwa mfano mara kadhaa nimekwama kufanya transaction kwenye branch zifuatazo Mikocheni, Mbezi Mwisho, Lumumba, Millenium tower, sasa kiboko ya yote ni kwenye customer care, hao wafanyakazi wanavyojib wanavyotaka wao mpaka mtu unajiuliza hivi hiyo kazi wamelazimishwa au salary ndogo? hakika customer care yao ni ZERO kabisa. hizo ATM zao ikifika ijumaa jion zinaenda kula BATA yaaan utazunguka jiji zima ili utoe hela, sasa najiuliza huyu Dr. KIMEI na team yake hawayaoni haya au ndio ile ya Mteja ni MTUMWA kwao?

CRDB Bank used to be the bank that listens.
 
Bora uzunguke mji mzima mafuta hayajakukatikia au bado hujaishiwa nauli, kwa ATMs vimeo nafikiri Barclays ndio wanaongoza
 
Atms za NBC hazikosi pesa hata siku moja

Bro labda huko ulipo

Mimi niko Moro na probability ya kuzunguka ATM zao ukakosa pesa (hadi ya branch yao kuu iliyoko karibu na posta) ni 30:70....ukizipata bila tabu ni maajabu

Siku moja nimeanza branch yao kuu hapo hola, nikaenda SUA kote hola, nikaja tumbaku dude ziro, nikapanda Msamvu kwenye kituo cha mafuta hakuna mpaka nikakereka nikakubali tu kuingia gharama kutolea Master Card CRDB....

Na usiombe uingie hapo ndani Customer care yao ni mbooovuuu sijapata ona...nimewahi kukaa 10min dawati LA huduma kwa wateja Hakuna MTU....kasheshe nenda kwenye teller unaweza kuta msururu then yuko mmoja tu....funga kazi kuna mama mmoja anasaidia process TISS anaiywa Mama Ndeka mpaka najiuliza kwa nini asiende tu kulea wajuku...pathetic
 
Hii taarifa inaniweka njiapanda.. Maana nataka ku-withdraw balance yangu NBC nije CRDB, Huko tena yale yale?
NBC walichonifanya.. Sitakubali.
^^
 
Tatizo la u monopoly...wacha tu wawaringie customers...wakija wawekezaji wapya na customers kuwakimbia watatia akili...

Nakumbuka those days Shoprite walivyokuwa wanadengulia customers...walipokuja kupata washindani hadi walianza kutia huruma...leo hii wameuzwa...

Hata mimi nina bad experience na CRDB ATMs na customer service...mpaka unajiuliza hawa wanalipwa mshahara kiasi gani...wana behave kama manesi wa Mwananyamala...

ATMs ikikaribia sikukuu weka ela zako kwenye simu ...else utakula ugali na maharage huku una pesa benki...

Na TIGO pesa na MPESA nao watawatia akili...
 
Hii taarifa inaniweka njiapanda.. Maana nataka ku-withdraw balance yangu NBC nije CRDB, Huko tena yale yale?
NBC walichonifanya.. Sitakubali.
^^

hamia tu CRDB kwa muda wakati huo tafuta fundi kabisa akutengenezee kibubu....
 
hawa jamaa wamenilostisha nliagiza gari tar 2 nikalipa through CRDB nikapewa recept nasubiria BL nianze process wiki ya tatu nawauliza japan wanasema wameona TT copy hela hawaioni nicheki na bank kwenda CRDB wananambia hela haikutumwa imagine wamekaa na hela 3 weeks na nimelipa charges zote za kutuma hela dah wanasema ni uzembe ulifanyika pesa haikutumwa wamenichosha leo sitarudia tena nimetoa salio langu lote bora NMB aise
 
Fella
CRDB wana mapungufu yao. Lakini kuilinganisha na NBC, mhhhhh! Hapo mnaionea CRDB. CRDB.

CRDB wana nafuu sana. Na bado wanakuja kasi. NBC inaelekea kuzimu. Nilikuwa mteja wa NBC toka kabla haijagawanywa hadi 2011. It was more than too much. Wala sijutii kuhamia CRDB. Wanasikiliza kwa kiasi chake.

Ila msilinganishe na customer service ya Western world. Hapa ni kibongobongo zaidi.
 
Mimi nililipa saa 4 asubuhi na siku hiyo hiyo saa 10 Japan wakanijulisha wamepata hela.
 
mkuu sansiro12 kwangu ni uzembe ulifanyika kwa yule wa counter kutokutuma ela baada ya kuzipokea na kunipa slip nkijua ela imeshaenda kumbe aliweka pembeni sjui akajisahau 3 weeks ndo najua
 
Bora nibaki zangu mkombozi na stanbic tu maana huku ktoa ni fasta tu
 
Fella
CRDB wana mapungufu yao. Lakini kuilinganisha na NBC, mhhhhh! Hapo mnaionea CRDB. CRDB.

CRDB wana nafuu sana. Na bado wanakuja kasi. NBC inaelekea kuzimu. Nilikuwa mteja wa NBC toka kabla haijagawanywa hadi 2011. It was more than too much. Wala sijutii kuhamia CRDB. Wanasikiliza kwa kiasi chake.

Ila msilinganishe na customer service ya Western world. Hapa ni kibongobongo zaidi.

Well said The Invincible

Huduma yao huwezi linganisha na NBC japo mapungufu hayakosekani.

NBC isingekuwa akaunti yao inatumika kwa transactions Kati yangu na ofisi ningeshafunga long time kitambo...Hopeless kabisa hawa NBC
 
Last edited by a moderator:
mkuu sansiro12 kwangu ni uzembe ulifanyika kwa yule wa counter kutokutuma ela baada ya kuzipokea na kunipa slip nkijua ela imeshaenda kumbe aliweka pembeni sjui akajisahau 3 weeks ndo najua

Njoo huku mkomboz na stanbic nakuahid hautpata huo usmbfu huku tuko na father house
 
[TABLE="class: infobox vcard, width: 22"]
[TR]
[TH]Total assets[/TH]
[TD]US$2.154 billion (TZS:3.6 trillion) (2013)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

CRDB Bank

sasa kama wana mtaji huo ni kwanini washindwe kuwa na network stable, wanategemea network za kimagumash? walah hawa CRDB wameniudhi kwa muda mrefu saaaaaana.
 
Back
Top Bottom