Hatuwezi kuzuwia uingizaji wa pikipiki toka nje na kutengeneza zetu?

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
396
655
Hivi serikali haiwezi kuchukua vijana wetu tukawapeleka china kwenda kujifunza utengenezaji na uundaji wa pikipiki?Hata kwa awamu?
Kwanini nasema hivyo pikipiki zimeshaonekana kuwa ni hijati kubwa kwa nchi yetu katika usafirishaji hasa vijijini.Kuliko sisi kuwa soko miaka yote ni wakati sasa tukaanda ujenzi wa viwanda hata kwa ngazi ya kanda na vijana wetu wakazitengenezea hapa hapa zikauzwa bei nafuu.Na imani pia material nyingi zinapatika hapa hapa nchini na soko lake pia linapatikana hata kwa nchi jirani.Ni wazo TU.
 
pale Kibaigwa kuna Wamba wanatengeneza Trailers za Tractors tangu 1990s lkn Kitila Mkumbo akiwa wzr wa Biashara akazindua Ugunduzi wa Makitu hayo in 2022... Kuna kitu hakipo Sawa Nchi hii
 
Unadhani ni rahisi kuiba tec za watu eenh?? Its not about manufacturing, its technology that matters.
Ndiyo technology si tunasema china ni nchi rafiki na Tz.Ndiyo huo urafiki utumike .
Hatuna chuma mkuu, tutazalisha na nini? Tuzalishe chuma kwanza
Leganga na mchuchuma?au haya maeneo yapo Kenya?
Tutengeze spare parts kwanza kabla ya kuwaza kutengeneza nzima nzima
Ulishajiuliza uwezo waliokuwa nao vijana wetu katika kufanya matengenezo,hapa nazungumzia mafundi pikipiki ambao wengi wao hawana shule kivile ila anauwezo wa kuichambua pikipiki kama imetengenezwa Tz.Kupitia maarifa hayo hayo sasa tuunde zetu na tuzipe majina yetu ya asili.Kama Simba motorcycle, Serengeti motorcycle n.k,nchi kama Burundi na Congo zinaweza kuwa soko letu kubwa kwa sababu ya ujaribu tuliokuwa nao hivyo hata gharama nayo itakuwa chini .Watanzania watapata ajira mbali mbali kupitia viwanda hivyo.Tukiamua tunaweza.
 
Hivi serikali haiwezi kuchukua vijana wetu tukawapeleka china kwenda kujifunza utengenezaji na uundaji wa pikipiki?
bhana kila mtu anadhani yeye ni great think kumbe andazi.

Haya ni mambo ya ngazi ya familia na mtu binafsi. hapo serikali inahusika vipi?
 
Wakati unaongea hivyo maccm yameanza kuchimba makaa ya mawe mchuchuma na kuyauza huku chuma huwajui kitahitaji kiasi Gani Cha mkaa. ccm mkosi
 
Back
Top Bottom