hatujaja bungeni kupongezana-mbunge wa nkasi(CCM)

STREET SMART

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
807
622
naangalia bunge live tbc jioni hii, huyu mbunge amewachana serikali ya ccm kuwa maendeleo kwa wananch ni wajib wa serikali na si ombi,amewaambia wabunge waache kupongeza/kupiga makofi kupongeza serikali kwa kila jambo wakati kuna wananch wengi wanatabika na ahadi nyingi za viongozi wakuu hazitekelezwi. Kumbe kuna majambazi mengine yana akili kidogo
 
Huyu mbunge lazima atawekwa kitimoto na wanamagamba wenzake ! Mawaziri wamebaki midomo wazi hawakuamini mbunge wa ccm kuikosoa Govt namna ile. Well done huyu mbunge anatakiwa ahamie CDM!
 
naangalia bunge live tbc jioni hii, huyu mbunge amewachana serikali ya ccm kuwa maendeleo kwa wananch ni wajib wa serikali na si ombi,amewaambia wabunge waache kupongeza/kupiga makofi kupongeza serikali kwa kila jambo wakati kuna wananch wengi wanatabika na ahadi nyingi za viongozi wakuu hazitekelezwi. Kumbe kuna majambazi mengine yana akili kidogo
Shida kuyajua, maana yanajificha katika magamba magumu sana na mazito kwelikweli, kuyatoa lazima uyachome moto, lakini ccm inabakia kuwa kimbilio la watu duni kifikra na watu wenye tamaa za mali na ukoloni mweusi
 
Mission zimeshaanza kusukwa taratibu, kufikia mwakani tutakuwa na kundi la wanamagamba wenye mlengo wa kutetea wananchi ili wapate kura, na hatimaye wapate nguvu ya kupachika rais wao 2015. Subirini mtaona, na hisi kuna mgombea nyuma yao! fikiria tu tokea asubuhi Lembeli naye kasema point leo!!
 
Jamaa kaipa serikali yake ya ccm za uso live ila aliposema wagonjwa wa UKIMWI waachwe wajifie kwani wanajitakia hapa aliharibu japo lengo lake ni kukerwa na namna fedha za Ukimwi zinavyoliwa na si kuhudumia walengwa.
 
kwa kweli aliongea vizuri sana hadi nikaona aibu kwa niaba ya wanaolamba serikali miguu. kanifurahisha zaidi mfano hai "bwana ngeleja (sio mheshimiwa,lol), kwangu sina umeme!''. kama wote wa ccm na upinzani wangekuwa wanaongea point bila kutapika nyongo tusingekuwa na hasira hii tuliyonayo!
 
Kesho watamjadili,amekiuka makubaliano ya kuitetea bajeti kwa mujibu wa kikao chao baada ya mkulo kuwasilisha......lo
 
Kesho!!! Huyo anawekwa kiti moto leo leo usiku na mpaka sasa atakuwa kashapewa vimemo vya kumpigia mikwala.
 
Kabla yake alichangia pia Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema naye alichangia vizuri sana kuhusiana na hilo hilo la kupongezana. Alisema kazi ya Mbunge siyo kuipongeza Serikali ila ni kuiambia itekeleze wajibu wake bila kujali Mbunge ametoka Chama gani. Pia alizungumzia kitendo cha wanasiasa kujifanya wako karibu na makanisa na misikiti kinapokaribia kipindi cha uchaguzi, na wanafurahi pia Viongozi wa dini wanapowataja kuwa ni chaguo la Mungu, lakini kibao kinabadilika wanapokemewa na kudai kwamba viongozi wa dini wanajiingiza kwenye masuala ya kisiasa.
 
jamaa hakubaika wala kupindisha maneno yuko very bold,kamtaja kabisa pinda uliahidi barabara lakini umekaa kimya, walitamani kummeza jamaa.
 
Yule ni mbunge wa Chadema iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa! Siyo vizuri kuleta thread bila uhakika wa unachokisema!
 
Yule ni mbunge wa Chadema iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa! Siyo vizuri kuleta thread bila uhakika wa unachokisema!
Mkuu baada ya mchungaji msiga kumaliza kuchangia, aliingia mbunge wa nkasi Ally Kessy,akatema cheche hizo. Kama hutaki kwaheri
 
jamaa kakomaa nao, watamsema sana ila naambiwa alipinga bajeti ya mkulo kwenye caucus ya chama chao lakini akapigwa biti nzito akauchuna. Ila watamshughulikia
 
Back
Top Bottom