voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,467
- 11,603
Ukiangalia Bungeni Live kwa sasa!
Utakachokiona ni mashindano ya wabunge wa CCM kusifia na kupongezana!
Utakachokiona ni picha ya Unafiki uliopitiliza kwa asilimia kubwa ndani ya jengo la bunge letu tukufu!
Wabunge wameleweshwa na pesa za mgao,ambazo zinagawiwa kwao,na kuishia kufujwa na watendaji wasio waadilifu nchini.
Ni kama vile wabunge wamelewa pesa za mheshimiwa Rais na kuwasahau wananchi wao na madhila wanayokutana nayo huko mitaani kwa sasa!
Kila mbunge anatumia muda mwingi kusifia,kupongeza na kisha kudhukuru kwa mgao alioupata jimboni kwake!
Maana yake ni nini?:
Ni kwamba,wanachokijali na kukipa umuhimu kwa sasa,ni wao kupata mgao na walau kujenga au kukamilisha mradi mmojawapo jimboni.
Jambo ambalo wanaamini wabunge wengi huko bungeni, kwamba,watalitumia kama mtaji kisiasa na kuweza kutetea nafasi zao kwenye uchaguxi mkuu 2025.
Lakini wanachokisahau ni kwamba,wananchi wanapitia wakati mgumu sana huko mitaani!
Na wanajaa hasira kupitiliza,pale wanapowaona wabunge wao,ambao ndio waliostahili kuwasemea,wamebadilika na kuwa wasakatonge na wasaka uteuzi huko bungeni.
Wameuguza ukumbi wa bunge,kama sehemu ya kumsalimia rais,na kushindana kumsifia wakitarajia kukumbukwa nae,pale ambapo kuna fursa ya uteuzi itakapojitokeza!
Wabunge wetu,ukiwasikiliza wanachokiongea bungeni,na ukaulinganisha uhalisia uliopo mitaani kote nchini,unaeza ukadhani hso wabunge ni wageni waikwa ndani ya mjengo wa bunge.
Wabunge wetu....wanacheka pale walipostahili kulia!
Na...Wanalia pale walipstahili kucheka!
Ni kama vile wako "Upside-down"...
Ni nini kimewakumba wabunge wetu jamani?
Mimi nimepita tu!
Ijumaa Kareem!..
Kesho ndio Eid na sio leo(Kwa mujibu na maelekezo ya mufti).