Hatuambiwi Kingunge ni mzaliwa wa wapi

Hatuambiwi Kingunge ni mzaliwa wa wapi

Jibu sahihi wanalo vingunge waliobakia Pius Msekwa na John Malecela.
 
Mimi kwa ujasiri wa yule baba ni naamini ni mkurya

Hivi Wakurya ni wajasiri???..Sina hakika na hili...ila nafahamu kuwa wana hasira na ni wakali...ujasiri una maana kubwa na pana.anyway .it is debatable....Wahehe ni wajasiri au wana hasira au ni wakali?, sijui..vipi wasukuma? na Wanyamwezi je?? Vipi Wangoni nao?? vipi Wazaramo pia?? anyway, ni mjadala...ingawa mijadala ya aina hii haina tija kwa mshikamano na umoja wa taifa letu.....
 
Hivi Wakurya ni wajasiri???..Sina hakika na hili...ila nafahamu kuwa wana hasira na ni wakali...ujasiri una maana kubwa na pana.anyway .it is debatable....Wahehe wana hasira au ni wakali?, sijui..vipi wasukuma? na Wanyamwezi je?? Vipi Wangoni nao?? vipi Wazaramo pia?? anyway, ni mjadala...ingawa mijadala ya aina hii haina tija kwa mshikamano na umoja wa taifa letu.....
Una shida na sisi wakurya?

Lukwafya
 
Kwanini unataka umjue vizuri baada ya kufa..?? Itakusaidia nini ukishamjua..?? Kwanini hukutaka kumjua wakati bado yupo hai...???

Wabongo tupendane jamani, japo kinafiki...!!
 
Wana Bodi Amani ya Bwana iwe Nanyi,

Ni kweli kwamba mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hatunae tena,
huyu mzee aliwahi Kuwa kiongozi wetu.
naomba kujua alizaliwa wapi na ni Kabila gani na inakuwaje azikwe Makaburi ya kinondoni.
Kuna kipindi nilijua Kingunge Mwiru ni ndugu wa Damu na chief Kinjikitile Mwale,

niliamini kabisa pale niliposikia Ana mtoto anaye itwa "Kinje" nilimpenda huyu mzee kwa ujasiri wake, ucheshi wake
kuifahamu itikadi
yake vizuri,
kuwa na msimamo (tujifunze hili)
kule kuongea kwake kwa "KOMA" pia jina Lake limekaa kiasili
"Kingunge Ngombale--Mwiru "


tunaomba wanaomjua kuzaliwa kwake watuelezee.


Tafadhali mods msiunganishe huu uzi.
Sikh zote ukisikia MTU yeyote anaitwa mwiru, ujue huyo ni mmatumbi kutoka wilaya ya kilwa, mkoa wa Lindi, mwiru ni ukoo au km mnavyoita watu wa bara koo, baadhi ya koo za kilwa ni pamoja na Mwiru , Mandwanga, Mweyo, Litumbi. Mpamba, Liponjo, mnyembwa, Uponda, Pendapo, Mboweto, Nganikele, Kiyonga, Kikope, Mketo, Mpondi, na nyengine nyingi, hivyo unavyosikia mwiru, ni kama unavyosikia Kimaro, Au Nyanda, Au Mwita, bado utajiuliza kimaro ni wawapi?
 
Marehemu kabila lake ni MMATUMBI
Ni mzaliwa wa KILWA KIPATIMU

Dini ya wazazi wake ni Mkristo dhehebu KATOLIKI
yeye Mwenyewe baada ya tafakuri nyingi ,udadisi Mwingi,midahalo na mabishano aliamua kuwa "FREE THINKER"

AU "INDEPENDENT THINKER" Marehemu mkewe yeye alikuwa ni Mkatoliki .

Amesoma UHURU MCHANGANYIKO kisha akaenda TABORA SCHOOL.

Kama taifa lingekuwa linajali HISTORIA YAKE huyu Mzee ni miongoni mwa watu waliopaswa KUIMBWA maana kama unamsifu NYERERE hupaswi kumuacha huyu.

Ni miongoni mwa watu wachache katika taifa hili waliomuelewa MWL. NYERERE miongoni mwa wanafunzi wake WENGI.
 
Wana Bodi Amani ya Bwana iwe Nanyi,

Ni kweli kwamba mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hatunae tena,
huyu mzee aliwahi Kuwa kiongozi wetu.
naomba kujua alizaliwa wapi na ni Kabila gani na inakuwaje azikwe Makaburi ya kinondoni.
Kuna kipindi nilijua Kingunge Mwiru ni ndugu wa Damu na chief Kinjikitile Mwale,

niliamini kabisa pale niliposikia Ana mtoto anaye itwa "Kinje" nilimpenda huyu mzee kwa ujasiri wake, ucheshi wake
kuifahamu itikadi
yake vizuri,
kuwa na msimamo (tujifunze hili)
kule kuongea kwake kwa "KOMA" pia jina Lake limekaa kiasili
"Kingunge Ngombale--Mwiru "


tunaomba wanaomjua kuzaliwa kwake watuelezee.


Tafadhali mods msiunganishe huu uzi.

unataka nani akuambie? msomi mzima unashindwa ku google tu unaanza kurusha lawama hovyo hovyo

mzaliwa wa Kilwa kipatimo

tafuta thread inayosa jinsi alivyogombana na kanisa katoliki
 
Mzee kingunge ni ndugu mjukuu wa kinjekitile ngwale mbabe wa vita vya waterwater.
 
Huyu jamaa ni M communist kutoka China.
isije Ukawa umesema hvyo kulingana na itikadi yake na Mavazi aliyokuwa akiyavaa [emoji23][emoji23] mzee alijua kusimamia kitu mpaka kikamjengea jina.
 
Swali zuri....Mimi nafahamu kuwa yeye ni mzaliwa wa Kilwa Kipatimu....kabila lake ni Mmatumbi....Kilwa Kipatimu kuna Misheni ya siku nyingi tangu ukoloni..wengi wa eneo hilo walipata elimu iliyokuwa ikitolewa na wamissionari, nadhani Kingunge ni miongoni mwao...kumbuka kuna Kilwa Kivinje...
kabisa Huenda ni miongoni mwao! Kingunge ana historia ndefu, watu wenye umri mkubwa kama wa Kingunge Ngombale Mwiru ni hazina kwa Taifa.

kijiografia Kilwa yote ilikuwa chini ya vita miaka hiyo. hata sisi darasani tulisoma mambo ya wakoloni. sijui miaka hii kama haya masomo yapo.
 
Ngombale Mwilu anatoka ukoo wa Kinjekitile Ngwale, Chifu aliyepigana vita ya majimji kuupinga utawala wa Wajerumani.

Kinjekitile Ngwale alikuwa na uwezo wa kuongea na mizimu. Hizi ni imani za asili kabla ya ukoloni kuingia
Lakini haujasema sehemu specific anayotokea uneeleza historia na watu anaohusiana nao
 
Mkuu ndoo kwenu ama katika harakati za kutafta mkate maana ile ukijani ulinivutia nikatamani nipate mtuu tufanye biashara lakini nikaogopa wajanja
Ahaaa, hapana Mkuu ila nimeoa kwenye ukoo huo huo.
 
Kingunge ni mkomunisti toka ugogoni kijiji cha Kigwe wilayani Bahi. Wazazi wake walimsomesha kwa biashara ya chumvi toka Lukulo. Mdogo wake yupo Ubungo msewe pale ni kiongozi serikali za mitaa kupitia Chadema. Ni maarufu sana. Najua hivyo tu
 
Back
Top Bottom