Hatuambiwi Kingunge ni mzaliwa wa wapi

Hatuambiwi Kingunge ni mzaliwa wa wapi

Wana Bodi Amani ya Bwana iwe Nanyi,

Ni kweli kwamba mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hatunae tena,
huyu mzee aliwahi Kuwa kiongozi wetu.
naomba kujua alizaliwa wapi na ni Kabila gani na inakuwaje azikwe Makaburi ya kinondoni.
Kuna kipindi nilijua Kingunge Mwiru ni ndugu wa Damu na chief Kinjikitile Mwale,

niliamini kabisa pale niliposikia Ana mtoto anaye itwa "Kinje" nilimpenda huyu mzee kwa ujasiri wake, ucheshi wake
kuifahamu itikadi
yake vizuri,
kuwa na msimamo (tujifunze hili)
kule kuongea kwake kwa "KOMA" pia jina Lake limekaa kiasili
"Kingunge Ngombale--Mwiru "


tunaomba wanaomjua kuzaliwa kwake watuelezee.


Tafadhali mods msiunganishe huu uzi.

Kilwa kipatimu ndio kwao kwa asili
 
Kilwa kipatimu, kabila Mngindo kwa mama na baba yake ni Mmatumbi, wanapendaga kusema 'bwana weweee!!! 'wanaasili ya Liwale babu yake John kinjekitile Ngwale Mwiru alitoka liwale kipindi cha vita vya majimaji akasogea kipatimu
 
Wabongo bwana eti source nizame chumvini, source mbunye haya zama huko chumvini tuone utatoka na habar gani zaid ya UTI, acha bangi mkuu
Unawaza ngono tuu kila wakati na ndio maan Trump anawaita shithole.
 
Sio kama nina dharau lakini hii inaonesha nu jinsi gani hatusomi historia yetu vizuri.
Vizazi viwili au vitatu vya gombare mwiru vipo ktk historia ya ukombozi Wa Taifa hili.
Mkuu ukisoma post zote zinamuhusu Mzee kingunge utaona kbs watu wanadanganyana,kwa uvivu wa kutokusoma vitu,halafu ni ma GT
 
Ngombale Mwilu anatoka ukoo wa Kinjekitile Ngwale, Chifu aliyepigana vita ya majimji kuupinga utawala wa Wajerumani.

Kinjekitile Ngwale alikuwa na uwezo wa kuongea na mizimu. Hizi ni imani za asili kabla ya ukoloni kuingia
Yaan wew ndo hamnaz umeambiw kingunge wew unaelezea kinjektile wee unafikil hio history ya daras la pili sis hatuifahm
 
Kuna watu wanasahau walikozaliwa au asili yao,
Inakuaje mtu aliewahi kuwa kiongozi kwa awamu nyingi lakini
Watanzania wengi hawjui asili yake, kuna walakini hapa!
Ni maoni tu c lazima.
 
Ngombale Mwilu anatoka ukoo wa Kinjekitile Ngwale, Chifu aliyepigana vita ya majimji kuupinga utawala wa Wajerumani.

Kinjekitile Ngwale alikuwa na uwezo wa kuongea na mizimu. Hizi ni imani za asili kabla ya ukoloni kuingia
bado wengine tunazo
 
Kusini mashariki mwa mwambao wa gaza ukitokea milima ya sinai karibu na mto jordani pale katikati ya mississippi ya mashariki ya kati
 
Tuwe tunajibu ki- staarabu MTU anauliza kutaka kujua Mzee wetu alikuwa MTU anatokea wapi ktk nchi hii Eti Mara tarime wengine somalia.nn maana ya kuuliza? Hujui waachie wanaojua watujuze
 
Back
Top Bottom