• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Hatua saba muhimu za uponyaji wa CHADEMA!

L

LENGEJU BOB

Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
53
Points
0
L

LENGEJU BOB

Member
Joined Nov 1, 2010
53 0
Na. Robert Victor Lengeju.


DONDOO
1. Busara ya Ukimya: kufikiri kabla ya kusema na kuchagua cha kusema
2. Toba, Msamaha, Upatanisho na Maridhiano
3. Kamati ya wazee wenye hekima, wasio na upande wala ushabiki na upande
4. Wasivuliwe uwanachama, lakini wasijereshwe kwenye vyeo vya awali.
5. Makundi yakemewe, yavunjwe
6. Zitto na Mbowe wakatazwe kugombea uwenyekiti.
7. Nyufa zizibwe haraka !

UTANGULIZI


Wiki kadhaa kabla ya Sakata ya kuenguliwa kwa Viongozi waandamizi wa Chadema kutoka katika nafasi zao za uongozi, niliandika Makala yenye Kichwa cha habari "CHADEMA MMELEWA SIFA, MNAPOTEZA UHALALI WA KUAMINIWA DOLA!.. Kwa wanaofahamu vema matumizi ya lugha ya nyakati watakuwa wameelewa tofauti kubwa kati ya NA…TA… na ME. Sikusema M'ME'POTEZA UHALALI, WALA M'TA'POTEZA UHALALI, bali M'NAPOTEZA Uhalali. Matumizi ya NA badala ya TA au ME sikuyaweka kwa bahati mbaya. Ni matumizi yaliyozingatia tafakuri ya kitafiti na uhalisia wa masuala ya msingi sana katika sayansi ya jamii na siasa na hasa katika mazingira ya siasa za Tanzania ya leo. Kwa ufupi lile lilikuwa ni angalizo, kwamba mnakoelekea siko na mkijirudi mnaweza mkasalimika. Ndiyo maana, kwa wale waliokuwa na msuli wa kuisoma mpaka mwisho Makala ile ndefu, waliona nimemalizia Makala ile kwa kusema….MSIPOJIREKEBISHA, TUTAWAADHIBU…Maana yake ni kwamba MKIJIREKEBISHA, TUTAWAPA TUZO!


POLE KWA WAHANGA


Kwa unyenyekevu, naomba nitoe pole zangu za dhati, kwa Kaka zangu Dr.Kitila Mkumbo, Mwigamba na Mh. Zitto Zuberi Kabwe (MB), kwa yale yaliyowakuta. Mimi ni mwanafunzi wa sheria, katika taaluma hii tunajifunza kuwaona watu wote, hata wale wanaotuhumiwa, kuwa hawana hatia mpaka pale watakapopewa nafasi ya kujitetea na kukutwa na hatia, pasipo shaka yoyote. Sina hakika ni kwa kiwango gani taratibu zilifuatwa katika kuwapa nafasi ya kujieleza, naambiwa Katiba ya Chadema inaelekeza kuwapa nafasi ya kujieleza kwa maandishi; nisiingie sana huko. Kwa leo nitoe pole tu, kwamba yamewakuta na ndiyo madhila ya siasa katika nchi hizi changa kidemokrasia.
Pole pia kwa CHADEMA. Mtu mwenye akili anaweza kupima uzito wa maamuzi mliyochukua na athari ambazo tayari zimeanza kujitokeza. Ni wazi kuwa uamuzi huo unatarajiwa kuleta athari mlizozitarajia lakini mlizojiandaa kuzikabili. Au pengine mmekubaliana na ukweli wa kitafiti, kwamba athari za kufanya mlichofanya ni ndogo kulinganisha na athari za kutokufanya mlichofanya. Kwa vyovyote vile, CHADEMA imeguswa, imetoneshwa, imeparuriwa, imeumizwa, imetikisika. Najua ninyi ni watu wazima, wenye mapenzi mema kwa chama na Nchi, wapiganaji mnaojitolea maisha kwa safari ya Demokrasia…Hili linawaumiza sana, kama Mama anavyomwadhibu mtoto wa kumzaa mwenyewe…Poleni sana, ndio ukubwa huo.


PONGEZI KWA CHADEMA


Bila haya, naomba nitoe pongezi za dhati kabisa, kwa Kamati kuu ya Chadema, kwa walau kuchukua hatua na kufanya maamuzi magumu. Pengine hili limesaidia kuchora mstari Fulani wa siasa za uwazi na uwajibikaji. Kwa nguvu aliyonayo Zitto ndani ya Chama na katika Siasa za Tanzania, inahitaji Chama chenye moyo wa Jiwe kuweza hata kuthubutu kumkemea!.. Dr. Kitila Mkumbo ni mmoja wa wanazuoni mahiri mno na tegemeo kubwa sana kwa Chadema hasa katika idara ya mipango na mikakati ya kisayansi. Huyu ndiye aliyesimamia utengenezwaji wa ilani ya uchaguzi iliyoizalishia Chadema wabunge na madiwani wengi Zaidi kuwahi kutokea katika historia ya ukuaji wa Chama hiki nguli cha upinzani Tanzania. Ni mwanazuoni ambaye kuingia kwakwe kwenye siasa kumepokelewa kwa moyo wa shukrani mno na kwamba kumgusa huyu naye, kunahiaji moyo wa jiwe na uthubutu wa hali ya juu. Katika hili, Jamii inajifunza mambo mawili makubwa.

1. Kwamba, chama chochote, chenye malengo ya kushika dola, kinapaswa kuonyesha kwa vitendo, kwamba kina uwezo wa kuchukua maamuzi magumu, hata yale yanayoelekea kukiumiza chenyewe, kwa muda; kama maamuzi yenyewe yamejengwa katika misingi ya uwazi, ukweli na kufuata sheria na taratibu.

2. Kwamba, vyama vya Siasa vinapaswa kujifunzwa kuwa, chama hakiendeshwi kwa nguvu ya mastaa flani ndani ya chama. Chadema wameonyesha kuwa hawababaikii mastaa, ukileta utovu wa nidhamu, unawajibishwa, mchana kweupe! Sina shaka mastaa waliosalia, ndani ya Chadema wameanza kuona nguvu ya chama badala ya nguvu ya watu fulani kwenye chama.

Mifano iko mingi sana. Kamati kuu ya ANC (chama cha ukombozi) cha Afrika ya kusini, juzi juzi tu kimemwondoa Kijana Machachali, maafuru na anayependwa sana na mwenye ufuasi mkubwa wa kundi la vijana wa chama na wale wa kawaida, Julius Malema, kwa kutofautiana na viongozi wake wa chama. Kwa hapa Tanzania kuna mifano mingi tu, ndani ya Chadema na Nje ya Chadema: Rejea Sakata la Dr. Kabour, Chacha Wangwe, David Kafulika, Hamad Rashid na Mansour, kuwataja wachache.

TAHADHARI KWA CHADEMA
Kama nilivyoainisha awali. Zitto kabwe ni Mwanasiasa kijana lakini mwenye historia ndefu sana ndani ya CHADEMA. Nimesoma neno kwa neno, nyaraka kadhaa,ikiwemo Katiba ya CHADEMA na Ilani yenu ya UCHAGUZI. Nimesoma waraka ule mlioukana wa Tuhuma za Mabilioni ya Zitto, nimesoma waraka wa Timu ya ushindi "Mkakati wa Mabadiliko, nimesoma Tamko la chama la kuwavua uongozi, nimesoma Tamko la wahanga la kujibu mapigo na nimesoma pia Tamko-rejesho, la Chama dhidi ya utetezi wa wahanga kwenye mkutano wa SERENA. Narudia, nimesoma neno kwa neno na kurudia rudia mata nyingi mno, nyaraka zote hizi. Nimetumia muda mwingi sana kweye mitandao ya kijamii (Si kwa kiwango cha kujinyima nafasi ya kufuatilia masomo yangu), nimefanya mahojiano na watu kadhaa, wekiwepo wenye majina makubwa na waheshimiwa. Watu wa kawaida, wasomi, viongozi wa dini, wakulima na wavuja jasho. Nimepata maoni ya madereva wa taksi na pikipiki, nimepata pia maoni ya wafanyakazi wa sekta ya usafi pale chuoni kwetu. Nimezungumza na wapiga debe. Zaidi ya 45% ya watu niliowauliza wamechanganyikiwa! Wengi wa niliozungumza nao hawana kadi za chama. Japo wanashabikia siasa! Maoni ya wengi ni Uzitto wa Zitto Kabwe! Kwamba, pamoja na utovu wa nidhamu, ana kundi kubwa mno la watu wanaojinasibisha kama wafuasi, walio tayari kumfuata kokote, wakati wowote!

Lakini hilo ka ufuasi halina msingi sana. Kwani kama makosa yangalikuwa ya kishetani sana, jamii ingaliwahukumu kwa kuwazomea kila wapitapo. Lakini mkutano wa Serena umethibitisha vinginevyo, kwamba miongoni mwa wanaowaunga mkono, wamo wanachama na viongozi waaandamizi wa CHADEMA, wale wenye ujasiri wa kujitokeza wazi wazi na wale ambao bado wanaonekana watii mwilini lakini mioyoni wameshahama zamani!

Tahadhari yangu ni kwamba, kundi hili lisipuuzwe. Alipotoka Mrema, NCCR ilibaki, lakini sote tunajua kuwa NCCR ya leo si ile ya wakati ule. Kwamba maamuzi kama haya yalishawahi kufanywa na hakukuwa na athari ni kauli ya KAMARI Zaidi. Kwamba kwa kuvaa pete fulani ya bahati, nitashinda game! Iko siku game itakataa, pete itakuwa nzito!

TAHADHARI KWA TEAM ZITTO
Katika tafuta tafuta yangu, kuna walionambia mnajiandaa kujiunga na chama flani kichanga cha siasa. Sikutaka kuamini na kwakweli sijaamini, nadhani ni uzushi wa kitaa, lakini lisemwalo lipo. Yaelekea mmepiga mahesabu na kuona hakuna pa kutokea. Mmekata tamaa na kuamua kuanza kivyenu. Ni uamuzi mzuri na unapewa nguvu ya kisheria na kikatiba. Lakini ni uamuzi hatari mno kwa mustakabali wa utu na hadhi yenu kisiasa. Nafahamu mna elimu kubwa na uzoefu Zaidi kuliko mimi kwenye masuala ya siasa na uongozi.

Lakini mimi, pamoja na wengi kama mimi tumewazidi eneo moja muhimu, sisi tunaishi mtaani, vijijini, huku high density, uswazi, ambako kwa usomi na uheshimiwa wenu mnakuja ama kwenye utafiti ama kwenye operation sangara, hamna ufahamu wa kutosha wa maisha yetu ya siku nzima kuanzia chai ya ugali wa kuchoma, dash ya mchana na kiporo cha ugali wa asubuhi kinacholiwa usiku kimya kimya! Kwenye mikutano ya siasa kuna lugha tofauti na vijiweni, trust me, huku vijiweni kuna majibu magumu kwa maswali magumu! Mkijaribu kufanya mnachotaka kufanya, mmekwisha!

Umaarufu wote mlionao umetokana na misingi mliyojengewa na CHADEMA. Wapo waliokwishaamini kuwa ninyi ni wasaliti, na kukimbia ni kuthibitisha usaliti wenu! Nimetiwa moyo na kauli ya Zitto, kwamba hang'oki Chadema! Naamini ni kauli ya M1 pia. Afya yenu kisiasa inategemea sana namna mnavyoweza kumaliza tofauti zenu na kubaki salama ndani ya CHADEMA!

Hizi kelele za wafuasi wenu ninazozishuhudia mitandaoni zinaashiria uchanga wa kisiasa. Hamuwezi kujidai ni wanachama waaminifu wa Chadema wenye lengo la kuimarisha chama huku mnashinda mitandaoni kukibomoa chama mnachokipenda. Kwa haya mnayoyaandika huku mitandaoni, hata ikitokea siku mmeshika chama hamtakuta mwanachama huko. Mmeshasema sana, tumewasikia. Zitto ameonyesha njia kwa kukubali yaishe. Alikuwa na nafasi ya kueleza yote hayo mbele ya waandishi wa habari lakini hakuona busara kufanya hiyvo. Tulidhani alionyesha ukomavu, lakini haya mnayoyaandika yanatuonyesha kuwa kumbe yale ya serena yalikuwa ni maigizo tu, hakuna busara wala usomi, mana ameacha yeye kusema lakini anawatuma wengine waseme...Hebu mkue sasa!

HATUA SABA MUHIMU
1. BUSARA YA UKIMYA:
kufikiri kabla ya kusema na kuchagua cha kusema
Watu wenye akili walipata kusema, kuwa ukimya "sometimes" ni majibu mazuri Zaidi kwa matatizo fulani fulani. Kwa hapa mlipofikia, yatosha, nyamazeni sasa. Acheni mara moja, majibizano ya kwenye vyombo vya habari au kwenye mitandao ya kijamii. Nimeona rafiki zangu kadhaa wakiwa bize kutafuta kitu cha kurusha facebook au Jamii forum kila siku, kwa lengo la kuponda kambi fulani. Huo ni ujinga, trust me! Huwezi kuukata mti ulioukalia! Mliyosema yametosha, machozi yameisha,vicheko vimekatika, sasa kaeni kimya. Ikiwalazimu kusema, bas chagueni cha kusema, mseme wapi, wakati gani na mseme na nani, katika mazingira yepi.

2. TOBA, MSAMAHA, UPATANISHO NA MARIDHIANO
Hili lina msingi katika masuala ya Imani juu ya MUNGU. Kwamba hakuna binadamu aliyekamilika. Ubabe haujengi wala kiburi hakina tija. Kwa waraka ule, MM, M1-M3 mmefanya makosa makubwa. Ndio maana hata ninyi wenyewe mlikiri makosa na kukubali kuachia ngazi. Ni makosa yatokanayo na misingi ya kinidhamu juu ya taasisi inayoongozwa na watu ambao wapo madarakani kwa mujibu wa sheria, bila kujali tamaa zao za kutaka kuendelea kuongoza! Mkakati ule, japo ni wa kawaida sana katika siasa za ushindani, umejaa lugha ambazo hazikupaswa kutolewa na watu wasomi wa kiwango chenu.

Tuhuma mlizoziainisha, japo ni siri, mliziainisha kwa namna ambayo mlijua, zikigundulika, ama iwe mtaji kwenu kushika hatamu za uongozi bila kujali athari mnazokiletea chama ambacho wenyewe mnakiri kukipenda mno! Kwa kweli, ni kama mlijiandaa kwa staili ya "Me or No one else"… Kisheria huo haukuwa uhaini kama inavyoaminishwa. Uhaini ni kula njama za kuangusha serikali/dola (state), rejea kesi ya SHARIF HAMAD V SMZ. Chadema sio dola, wala state, kosa lililofanyika ni ukorofi, utofu wa nidhamu au hata ukengeufu, lakini sio uhaini. Hata hivyo ni kosa kubwa linalohitaji mkosaji ajue kuwa alikosea. Kile alichofanya Dr.Kitila cha kuomba msamaha, kinapaswa kufanywa tena ki-mkakati, Msione haya, chukueni muda wa kutafakari na kutafakuri, mnaweza, na mtajitwalia heshima!

Watu kadhaa mashuhuri pia wanawaza kama mimi katika hili. Mkurugenzi wa TAMWA, Mama Ananilea Nkya amaenukuliwa na Gazeti la Mawio (Nov 28, 2013) akisema na ninanukuu " Niwape ushauri kidogo Dr.Kitila, Mwigamba na Zitto. Kama kweli haya tulioelezwa mmehusika, ni vema mkakubali kuna mahala mmepotoka kiasi….Tulieni, tafakarini na ombeni radhi. Adhabu iliyotolewa kwenu ya kuvuliwa vyeo ni utaratibu wa kibinadamu wa kurekebishana ". Huyu ni mmoja wa wanawake nguli katika masuala ya Kijamii, ni msomi na mpiganaji wa kupigiwa mfano. Kwa vyovyote vile, ushauri wake wafaa kuchukuliwa kwa uzito.
Naye Prof.Abdallah Safari, amenukuliwa kupitia chanzo nilichotaja awali akiunga mkono dhana ya toba na msamaha kama suluhisho la kistaarabu Zaidi; amesema " kwakuwa Zitto na Dr.Kitila wameomba radhi na kukubali kujiuzuru, hakuna haja ya kuendeleza malumbano zaidi"

Kwa kutilia mkazo dhana hii, Zito kabwe na Dr.Kitila Mkumbo wote wameonekana kukubaliana na dhana hii kwa kukubali kwao si tu kuomba radhi bali pia kuwa tayari kujiuzuru nafasi zao za uongozi, kabla ya kamati kuu kukataa ombi lao la kujiuzulu na kuamua kuwafukuza. Wakati zito akinukuliwa kutamka ndani ya KK "Nimesikia ushauri wa kaka yangu, Komu...najiuzulu kulinda hadhi ya chama changu na mimi binafsi". Kitila Mkumbo kwa upande wake amenukuliwa akikubali mapungufu yaliyomo kwenye waraka na kuomba msamaha. Kuelekea kwenye kujieleza ni kwanini wasifukuzwe, nashauri wahanga hawa wajipange kuomba radhi ya dhati na kamati maalum isimamie kuhakikisha kwamba kuomba kwao msamaha isiwe ndiyo tiketi ya kuadhibiwa na kuumbuliwa Zaidi na maadui zao.

3. KAMATI YA WAZEE
Tafuteni watu wenye hekima, ndani au nje ya CHADEMA. Wale walio kwenye minong'ono achaneni nao. Mimi nitawataja wachache..ndani ya chama chukua jembe kama Prof. Baregu na Prof. Safari. Msiwategemee sana wazee wa chama pekee katika kutatua hilo, wazee wa chama walishashindwa ndo maana mmefika hapo mlipo. Pia, msione haya, tokeni nje kidogo chukua watu kama akina Mzee Joseph Butiku, Mwalimu Azavery Lwaitama na wengine mnaowafahamu kuwa wanaweza kusimamia mkakati wa upatanisho bila kuingiza hisia za upande fulani. Mkiweza, chukueni wazee kutoka vyama marafiki vyaTanzania, Afrika au hata nje ya Afrika.

4. WASIVULIWE UANACHAMA, LAKINI WASIRUDISHWE KATIKA NAFASI ZAO ZA UONGOZI
Kama nilivyokwisha eleza hapo awali. Hawa watu wasivuliwe uanachama kama ambavyo inaonekana ni nia ya kudumu ya CC ya Chadema. Tamko rasmi litolewe likijikita kwenye maelezo yao ya utetezi wa maandishi. Kwamba wamejieleza vya kutosha na wameridhisha CC, na hivyo, wanabaki kuwa wanachama. Wasirejeshwe katika nafasi zao kwani huko kutamaanisha chama ni kigeugeu. Lakini wanaweza kupatiwa nyazfa zingine ili kuonyesha Imani kwao, kuwapa tena nafasi ya kuthibitisha vinginevyo na kuwapa fursa ya kufanya malipizi wa dhambi zao kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kwa ari Zaidi. ZZK anaweza akabaki na cheo cha Naibu Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ili kumpa fursa ya kuendelea kusimamia mitakati ya chama katika bunge, akiwa ni miongozi mwa wabunge wazoefu ki-mkakati na kiuongozi, miongozi mwa wabunge wa CDM walioko bungeni sasa.

5. MAKUNDI YAKEMEWE, YAVUNJWE
Viongozi wa mitandao watangaze kuvunja mitandao yao. Kamati maalumu iundwe kufuatilia nyendo, ili kujiridhisha kuwa kuna mtandao mmoja tu wa CHADEMA. Hili lifuatane na kutajwa kwa wanamitandao waandamizi, katika kamati maalumu, kuitwa na kuonywa mbele ya wakubwa wao, kwamba mitandao sasa basi, mkakati wa ushindi ni mmoja tu na mabadiliko tunayohitaji ni ya kushika dola, sio uenyekiti wa chama! Mapambano yanayoendelea ki-mitandao yanazidi kukipasua chama na kuzidi kukiondolea uhalali wa kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

6 MBOWE NA ZITTO WASIGOMBEE UENYEKITI WA CHAMA
Pengine hili ni jambo kubwa na gumu sana kushauri na kutekelezeka. Lakini kwa utafiti nilioufanya, busara inaelekeza nishauri hivi bila kuogopa. Kwakuwa moja ya sababu za msingi za mgogoro wenu ni suala ya uchaguzi wa ndani. Basi itamkwe bayana, kuwa MBOWE na ZITTO wamekatazwa na CHAMA kugombea uwenyekiti.

Mimi siamini kabisa kwamba Chama kikubwa kama Chadema kina watu wawili tu wenye uwezo wa kuwa wakuu wa chama. Sitaki kuamini kwamba Chadema ni Zitto na Mbowe tu. Watu wengine, hasa wale wasio na majina makubwa wagombee nafasi hiyo. Na hata ikiwa ni wale wenye majina lakin wenye kukubalika na pande zote na wenye ushawishi ndani ya chama na Taifa. Napendekeza mtu kama Prof. Baregu au Prof. Safari. Kwa mujibu wa waraka ule wa mkakati wa Mabadiliko ziko tuhuma za kijinga lakini pia yako mapungufu ya ukweli ambayo kama ni kweli, mwenyekiti wa sasa anapaswa kupumzika na kuwa miongoni mwa washauri wakuu wa chama. Pia, pamoja na mapungufu kadhaa ya ZZK, kwa muktadha wa hali halisi ilivyo, ni afya kwa chama kama atakatazwa pia kutafuta huo ufalme kwa wakati huu. Wote wanagombania uwenyekiti na kusababisha mpasuko, tuwaadhibu kwa kuwanyima wote fursa hiyo. Lakini kabla ya adhabu, wajipime wenyewe na waone kama nini ni Zaidi kati ya wao kuwa wafalme na mustakabali wa chama na Taifa.

7. NYUFA ZIZIBWE HARAKA
Kuna jambo zuri sana limeibuliwa na huu waraka wa ‘kisaliti' wakati tunawaadhibu wahusika tusijifanye hatuyaoni yaliyoandikwa. Jaribio lolote la kujifanya kufunika, kujisahaulisha au ‘kupotezea' yali yaliyomo kwenye waraka ni hadithi ya mficha maradhi tu na kifo kitamuumbua. Habari za udini, ukanda na ukabila zimepigiwa makelele muda mrefu sana.Wenye wakili tunajua kuwa hizo ni propaganda mfu, lakini si vema kuzipuuzia, uandaliwe mkakati wa kuzikabili na kuzifafanua kwa kurudia rudia mpaka zife kabisa.

Habari za matumizi mabaya ya fedha bado hazijapatiwa majibu. Tuleteeni majibu, hata kama ni ya kisiasa. Mtu akisema mnafuja pesa nanyi mkajibu "Buku7 za Lumumba", wenye akili tunajua kuna kitu kinafichwa. Tunataka majibu ya kusayansi, wekeni hadharani taarifa za fedha, toeni ufafanuzi wa masuala na hisia zote zinazohusu matumizi ya pesa. Kama kuna wanaodhani mwenyekiti au katibu ni wababe hao nao wanapaswa kuridhishwa vinginevyo. Kwa ufupi ni kwamba, hakikisheni mnajibu kila hoja kwa utaalamu na ustadi wa hali ya juu, kuondoa chembe ya shaka na kusimika uwazi, usafi na uimara wa mwenendo wa tabia zenu kama watu na kama chama kikuu cha siasa.

HITIMISHO
Wakati naandika Makala ile ya "CHADEMA MMELEWA SIFA":…Nilipokea simu, email na sms zisizo na idadi. Wengi wakipongeza na wengine wakiniponda. Feedback zao zilinitia moyo na kunifundisha mambo mengi makubwa. Kuna waliohusianisha makala ile na Buku7 za Lumumba, lakini baada ya Tukio la kuvuliwa uongozi Zitto na Kitila wengi wa walionitukana sasa wanakubaliana na mantiki ya makala ile. Sijatumwa na mtu na sitatumwa, ninaandika kwa utashi kamili kama binadamu na hasa kama Mtanzania ninayesoma kwa kodi ya masikini wa Tanzania. Kila mwenye akili timamu, atapenda kuona Demokrasia inakua na kushamiri Tanzania. Ni lazima kutumia kila fursa kutoa mchango katika ukuaji wa demokrasia. Tunayoandika yanabaki kuwa ushahidi wa kihistoria kwa kizazi cha sasa na cha baadaye. Watoto wangu na wajukuu zangu watajifunza na kuthamini matumizi bora ya kipawa cha akili na mawazo katika kusukuma ari ya watu kujitambua, kujitawala na kujiletea maendeleo endelevu.

Kada maafuru wa CCM, Musfafa Sabodo amekuwa akichangia mamilioni CHADEMA, wengie wanamshangaa na wanapomuuliza jibu lake ni rahisi sana "Ninasaidia ukuaji wa demokrasia, nikiamini ukuaji wa uchumi na hali za kijamii za watanzania utatokana na kiwango cha ukuaji wa demokrasia." Kwa sababu hiyo, kila mwenye kuitakia mema Tanzania, kila mwenye ndoto za maisha bora, kila mwenye kudhani anataka kuchangia maendeleo ya nchi yetu, maji safi, barabara, huduma bora za afya, kupambana na rushwa, ufisadi na uwajibikaji....basi atoe mchango wake katika kukuza demokrasia.

Sio siri tena, kwamba uwajibikaji tunaoshuhudia hivi sasa wa serikali ya CCM kwa kiwango cha kuwafanya wajidai kuwa wanacho cha kuwaonyesha wapiga kura unatokana na msukumo wa ukuaji wa demokrasia, kwamba vyama vya siasa vinapiga kelele, asasi za kiraia ziko macho na wananchi wameamka! Huu ndio ustaarabu na huu ndio ukombozi wa kweli. Bila upinzani imara, hakuna Maendeleo, huu ni ukweli wa kisayansi!

Mwandishi wa Makal hii ni Mtafiti, Mwanasosholojia na Mtaalamu wa uandishi, uandaaji na usimamizi wa Miradi. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Mwaka wa tatu Shahada ya Sheria, Pia ni Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro.(MUSO-SECRETARY GENERAL).Anapatikana kwa Email: rlengeju@gmail.com Simu # 0715901001 au 0762341522
 
palalisote

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Messages
8,340
Points
0
palalisote

palalisote

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2010
8,340 0
mjadala umefungwa. jamii ya akina nyakarungu hii toka mzumbe.
 
Mandown

Mandown

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2012
Messages
1,668
Points
1,250
Mandown

Mandown

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2012
1,668 1,250
Hivi yule mheshimiwa anaye shikishwa ukuta mbona haja toa tamko lolote toka sakata la uasi lianze .... manake yeye ndiomuanzilishi wa hoja ya unafiki
 
K

Kabale Ndagalu

Member
Joined
Nov 22, 2013
Messages
5
Points
0
K

Kabale Ndagalu

Member
Joined Nov 22, 2013
5 0
Mimi pia nimeguswa sana na kinachoendelea CDM, kusema ukweli kufa kwa chadema hata mwana CCM makini hawezi kufurahia.
CDM ni chama cha watanzania ,niliwahi kufanya kazi na watu kutoka USA, hata kama mtu ni Republican/Democrats hawezi kuota wala kuwaza eti chama kimojawapo kife kwa maanufaa ya chama chake,mmoja alinitolea mfano wa kutupa T shirt kwa sababu umepata shart,kwa maana yeye anaamini kila nguo itafaa kwa wakati na majira furani.
Nimefarijika sana na makala yako bwana Lengeju,ni makala iliyojaa kila chembe ya Utanzania na upeo wa kuionea huruma hii nchi,maana anaye ionea huruma nchi hii ni sharti awe na maono ya kukomaza Demokrasia.

Ni kweli usio pingia kuwa binadamu tumeumbwa kwa kutofautia mmoja na mwingine,ili maisha yaende ni sharti tukabali usemi usemaosema (give and take).

Haiwezekani tukubaliane kwa kila jambo,na ukikuta watu wanakubaliana kila jambo,fuatilia huenda watakuwa na matatizo ya kufikiri,nadiriki kusema huenda ni majuha.Maana haiwezekani watu wote watano mfano mukubaliane kwa kila kitu,haiwezekani,ila watu wenye busara hukubali pia mawazo pinzani/kinzani na wao.

Mfano mimi ni Dr wa magojwa ya binadamu,nawaza namna gani mgonjwa anaye umwa ugonjwa fulani nitamtibuje,mwingine ni engineer anawaza hivi atapitisha umeme kwenye maji ufike Zanzibar. Laiti hawa wote wangewaza kitu kimoja hakika maisha yangekuwa majanga,dunia ingekuwa sehemu mbaya kabisa kuishi,lakini kwa kuwa binadamu tunatofautiana kuna vitu anuwai vinaendelea kwa wakati mmoja.

Hivyo mimi ni muumini mkuu wa kuamini kila fikira/wazo au mtizamo furahi unahiji kuangaliwa kwa umakini mkubwa pengine unaweza kuwa ndo mwanzo wa kitu kimoja bora kabisa,ili mradi umepewa nafasi ,umepata tafakuri ya kina na kuja na ufafanuzi wenye kuonesha mlengo hasi na chana na watu ambao hawana mlengo fulani ili kutendea haki wazo/mtizamo fulani.Ikidhihirika kuwa si bora kwa wakati wowote au kwa wakati huu au wakati fulani,pia mwenye wazo akubali au aende ajipange upya kwa maana ya kuboresha zaidi,au atafute namna nyingine ya kuwasirsha mawazo yake apate kueleweka maana pingine hakueleweka vizuri,ila asitumie nguvu au jadhiba kuladhimisha anachoamini.

Mh ZZK na wenzie pamoja na Viongozi wa chadema walioko madarakani hasa Mwenyekiti wetu mpendwa Freemani Mbowe kama kweli wanapenda maendeleao na uhai wa demokrasia changa ya nchi yetu ,niwaombe tu wasome makala ya huyu bwana hasa hatua ya kwanza,ya sita na ya saba.

Kijana amejitahidi sana kuchambua bila kuegemea upande wowote,binafsi nakubaliana naye mia kwa mia.Tofauti zetu sizizime doto ya vijana wa kitanzania.

Pia naomba niwaonye wana chama wa chama pinzani na CDM kama kweli wako nyuma ya mipango hii ovu,hawako salama maana dhambi hii ni kubwa kuliko ufisadi,hela zinatafutwa ila demokrasia hainunuliwi kwa pesa wala thamani yake haipo.

Litakuwa jambo la ajabu sana eti mtu kuwa CCM anafanya mipango ya kuua chama kingine tena kwa kodi zetu,ni dhambi ambayo huwezi kutubu ukapata msamaha.

Kwa hili naomba Rais Kikwete aingilie kati,pamoja na mambo mengi anayozushiwa Mkuu wa nchi yetu sijaona akiwa msitari wa mbele kuhanisi demokrasia ya nchi yetu.
Naamini anayo nia thabiti ya kuona emokrasia ya nchi yetu inakua kuliko wakati wowote wa uhai wa Taifa hili changa,hivyo sidhani wala siamini kama anaweza kuruhusu hela za kodi zitumike kunajisi demokrasi kiasi hiki.

Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania
 
G

Guturo

Member
Joined
Sep 14, 2013
Messages
15
Points
20
G

Guturo

Member
Joined Sep 14, 2013
15 20
Mungu baba muweza wa yote hebu wafunulie hawa wana wako walau waweze kung'amua hiki kilichofafanuliwa na huyu ndugu. Personally naikubali makala hii.
 
tofyo

tofyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Messages
2,685
Points
1,500
tofyo

tofyo

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2013
2,685 1,500
naomba ufafanuzi juu ya kitila mkumbo.
_ ali kiri makosa gani?
_ali kubali kuratibu na kuandika waraka?
_alikiri kutengeneza mparaganyiko wa chama?
Embu naomba upembuzi yakinifu juu ya kile kinachosemwa kuwa mkumbo ali kiri.
Na kwa kuongezea maadam wewe umeruka kesi ya uhaini wa zitto na mkumbo basi tukubali kuwa alicho kifanya zitto na mkumbo ni kukubali yaishe kwa wakati ule ili kuepusha malumbano
labda niseme bila uwoga kwamba zitto na mkumbo hawana hatia yoyote, na kama wataendelea kuwatuhumu kuwa niwahalifu wa chama. ni kwamba hii vita ya maneno majukwaani haito isha na mwisho wa siku itabaki tukose wote.
 
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,777
Points
1,195
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,777 1,195
naomba ufafanuzi juu ya kitila mkumbo.
_ ali kiri makosa gani?
_ali kubali kuratibu na kuandika waraka?
_alikiri kutengeneza mparaganyiko wa chama?
Embu naomba upembuzi yakinifu juu ya kile kinachosemwa kuwa mkumbo ali kiri.
Na kwa kuongezea maadam wewe umeruka kesi ya uhaini wa zitto na mkumbo basi tukubali kuwa alicho kifanya zitto na mkumbo ni kukubali yaishe kwa wakati ule ili kuepusha malumbano
labda niseme bila uwoga kwamba zitto na mkumbo hawana hatia yoyote, na kama wataendelea kuwatuhumu kuwa niwahalifu wa chama. ni kwamba hii vita ya maneno majukwaani haito isha na mwisho wa siku itabaki tukose wote.
Hakuna cha kukosa wote wala nini, wao waende huko kwa wenye mahaba nao, wote tumeshuhudia wanao kuja kuwatetea na kulia lia kwamba hawajatendewa haki ni kinanani? Hivi hata kama una ubongo mdogo kama wa kuku huwezi kujiuliza kulikoni jirani kulia hadi kuzimia kwa ajili ya msiba wa mchumba wako?
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,596
Points
2,000
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,596 2,000
Hillarious indeed....!

Yaani Mbowe anyimwe haki yake ya kikanuni,kikatiba na kidemokrasia kwa sababu ameongoza kikao kilichowaadhibu wasaliti?

Yes,CHADEMA ina watu wengi.Wapo akina Lissu na wengine wenye misimamo isiyotiliwa shaka lakini haiwezi kuwa hoja ya kumnyima Mbowe nafasi ya kugombea
 
Isalia

Isalia

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
1,045
Points
1,250
Isalia

Isalia

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
1,045 1,250
Uchambuzi ni mzuri ila hapa penye kifungu kuwa mbowe na zitto wasigombee wengi utawatanza ingawa pana ukweli
 
kelvin complex

kelvin complex

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
558
Points
500
kelvin complex

kelvin complex

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
558 500
yan Mungu katuumba tofauti sana yan kunabaadhi ya wa2 akili zao cjui zkovp, anapotokea m2 anaeandika mambo mazur na muhimu kwa ustawi wa demokrasia ya nchi na chama(cdm) wao huwa mstari wa mbele kucreticize,bila hata hoja ya msingi, tubadilike jamani, sio kila wakati lazima uchangie mada kama ur pointless
 
luhala

luhala

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Messages
412
Points
0
luhala

luhala

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2012
412 0
Sijapata kusoma andiko lililosheheni busara kama hili tokea kuanza kwa sakata hili tete na nyeti kwa ukuaji wa demokrasia nchini mwetu. Hakika mwandishi huyu anastahili heshima. Ameweka mizania sawa katika kila kipengele alichokijadili, na ametoa mapendekezo mujarab kwa tatizo hili tete.
 
Karikenye

Karikenye

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
565
Points
195
Karikenye

Karikenye

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
565 195
With due respect you are PRO ZITTO! Baregu pia ni PRO ZITTO! Dr Lweitama ni Neutral, Prof Safari ni PRO ZITTO pia! All in All CCM hawamtaki MBOWE kwenye Chair kwa sababu chini ya uongozi wake CHADEMA wamefanikiwa sana! Ni rahisi tu CHADEMA imejengwa na watu ambao katika biashara zao wamefanikiwa hivyo misingi ya uongozi wanaijua maana wanaitumia kila siku kwenye biashara zao ambazo zimefanikiwa!!
 
L

LENGEJU BOB

Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
53
Points
0
L

LENGEJU BOB

Member
Joined Nov 1, 2010
53 0
Sijapata kusoma andiko lililosheheni busara kama hili tokea kuanza kwa sakata hili tete na nyeti kwa ukuaji wa demokrasia nchini mwetu. Hakika mwandishi huyu anastahili heshima. Ameweka mizania sawa katika kila kipengele alichokijadili, na ametoa mapendekezo mujarab kwa tatizo hili tete.
Umenigusa, umenitia Moyo...Asante
 
M

Mwihadisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
608
Points
195
M

Mwihadisa

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2012
608 195
Kaka, heshima yako. Binafsi si Mwana Chadema ila ni mfuasi wao mkubwa. Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo nakiri sijawahi kuiona makala iliyochambua mgogoro huu na kujaribu kutoa suluhu kama ulivyofanya wewe. Niseme tu Zitto na Kitila wana makosa makubwa lakini yaliyoandikwa kwenye huo waraka yapo yenye ukweli ndani yake.

Nashauri makala yako hii isambazwe kwenye magazeti hasa ya Jumapili na Jumatano ili Watanzania walau sasa baada ya kusikia malumbano ya pande mbili kwa muda mrefu sasa wasome mawazo ya watu wanaotafuta suluhu katika mgogoro huu.

Hili la Mbowe na Zitto kuzuiwa kugombea lilipaswa kuwa la kwanza kwa sababu inaelekea ndio kiini ch mgogoro huu. Wanaosema Mbowe ana hakiya kugombea wajiulize kwanini Zitto alishauriwa ajiondoe mwaka 2009 na akakubali? Kama nia ni kujenga chadema imara kuelekea 2015 ni vizuri watu wakajifunza ku sacrifice baadhi ya mambo.
 
salmar

salmar

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
799
Points
250
salmar

salmar

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
799 250
Sultan mbowe na mtakatifu mchukua wake za watu na ww mbeba sumu naliona anguko lenu
 

Forum statistics

Threads 1,402,876
Members 531,004
Posts 34,407,781
Top