Mimi pia nimeguswa sana na kinachoendelea CDM, kusema ukweli kufa kwa chadema hata mwana CCM makini hawezi kufurahia.
CDM ni chama cha watanzania ,niliwahi kufanya kazi na watu kutoka USA, hata kama mtu ni Republican/Democrats hawezi kuota wala kuwaza eti chama kimojawapo kife kwa maanufaa ya chama chake,mmoja alinitolea mfano wa kutupa T shirt kwa sababu umepata shart,kwa maana yeye anaamini kila nguo itafaa kwa wakati na majira furani.
Nimefarijika sana na makala yako bwana Lengeju,ni makala iliyojaa kila chembe ya Utanzania na upeo wa kuionea huruma hii nchi,maana anaye ionea huruma nchi hii ni sharti awe na maono ya kukomaza Demokrasia.
Ni kweli usio pingia kuwa binadamu tumeumbwa kwa kutofautia mmoja na mwingine,ili maisha yaende ni sharti tukabali usemi usemaosema (give and take).
Haiwezekani tukubaliane kwa kila jambo,na ukikuta watu wanakubaliana kila jambo,fuatilia huenda watakuwa na matatizo ya kufikiri,nadiriki kusema huenda ni majuha.Maana haiwezekani watu wote watano mfano mukubaliane kwa kila kitu,haiwezekani,ila watu wenye busara hukubali pia mawazo pinzani/kinzani na wao.
Mfano mimi ni Dr wa magojwa ya binadamu,nawaza namna gani mgonjwa anaye umwa ugonjwa fulani nitamtibuje,mwingine ni engineer anawaza hivi atapitisha umeme kwenye maji ufike Zanzibar. Laiti hawa wote wangewaza kitu kimoja hakika maisha yangekuwa majanga,dunia ingekuwa sehemu mbaya kabisa kuishi,lakini kwa kuwa binadamu tunatofautiana kuna vitu anuwai vinaendelea kwa wakati mmoja.
Hivyo mimi ni muumini mkuu wa kuamini kila fikira/wazo au mtizamo furahi unahiji kuangaliwa kwa umakini mkubwa pengine unaweza kuwa ndo mwanzo wa kitu kimoja bora kabisa,ili mradi umepewa nafasi ,umepata tafakuri ya kina na kuja na ufafanuzi wenye kuonesha mlengo hasi na chana na watu ambao hawana mlengo fulani ili kutendea haki wazo/mtizamo fulani.Ikidhihirika kuwa si bora kwa wakati wowote au kwa wakati huu au wakati fulani,pia mwenye wazo akubali au aende ajipange upya kwa maana ya kuboresha zaidi,au atafute namna nyingine ya kuwasirsha mawazo yake apate kueleweka maana pingine hakueleweka vizuri,ila asitumie nguvu au jadhiba kuladhimisha anachoamini.
Mh ZZK na wenzie pamoja na Viongozi wa chadema walioko madarakani hasa Mwenyekiti wetu mpendwa Freemani Mbowe kama kweli wanapenda maendeleao na uhai wa demokrasia changa ya nchi yetu ,niwaombe tu wasome makala ya huyu bwana hasa hatua ya kwanza,ya sita na ya saba.
Kijana amejitahidi sana kuchambua bila kuegemea upande wowote,binafsi nakubaliana naye mia kwa mia.Tofauti zetu sizizime doto ya vijana wa kitanzania.
Pia naomba niwaonye wana chama wa chama pinzani na CDM kama kweli wako nyuma ya mipango hii ovu,hawako salama maana dhambi hii ni kubwa kuliko ufisadi,hela zinatafutwa ila demokrasia hainunuliwi kwa pesa wala thamani yake haipo.
Litakuwa jambo la ajabu sana eti mtu kuwa CCM anafanya mipango ya kuua chama kingine tena kwa kodi zetu,ni dhambi ambayo huwezi kutubu ukapata msamaha.
Kwa hili naomba Rais Kikwete aingilie kati,pamoja na mambo mengi anayozushiwa Mkuu wa nchi yetu sijaona akiwa msitari wa mbele kuhanisi demokrasia ya nchi yetu.
Naamini anayo nia thabiti ya kuona emokrasia ya nchi yetu inakua kuliko wakati wowote wa uhai wa Taifa hili changa,hivyo sidhani wala siamini kama anaweza kuruhusu hela za kodi zitumike kunajisi demokrasi kiasi hiki.
Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania